USHAURI; Jinsi Unavyoweza Kuendelea Kuwa Na Hamasa Kubwa Kila Siku.

Karibu msomaji wa AMKA MTANZANIA kwenye kipengele cha ushauri wa changamoto mbalimbali zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Leo tutajadili changamoto ya kukosa hamasa mara baada ya kuanza kufanya kitu. Mara nyingi mtu unapopata wazo za kuanza kitu kipya aunakuwa na hamasa kubwa sana, lakini baada ya kuanza kitu hiko hamasa ile huisha na kama usipokuwa makini unaweza kujikuta unakata tamaa na kuacha kabisa kukifanya.

HAMASA

Kabla hatujaangalia ni kitu gani mtu unaweza kufanya ili kuondokana na hali hii ya kukosa hamasa, tupate maoni ya msomaji mwenzetu.

Changamoto yangu kuu ni kwamba, nakuwa na mudi ya kufanya jambo kwa kudhamiria, lakini badaa ya siku mbili hadi tatu hamu /hamasa ya kutekeleza maamuzi inapotea sijui ni kwanini, ila nazani ndo chanzo cha ‘Breaking the chain’. Nakosa mwendelezo wa fikra kwa ufupi!

Kama tulivyoona kwa msomaji mwenzetu hapo, hiki ni kitu ambacho kinatokea kwa watu wengi sana. Hata mimi kimewahi kunitokea mara nyingi na nina hakika hata wewe kimekuwa kinatokea.

Kuna mambo mengi unayoweza kufanya ili kuweza kuendelea kuwa na hamasa kubwa ya kufanya jambo uliyoanza nayo mwanzo. Hapa tutajadili mambo matano muhimu ambayo kila mtu anaweza kuyafanya na akaondokana na hali hiyo ya kukosa hamasa.

1. Weka malengo na mipango kabla ya kuanza kufanya jambo lolote.

Kila unapopata wazo la kufanya jambo jipya, unaweza kuwa na hamasa kubwa sana itakayokufanya ukimbilie kufanya jambo hilo bila ya kuwa na malengo au mipango yoyote. Hii inasababisha kufanya tu kwa msukumo wa hisia na hisia zile zinapokwisha unakosa kabisa msukumo wa kuendelea kufanya. Lakini kama utakaa chini na kuweka malengo na mipango, pale msukumo wa awali unapopotea unaweza kurejea kwenye malengo na mipango yako na kujua ni kipi unatakiwa kufanya ili kufikia malengo hayo.

2. Jiulize kwa nini ulianza kufanya jambo hilo.

Njia nyingine nzuri ya kurudisha hamasa ya mwanzo ni kujiuliza kwa nini ulianza kufanya jambo unalofanya. Kitu kikubwa kilichokupa hamasa ya kuanza jambo ni sababu fulani ambayo ilikusukuma kuanza jambo fulani, huenda kilichokusukuma ilikuwa kuwasaidia watu, huenda ilikuwa ni kuboresha maisha yako. Kwa kujikumbusha mara kwa mara kitu kilichokufanya uanze kufanya jambo hilo kutakuhamasisha kama ilivyokuwa awali.

3. Angalia picha kubwa ya mbeleni.

Katika jambo lolote unalofanya, kuna manufaa makubwa sana kwako na kwa  wanaokuzunguka katika siku za mbele. Yajue manufaa haya na yaangalie kila mara ambapo unakosa hamasa. Inaweza kuwa picha kubwa ni kuboresha maisha yako, inaweza kuwakuwasaidia watu wengi zaidi kufikia ndoto zao na kadhalika. Angalia jinsi gani ambavyo ukikata tamaa sasa utajiangusha wewe mwenyewe na wengine pia.

4. Soma vitu vya kukuhamasisha.

Soma vitabu mbalimbali vya kukuhamasisha, soma vitabu vya watu unaowakubali kutokana na mchango wao mkubwa kwenye jamii na dunia kwa ujumla. Kwa kusoma maisha yao na mambo waliyofanya itakuhamasisha sana.

