Sasa hivi tumekuwa watu wa kuendeshwa na shauku inayotokana na hisia. Na hii imetufanya tuwe wateja kwa wanaoweza kuzitumia hisia na shauku zetu.
Kwa mfano;
Kuna tofauti gani kwa anayenunua simu mpya iliyotoka leo kwa kusubiria muda mrefu na atakayekuja kuinunua kesho wakati kumetulia?
Kuna tofauti gani kati ya anayesikia habari mpya leo, BREAKING NEWS na atakayeisikia kesho?
Kuna tofauti gani kwa atakayekuwa wa kwanza kusambaza habari na ambae hatakuwa na haraka hiyo?
Yote haya na mengine mengi hayana tofauti ila yanatufanya tuwe wateja wa matoleo mapya, habari zilizovunjika na mbaya zaidi kusambaza habari ambazo hatuna uhakika nazo ili tu uwe wa kwanza……
Huna haja ya kuwa wa kwanza katika mambo haya, ni kujiongezea tu msongo.