Mambo Matatu Ambayo Ni Muhimu Kila Mtu Kujifunza Na AUDIO BOOKS Za Kujifunzia.

Katika kitu kimoja ambacho kila mmoja wetu anakitafuta kwenye maisha ni mafanikio. Haijalishi umeajiriwa, umejiajiri au unafanya biashara, unapenda siku zijazo uwe na mafanikio kuliko ulivyo leo. Unataka siku za mbeleni uwe na kipato kikubwa kuliko unachokipata sasa na pia unapenda mbeleni uwe na ushawishi mkubwa kuliko ulionao sasa.

Pamoja na kuwa kila mtu anapenda vitu hivyo bado ni wachache sana ambao wanafanya juhudi za dhati kufikia huko. Ndio namaanisha wewe unapenda kufikia mafanikio lakini hufanyi juhudi zozote za kukufikiasha kwenye hayo mafanikio. Au juhudi unazofanya hazina tija kwa wewe kubadilika.

Linapokuja swala la kufikia mafanikio makubwa, watu wengi hasa waajiriwa hufikiria kufanya kazi kwa bidii ndio suluhisho. Hivyo huongeza juhudi kwenye kazi na wakati mwingine kuchukua kazi ya ziada. Pamoja na yote haya bado mambo yanaendelea kuwa magumu. Tatizo ni nini?

Leo utajifunza mambo matatu muhimu unayotakiwa kujifunza ili uweze kufikia mafanikio kwa chochote unachofanya. Pia utapata AUDIO BOOKS zenye vitabu utakavyoweza kujifunzia mambo hayo matatu.

1. Jifunze jinsi ya kuuza(sales).

Kila mmoja wetu anauza, uwe umeajiriwa au unafanya biashara kuna kitu unauza. Kama umeajiriwa unauza muda wako na utaalamu wako kwa mwajiri wako. Kama unafanya biashara unauza bidhaa au huduma. Kama ni kiongozi au mwanasiasa unauza sera na mawazo yako. Kwa vyovyote vile unahitaji kujifunza jinsi ya kuuza muda, huduma, bidhaa na hata mawazo yako vizuri ili uweze kufanikiwa kupata kile unachotaka.

2. Jifunze mbinu za mawasiliano(communication skills).

Mawasiliano ni kitu cha msingi sana kwenye maisha yetu. Jinsi unavyozungumza na mtu ana kwa ana, kwenye simu na hata kutumia maandishi ina mchango mkubwa sana katika kumshawishi mtu huyo. Unaweza kumshawishi mtu yeyote hata awe mgumu kiasi gani kama utajifunza na kujua mbinu za mawasiliano bora.

3. Jifunze jinsi ya kukubaliana(negotiation).

Katika maisha ya kila siku, kwenye familia, kazi na hata biashara kuna wakati tunakuwa tunapishana mawazo na watu wengine. Lakini watu hawa ambao tunapishana nao mawazo ni muhimu sana kwetu ili kuweza kufikia mafanikio. Katika wakati kama huu unahitaji kujua mbinu za ushawishi na kukubaliana ili uweze kumshawishi mtu mliyepishana nae mawazo aweze kukubaliana na mawazo yako. Na pia wakati mwingine unatakiwa kuwa na makubaliano ambayo pande zote zitafaidika.

Hivyo ni vitu vitatu muhimu sana ambavyo kila mtu anatakiwa kujifunza ili kuweza kufikia mafanikio kwenye kitu chochote anachofanya.

Unawezaje kujifunza vitu hivi?

Kama nilivyosema, kuna uwezekano mkubwa sana kwamba hujawahi kufanya juhudi za makusudi za kujifunza vitu hivi muhimu. Leo utapata nafasi nzuri ya kuweza kujifunza vitu hivi muhimu.

Nimeandaa memory kadi yenye AUDIO BOOKS(vitabu vya kusikiliza) ambapo unaweza kujifunza vitu hivi kwa kusikiliza. Unaweza kutumia memory kadi hiyo kwenye simu, gari, kompyuta au kifaa chochote kinachokubali memori kadi. Memory Kadi hii ina ukubwa wa 4GB na ina vitabu 21.

VITABU VILIVYOPO KWENYE MEMORY CARD YA 3

1. Brian Tracy – Become a Sales Superstar

2. Brian Tracy – Effective Manager Series – Marketing

3. Brian Tracy – Psychology Of Selling

4. Effective and persuasive communication – Steven K. Scott

5. Jim Rohn – Building Your Network Marketing Business

6. Made for Success – Persuasive Selling and Power Negotiation

7. Magnetic Marketing [Tony Robbins, T Harv Eker, Robert Kiyosaki, Bob Proctor]

8. Personal MBA Business Crash Course

9. Robert Kiyosaki – Sales dogs 3 CDs

10. SalesBible

11. The Greatest Salesman in The World – Og Mandino

12. Think and Grow Rich

13. Tom Hopkins & Laura Laaman – The Certifiable Salesperson

14. Unlimited Selling Power by NLP

15. Zig Ziglar – Secrets of Closing the Sale

16. Zig Ziglar – Sell Your Way To The Top

17. Becoming a Person of Influence – John C Maxwell

18. Running With the Giants Unabridged – John C Maxwell

19. Tom Hopkins-Avoiding the 10 biggest sales and marketing mistakes

20. Zig Ziglar – keys to closing

21. Zig Ziglar-Today-the first day of the rest of your life

Jinsi ya kupata memory kadi hii.

Memory kadi hii yenye vitabu hivi itatolewa ndani ya wiki hii na gharama ya kadi ni tsh 30,000/=. Kama upo dar es salaam utapatiwa kadi yako na kama uko mkoani utaongeza tsh 5,000/= kwa ajili ya usafiri na utatumiwa kadi yako huko uliko. Kupata kadi hii tuma fedha tsh elfu 30 kwa waliko dar na tsh elfu 35 kwa walioko mikoani kisha utaandaliwa kadi yako na kupatiwa mwisho wa wiki hii. Mwisho wa kutuma fedha ili kuandaliwa kadi ni ijumaa tarehe 03/10/2014. Wahi nafasi hii ya kipekee ya kuongeza ujuzi wako ili kuweza kufikia mafanikio makubwa.

Kama ulikosa memory card za nyuma unaweza kuziangalia hapa na kutuma fedha ili uandaliwe. Kutuma fedha, mpesa tuma kwenye namba 0755953887, tigo pesa au airtel money tuma kwenye namba 0717396253.

Nakutakia kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa.

TUPO PAMOJA.

kitabu-kava-tangazo432

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: