Kama Una Tabia Sugu Inayokukera Iondoe Hivi.

Kurekebisha tabia sugu kwa kawaida mara nyingine humaanisha ni kupambana na mazoea sugu ambayo yamejikita kwa mtu na ambayo ni vigumu kuyarekebisha. Ni jambo la hakika kabisa kwamba mazoea sugu ni yenye athari mbaya kwa mtu, kwani huingilia na kuharibu mfumo wake mzima wa kufikiri na hata shughuli zake za kawaida za kila siku. 
 

Watu wengi, hatimaye hukata tamaa na kudhani kwamba hawawezi kusonga mbele bila kuwa na tabia hizo sugu ambazo zimejijenga kwa kipindi kirefu. Ikumbukwe kwamba mazoea sugu ni jambo la kawaida kwa binadamu. Wote huwa tunaonesha tabia au mazoea sugu kuelekea jambo Fulani kila siku na kwa njia zinazotofautiana.
Kwa vile tabia sugu na zenye madhara kwetu yamekuwa ndiyo mambo ambayo hututesa na kutusumbua katika maisha yetu, hivyo wengi wetu wamekuwa wakitafuta suluhu ya kuondokana nazo siku hadi siku. Hizi ni tabia ambazo tumekuwa nazo kwa muda mrefu, hivyo tusitegemee mazoea haya sugu kupotea kiurahisi kama tusipochukua hatua za kuondokana na tabia hizo.
Kumbuka kwamba, unaweza kupambana na tabia sugu, iwe ni kwenye matumizi ya pombe yaliyopita kiasi, dawa za kulevya, tumbaku, ulafi na tabia nyingine ambazo zimekuwa sugu kwako na ambazo ungetaka kuzifanyia mabadiliko. Epukana na hali ya kuhisi au kuona kwamba ni jambo gumu kwako kuacha mazoea na tabia yako sugu, amini kwamba, unaweza kuacha tabia hizo. 
Utawezaje sasa kupambana na tabia hizi sugu na kuzitoa kabisa katika maisha yako?
1. Kaa mbali na mazingira yatakayokushawishi kuirudia tabia yako ya mwanzo. 
Katika siku za mwanzo za kuacha tabia na mazoea yako sugu, hali huonekana kuwa ni isiyoweza kubadilika. Kama wewe ni mvutaji sugu wa sigara na umeamua kuacha kuvuta, mara unapoingia kwenye chumba au eneo ambalo watu wengine wanavuta sigara, hali hiyo huanza tena kukukumbusha na kukusukuma uanze tena kuvuta sigara. 
Ili kuishinda hali hii ni lazima ujifunze kukaa mbali na mazingira yote yatakayokurudisha kule ulikotoka. Ni lazima ukumbuke kwamba, nguvu inayotokana na mazoea sugu uliyonayo huendelea kupungua kadri unavyoendelea kubadilika kila siku. Usichoke upo wakati utakuwa huru kutoka kwenye tabia yako hiyo inayokusumbua.

2. Epuka kuwa na kauli au fikra hasi zinazohusiana na tabia yako.
Mtu mwenye tabia sugu anapaswa kuepukana na kauli kama hii, ‘Ni hatari, hali  hii haiwezi kuvumilika,’kwani imani kuelekea kwenye kauli hizi, itakufanya uendelee kuhisi vibaya na hivyo kushindwa kufanya mabadiliko ya kweli na yanayofaa, ambayo unataka yabadili tabia yako hiyo na kuwa mpya.
Kwa haraka haraka, mazoea sugu humjengea mtu picha ya matamanio chanya na mazuri. Tunapokuwa sugu kuelekea jambo fulani huwa tunadhani kwamba jambo hilo linatutengenezea hali fulani itakayotufanya tusijikie raha au hata kutupunguzia matatizo fulani. Kwa kweli, mazoea sugu hudanganya, hutuonesha faida peke yake bila kutuonesha hasara yake. 
3. Jifunze kutazama  matokeo yake ambayo ni hasi na mabaya
Hapa inabidi ujiulize maswali mwenyewe yatakayokusaidia kukutoa kwenye tabia yako mbaya. Unaweza ukajiuliza nitajisikiaje hapo baadaye iwapo nitaendelea na mazoea haya? Nitapata mambo gani mabaya iwapo nitaendelea na mazoea haya? Je, hasara ya mazoea haya, itazidi faida yake? Kwa kadri utakavyojiuliza maswali haya utakuwa unapata majibu yakukusaidia kuitoa tabia yako mbaya.
4. Jaribu kujenga picha kuwa, mtu Fulani wa karibu yako ana mazoea sugu ya aina Fulani. Je, ni namna gani utamudu kumshawishi aachane na mazoea hayo
Ni wazi kabisa iwapo utamudu kulitolea majibu sahihi swali hili, basi utakuwa umemudu kuanza kufanya mabadiliko kwa upande wako pia. Kujitenga na mazoea sugu kunatutaka sisi tuitolee majibu hali hiyo katika njia inayofaa na isiyoweza kutuumiza. 
5. Tembelea maeneo au mazingira yenye kuvutia kama vile ufukwe wa bahari, ziwa na bustani. 
Hili ni jambo linaloweza kukusaidia pia uondokane na mawazo yenye mazoea sugu kutoka akilini na hivyo kuweza kustarehe na kupumzika. Unapokuwa unatembelea maeneo hayo yanakuwa yanakusaidia kuijenga na kuibadili akili yako na kuifanya ifikiri tofauti zaidi. Hivyo, utajikuta tabia yako sugu inaanza kuondoka pole pole. 
6. Jitafutie shughuli ambayo inahitaji matumizi ya akili zaidi.
Kama unauwezo wa kuandika riwaya, tamthiliya au makala nzuri ni vizuri ukafanya shughuli hizi kila siku na kila mara ili kuweza kukusahaulisha na tabia sugu inayokusumbua. Ukifanya hivi kwa muda, utajikuta ndivyo unavyoweza kuzoea na hatimaye kusahau kabisa tabia sugu inayokutesa na kukusumbua katika maisha yako.
Hivi ndivyo unavyoweza kumudu kuondokana na tabia sugu zinazo kusumbua, nakutakia mafanikio mema na endelea kutembelea mtandao huu wa AMKA MTANZANIA kwa kuhamasika zaidi.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE.
IMANI NGWANGWALU
0767 04 80 35
0713 04 80 35/ingwangwalu@gmail.com

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: