Tunaishi kwenye dunia ambayo kuna njia nyingi sana za kujifunza ili kufikia malengo yetu.

Unaweza kujifunza kwa kufundishwa, yaani kusoma au kukaa darasani au kupata aina yoyote ya mafunzo. Hii ni njia nzuri ya kujifunza.

Pia unaweza kujifunza kwa kushindwa kutokana na makosa yako. Yaani pale unapofanya jambo ukashindwa unajifunza njia ambayo imekufanya ushindwe ni nini na kutokurudia tena. Hii ni njia bora ya kujifunza maana hutosahau.

Njia nyingine unayowez akutumia kujifunza ni kupitia makosa au uzoefu wa watu wengine. Hapa unasoma au kuangalia kile ambacho watu waliofanikiwa wamefanya au hawafanyi na wewe kufanya kama wao. Hii ni njia bora sana ya kujifunza kwa sababu inakupunguzia muda ambao ungepoteza kwa kusubiri ujifunze kwa makosa yako mwenyewe.

Leo hapa utajiongeza kwa vipande kumi vya ushauri bora kuwahi kutolewa. Uchukue kama ulivyo na ufanyie kazi.

1. Haijalishi kama utatumia masaa 1000 kufanya kitu, kama unafanya kwa kukosea ulichojifunza ni jinsi ya kufanya kitu kwa kukosea.

2. Kama utamlaumu mtu mwingine usitegemee mabadiliko yoyote.

3. Usibishane na mjinga, atakayekuwa anaangalia kwa pembeni hatojua tofauti yenu.

4. Acha kuchukulia kila kitu binafsi, hakuna anayekufikiria wewe zaidi ya unavyojifikiria mwenyewe.

5. Kama unataka kukumbuka kitu kiandike mahali.

6. Fanya chochote unachofanya kama wewe ndio mtaalamu uliobobea, kila mtu atakuacha uendelee na kile unachofanya.

7. Jua ni kitu gani unachopenda kufanya, halafu fikiria ni jinsi gani mtu anaweza kukulipa kwa wewe kufanya kitu hiko.

8. Kama umekosea kubali kosa, kama uko sahihi kaa kimya.

9. Nunua kile ambacho utakitumia.

10. Mara zote kuwa na mpango, na mipango mingi itashindwa.

Hivyo ndio vipande kumi vya ushauri bora kuwahi kutolewa. Chukua ushauri huo na ufanyie kazi.