Wiki chache zilizopita tuliweka makala ya kijana wa kitanzania aliyeanza biashara na mtaji wa milioni nne na baada ya miaka mitatu ana zaidi ya milioni mia moja. Kama hukupata nafasi ya kusoma makala hiyo bonyeza hayo maandishi.

Katika makala ile tulipata kwa ufupi historia ya John Matiku na niliahidi kwamba John ataendelea kutushirikisha mbinu mbalimbali alizotumia kufikia mafanikio haya makubwa. Kwa ahadi hiyo, leo unapata makala moja wapo na nyingine zitaendelea kukujia hapa hapa AMKA MTANZANIA hivyo endelea kutembelea kila siku.

Leo John anatushirikisha jinsi ubunifu kidogo ulivyobadili mwelekeo wa biashara yake.

Ndio nasubutu kusema ni ubunifu kidogo kwakua nilicho kibuni kipo! Kama nilivyoeleza kwenye makala yangu ya kwanza, kuwa mwanzo biashara ilikua ngumu sana na ugumu huo ukageuka fursa ya soko kubwa lenye wateja marafiki ambao tunasafiri pamoja mpaka leo. Leo ninakusudia kukueleza wazo zima lilivyoanza. Hii ndio siri ya kazi na biashara nyngi duniani, UBUNIFU, na wamiliki wengi hawawezi kuisema siri hii maana wanaamini wakikwambia na wewe utafanya kama wao. Lakini mtazamo wangu sio huo ndio maana hapa nimeamua kukueleza siri hii ya kunitoa 4.6m hadi 100M.

magori

Nilipoona hali ni mbaya na nilicho nacho mkononi ni bidhaa hizo ambazo thamani yake ni hyo hapo juu nilifikili mbinu mbadala ya kuziuza kwa wateja. Nilijiuliza maswali yafuataya  kabla ya kuamua kufanyia kazi ubunifu wangu;

1. Je bidhaa zangu ni mbaya kiasi kwamba zisinunuliwe?
2. kauli yangu haitoshi kumshawishi mteja anunue?
3. Nini kinachozuia wateja wanaouliza bei na kufanya “window shopping” dukani kutonunua?

Nikajijibu mwenyewe kua bidhaa zinahtajika na ushawishi wa wateja ninao, isipokua huenda wateja hawajaniamini. Na zaidi huenda wengi wao hawana fedha kipindi wanapolitembelea duka langu. Ndipo nikaamua kuja na wazo la kuwakopesha kwa masharti nafuu nikiwa na malengo mawili kichwani;
1.kusaidia upatikanaji wa mzunguko kwenyebiashara

2.kujijengea wateja wa kudumu wa bidhaa zangu.

Malengo ambayo yote yalifanikiwa kwa kiwango kikubwa sana.

KUKOPESHA SI UBUNIFU MKUBWA maana sote tunajua kuwa mikopo ya vifaa ipo na zipo kampuni zilizosajiliwa rasmi kutoa mikopo na ndio maana nasema ni UBUNIFU KIDOGO TU.

Kwangu tofauti na watu wengi walivyo “ubunfu ni mpango utakaotekelezwa na kumletea mtu ukombozi wa athari zinazomzonga yeye na wenzake. Hivyo ubunifu hauna maana yoyote kama haujawekwa kwenye matendo ukatoa matunda yanayokusudiwa”

Hivyo baada ya kuliafiki wazo hilo ilinibidi kuandaa mpango wa kulitekeleza wazo hilo mara moja ilinibidi kuchangua watu nitakao anza nao na mbinu za kuwakopesha ili wanilipe kwa uamifu bila kuingia gharama kubwa za kisheria na za kumdai mteja. Hivyo niliamua kuandaa mpango wa jinsi gani nitawatambua wateja wangu na nitawafikishiaje taarifa lakin pia nitawakopeshaje kile wanachokitaka na watanijlipaje muda utakapowadia wakunilipa. BAADA ya hapo nikatekeleza mpango wangu hatua kwa hatua na ikanisaidia kufikia hapa leo.

Mwisho naomba ujue kua BIASHARA lazima ibadilike kulingana na hali, hauwezi kufanikiwa kwa kulazimisha mfumo huohuo ulionao si lazma njia hiyohiyo waliyopita wengine ndio na wewe uipite weka ubunifu kidogo tu! Na utaona matokeo Makubwa na usioyatalajia.

Nakutakia kila la kheri kwenye mafanikio ya biashara yako.

TUKO PAMOJA.