Soma pia mitandao ambayo inakuhamasisha, mtandao kama AMKA MTANZANIA, KISIMA CHA MAARIFA na mingine iliyoko chini ya AMKA CONSULTANTS itakupatia elimu, ushauri na hamasa kubwa ya kuendelea kutekeleza mipango na malengo yako. Kusoma blog zote zilizopo chini ya AMKA CONSULTANTS bonyeza maandishi haya.

Pia jiunge na mtandao wa AMKA MTANZANIA ambapo utakuwa unatumiwa vitabu mara kwa mara. Kujiunga bonyeza hapa na uweke email yako.

5. Kuwa mvumilivu.

Waswahili wanasema mvumilivu hula mbivu, ni kweli kabisa. Katika maisha uvumilivu ni kitu muhimu sana ili kuweza kufikia mafanikio kwenye jambo lolote. Mara nyingi tunapoanza jambo tunakuwa hatujajua kuna changamoto tutaklutana nazo. Unapoanza kufanya jambo na changamoto zikaibuka ndio hamasa inaposhuka na kuishia kukata tamaa. Kuwa mvumilivu hata mambo yanapokuwa magumu, ukishindwa jifunze kutokana na makosa uliyofanya na usiyarudie tena. Ukiendelea kuwa mvumilivu na kung’ang’ania utatimiza malengo yako.

Nyongeza; Tafuta mtu utakayefanya nae jambo au utakayewajibika kwake.

Njia nyingine nzuri ya kuendelea kuwa na hamasa ya kufanya jambo ni kutafuta mtu ambaye utakuwa unafanya nae jambo hilo. Mnapokuwa wawili au zaidi mnaweza kupeana moyo na kuendelea kufanya mlichoanza kufanya. Kama utakosa mtu wa kufanya nae, basi tafuta mtu ambaye utawajibika kwake. Mwambie mtu huyo kwamba umepanga kufanya jambo fulani na yeye awe anakufuatilia kama kweli unafanya jambo hilo. Kama kwenye mazingira yako huwezi kupata mtu wa kukufuatilia kwenye AMKA CONSULTANTS tunayo MENTORSHIP PROGRAM ambayo itakusaidia sana kuondokana na hali hiyo. Kupata maelezo zaidi kuhusu MENTORSHIP PROGRAM bonyeza hayo maandishi.

Fanya mambo hayo na kila siku utakuwa na hamasa kubwa sana ya kuendelea kufanya jambo ulilopanga kufanya. Kama njia zote kabisa zitashindikana, MENTORSHIP PROGRAM haiwezi kushindwa. Unaweza kujiunga na program hiyo na ukajihakikishia kufikia mafanikio makubwa kama kweli utafanya kazi kwa bidii na maarifa.

Nakutakia kila la kheri katika safari ya kufikia mafanikio makubwa.

TUPO PAMOJA, TUTAKUTANA KILELENI.

Kama una changamoto ambayo inakuzuia kufikia malengo yako unaweza kuitoa kwa kubonyeza maandishi haya na kujaza fomu.(CHANGAMOTO NYINGI ZINAZOTOLEWA SASA TULISHAZIJIBU HUKO MWANZONI, VITU KAMA KUPATA MTAJI, MATUMIZI YA FEDHA NA BIASHARA GANI MTU UFANYE TULISHAZIPATIA MAJIBU. KABLA YA KUWEKA CHANGAMOTO YAKO TAFADHALI PITIA MAKALA ZA NYUMA ZA KIPENGELE HIKI CHA USHAURI KWA KUBONYEZA HAPA NA KAMA CHANGAMOTO YAKO HAIJAJIBIWA NDIO UIWEKE.) Changamoto yako inaweza kuwa moja makala zijazo kila siku ya jumatatu. Kama unahitaji ushauri wa haraka wasiliana na mimi kwa kwa email amakirita@gmail.com au simu 0717396253/0755953887.

kitabu-kava-tangazo432

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s