Hiki Ndio Kitu Kimoja Unachokosa Ili Kufanikiwa Na Hivi Ndivyo Utakavyokipata.

Umesoma na kuhitimu vizuri ila umetafuta kazi bila ya mafanikio yoyote.

Unafanyakazi sana lakini huoni maendeleo yoyote zaidi ya kusukuma siku na kulipa madeni.

Umefanya biashara kwa muda sasa aliki huoni biashara yako ikikua zaidi ya kupata tu hela ya kula.

Umejitahidi kubadili na kuboresha maisha yako lakini huoni mafanikio yoyote.

Hizi ni baadhi ya hali ambazo unaweza kuwa unazipitia au umewahi kuzipitia katika wakati mmoja kwenye maisha yako.

Kutokana na hali hizi zinazofanya maisha yako kuwa magumu unaweza kuwa umeshamlaumu kila mtu unayeweza kumfikiria.

Umeilaumu serikali kwa kukusomesha ila ikashindwa kukupatia kazi.

Unamlaumu bosi wako kwa kukosa utu na kushindwa kukulipa kile unachostahili ili maisha yako yawe bora.

Unalaumu uchumi, msimu, mamlaka za serikali kwenye kushindwa kupata mafanikio kwenye biashara zako.

Au unalaumu wazazi wako kwa namna fulani walivyochangia hapo ulipo.

Swali ni je, tokea umeanza kulaumu watu au vitu hivyo umepata suluhisho gani?

Ni kweli kwamba una matatizo mengi yanayoendelea kwenye maisha yako na kwenye kazi au biashara zako. Lakini tokea umeanza kulaumu umepata syluhisho gani? Miaka mitano iliyopita ulikuwa unalaumu hivyo hivyo kuhusu kazi yako lakini mpaka leo bado unaifanya na hakuna malalamiko makubwa.

Kitu Kimoja Unachokosa.

Kuna kitu kimoja unachokosa ndio maana unashindwa kupata mbinu nzuri za kuondoka kwenye matatizo yako. Kwa kukosa kitu hiki unajikuta ukiamini kwamba unachoweza kufanya wewe ni kulalamika tu na hivyo kuzidi kujiweka kwenye hali mbaya.

Kitu kikubwa unachokosa ni MAARIFA. Unakosa maarifa mapya na mengi ya kuweza kukutoa hapo ulipo. Kumbuka mameno haya; watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Ukosefu wa maarifa ndio chanzo kikubwa cha wewe kuendelea kuteseka na maisha haya.

Umesoma ila umekosa kazi, tatizo huna maarifa ya kujiajiri na kutengeneza ajira nyingi zaidi. Umefanya kazi kwa muda mrefu sasa lakini haikuridhishi, tatizo huna maarifa ya kukufanya uwe bora zaidi au ujiajiri.

Maarifa ninayozungumzia hapa sio lazima yawe yale ambayo umesomea au kufanyia kazi, kuna vitu kama nidhamu binafsi, elimu ya fedha na hata kujihamasisha pale mambo yanapokuwa magumu.

Ni muhimu sana wewe kupata maarifa haya ambayo yatakutoa hapo ulipo.

Unaweza kupata wapi maarifa haya.

Kuna sehemu nyingi za wewe kupata maarifa lakini kuna sehemu moja ambayo unaweza kupata maarifa ya kiwango cha juu sana. Na hii ni KISIMA CHA MAARIFA. Kwenye KISIMA utapata maarifa ya biashara na ujasiriamali, tabia za mafanikio, mbinu za mafanikio makubwa, uchambuzi wa vitabu na hata vitabu mbalimbali.

Kupitia KISIMA CHA MAARIFA utaanza kuona mwanga wa kule unakotazamia kufikia na utaweza kujifunza na kuhamasika ili kuelekea kwenye njia hiyo.

Kupata maelezo ya JINSI YA KUJIUNGA NA KISIMA CHA MAARIFA bonyeza maandishi hayo.

Chukua nafasi ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA leo na hutajutia maamuzi yako, tena kwa kiasi kikubwa utajilaumu kwa nini ulichelewa kujiunga.

Napenda sana wewe ufanikiwe kwa sababu najua ukifanikiwa na jirani yako nae atafanikiwa na hii itasambaa mwisho wa siku tutakuwa tumesaidia taifa zima kufanikiwa. Hii ndio sababu nimewekeza nguvu nyingi kwenye KISIMA CHA MAARIFA na kutoa mbinu zote zinazotumiwa na watu waliofanikiwa sana duniani. Usikose mbinu hizi ambazo zitabadili kabisa maisha yako.

Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya kufikia mafanikio.

TUKO PAMOJA.

P.S Ukijiunga na KISIMA leo utapata makala za siku 30 za mafanikio, uchambuzi wa kitabu cha RICH DAD POOR DAD na wiki ijayo tutaanza uchambuzi wa kitabu THE RICHEST MAN IN BABYLON. Pia utajifunza jinsi ya kujijengea nidhamu binafsi ambayo ndio msingi mkuu wa mafanikio.

Jiunge na KISIMA CHA MAARIFA ufaidi hayo yote ambayo yatakusaidia sana.

kitabu-kava-tangazo432

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: