Mtazamo chanya na tabia nzuri zitakuwezesha kufikia mafanikio makubwa. Fikra zako zinazotokana na mtazamo wako ndizo zitakazokufanya uweze kufanikiwa au ushindwe kufanikiwa.
Fikiria mambo madogo na utakuwa mtu mdogo, fikiria mambo makubwa na utakuwa mtu mkubwa kama ukitenda yale unayofikiri.
Mtu mwenye mtizamo sahihi haonyeshi tu kufanikiwa bali hufikia mafanikio makubwa sana. Maisha yao, matendo yao na hata maneno yao huonesha ni watu wa mafanikio. Kwa tabia hii huweza kuwavutia wengi zaidi na hivyo kuweza kufikia mafanikio makubwa.
Je mtazamo, tabia au mawazo yanaweza kujengwa?
Kama tulivyosema kwamba ili kufikia mafanikio makubwa ni lazima kuwa na mtizamo, tabia na hata mawazo sahihi. Na tabia hutokana na mtizamo na mawazo. Hivyo je unaweza kujenga mtizamo na mawazo sahihi? Hiki ni kitu ambacho kinawezekana na hata wewe unaweza kukifanya kuanzia sasa.
Unaweza kutengeneza mtazamo na mawazo chanya kwa kuzingatia yafuatayo;
1. Tengeneza mtizamo wa kwamba unajipenda na kupenda wengine.
2. Tengeneza mtizamo kwamba wewe ni mtu wa pekee na kila unayekutana naye ni mtu wa pekee.
3. Tengeneza mtizamo kwamba umejawa na shauku.
4. Tengeneza mtizamo kwamba umejawa na kujiamini.
5. Tengeneza mtizamo kwamba nafurahi kukusaidia wewe
6. Tengeneza mtizamo kwamba wewe na kila unayekutana naye ni mtu muhimu.
Tengeneza mitizamo hii na itumie kila siku na utaona mabadiliko makubwa kwenye maisha yako.
Umuhimu wa kujiona wewe ni muhimu.
Wewe kama ilivyo kwa watu wengine wote unahitaji kujiona ni muhimu na pia unahitaji kujiona unakubalika. Watu wengine wanakutambua kwa vile ulivyo na vile unavyoweza kufanya, na kama unahitaji kuwa tofauti ni lazima uwe na mtizamo wa mafanikio zaidi. Lazima uoneshe mafanikio ili wangine waweze kuvutiwa na wewe. Ni lazima uoneshe uongozi ili wengine wawe na uhakika kupitia wewe wanaweza kupata kile wanachohitaji. Ni katika hali hii ya uaminifu na uongozi ambapo unaweza kupata wafuasi wengi na kama unafanya biashara ukawa na wateja wengi sana watakaokupelekea kufikia mafanikio makubwa. Mtu ambaye anajiona ni muhimu anaweza kuwafanya wengine kuwa muhimu na hivyo kujenga nao uhusiano mzuri. Anza kujiona muhimu sasa.
Mafanikio na shauku.
Ili uweze kuwahamasisha wengine wakusaidie wewe kufikia mafanikio makubwa ni lazima uweze kujihamasisha mwenyewe kwanza. Ili uweze kufikia mafanikio makubwa ni lazima ujenge mtizamo wa kuwa na shauku kwa kile unachokifanya na kwa wale unaokutana nao. Shauku hii itawapa watu nguvu ya kuweza kwenda na wewe katika kile unachotaka wafanye.
Unawezaje kuhamasika na kuhamasisha wengine?
1. Onesha mawazo yako na jioneshe wewe mwenyewe.
Tumia kila nafasi unayopata kutengeneza picha kubwa ya kile unachofikiri na jinsi kinavyoweza kuwasaidia wengine. Onesha utu wema, uaminifu na urafiki. Toa bila ya kutegemea kupokea na wafanye watu wajisikie vizuri kukutana na wewe. Wasifie watu pale inapostahili na onesha kujali kile wanachofanya au walichofanya.
2. Usihukumu kwa kuona mara moja.
Unapokutana na mtu mara ya kwanza usifanye majumuisho kutokana na ulivyomuoan au ulichoona anafanya au kusema. Mjue mtu vizuri na tengeneza uhusiano mzuri na urafiki pia.
3. Angalia zaidi kwa kila mtu na kila kitu.
Katika kufikia mafanikio unahitaji watu, iwe ni wateja, washirika au hata wafanyakazi. Hakikisha unamjua vizuri kila mtu ambaye unahusiana nae kwa namna moja au nyingine. Jua ni vitu gani anapendelea, jua ana udhaifu gani, jua ana kipi ambacho unaweza kukitumia na pia jua kuna kipi ambacho mnaweza kushirikiana. Kama ni mteja jua hitaji lake hasa na jinsi gani unaweza kulitimiza, utatengeneza wateja wengi sana kwa njia hii.
4. Ona mazuri kwa kila mtu na kwa kila kitu.
Weka utaratibu wa kutokujumuisha kwamba kitu fulani au mtu fulani ni mbaya kabisa na hafai. Katika hali yoyote au mtu yoyote hata awe mbaya kiasi gani kuna kitu kizuri unachoweza kunufaika nacho. Tafuta ni kipi kizuri ambacho kinaweza kukunufaisha na angalia ni jinsi gani unaweza kukitumia kufikia mafanikio makubwa.
5. Ongea mazuri wakati wote.
Popote unapokuwa na chochote unachofanya usijihusishe na kuongea maneno mabaya juu ya kitu au watu. Usiwe mtu wa kubeba habari mbaya au kuwakatisha wengine tamaa. Usiseme uongo, usisengenye na wala usisambazo umbea. Kuwa msambazaji wa habari nzuri, kuwa mtu wa kuwafariji wengine na kuwatia moyo na utakuwa rafiki wa wengi.
6. Jali watu wengine.
Moja ya njia za kukuwezesha kufikia mafanikio makubwa ni kujali watu wengine. Kila mara usifikirie kuhusu wewe tu na jinsi utakavyofikia malengo yako. Mara zote fikiria wale wanaokuzunguka na ni jinsi gani wanaweza kunufaika kupitia wewe. Kama unafanya biashara fikiria ni jinsi gani mteja wako atanufaika au maisha yake kuwa bora kwa bidhaa au huduma unayokwenda kumpatia. Kwa njia huu utawasaidia wengi na utajenga uhusiano mzuri ambao utakuwezesha kufikia mafanikio makubwa.
7. Wape moyo wengine.
Kila binadamu anapitia wakati mgumu katika kipindi fulani. Kuwa mtu wa kuwapa watu moyo na hata kuwahamasisha pale wanapoona mambo ni magumu na hawawezi tena. Kwa njia hii utawasaidia wengi na wao pia watakusaidia wewe kuweza kufikia malengo yako.
Tumia mbinu hizi na ujenge mtizamo na mawazo chanya kwa kile unachofanya na kwa kila unayekutana naye. Tengeneza uhusiano mkubwa na watu wengine na uhusiano huu utakuwezesha kufikia mafanikio makubwa.
Nakutakia kila la kheri katika safari ya kufikia mafanikio makubwa. Karibu kwenye FORUM YA SIKU 30 ZA MAFANIKIO ili tuweze kuendelea kujadiliana.(bonyeza hayo maandishi kuingia kwenye mjadala)
TUKO PAMOJA.
MUNGU IBARIKI AMKA MTANZANIA,KISIMA CHA MAARIFA NA PIA WA KUMBARIKI ZAIDI NI AMANI MAKIRITA AMINA.
LikeLike
Asante sana Jacqueline,
TUKO PAMOJA.
LikeLike