Tabia Saba Za Watu Wasiokuwa Na Mafanikio.

Tumejifunza sana kuhusu tabia za mafanikio. Na fikiri utakuwa unajua tabia kadhaa ambazo ukiwa nazo unaweza kufikia mafanikio unayotarajia kwenye maisha yako.

Lakini pamoja na kujua tabia hizo mbona watu wengi bado wanashindwa kufikia mafanikio?

Jibu rahisi ni kwamba wanaendelea kung’ang’ania tabia zile zile ambazo zinawafanya wasipate mafanikio.

SOMA; Huu Ndio Ushauri Muhimu Sana Wa Kuishi Nao Kila Siku Kwenye Maisha Yako.

Tabia hizo ni zipi basi? Zipo nyingi kulingana na makundi mbalimbali ya watu ila hizi saba zipo kwa watu wote ambao hawana mafanikio.

1. Kuahirisha mambo. Watu wote ambao hawajafanikiwa wana tabia ya kuahirisha mambo. Wataweka malengo na mipango mizuri sana ila wanapofika kwenye utekelezaji wanaanza kuahurisha. Wanajishawishi watafanya kesho cha kusikitisha ni kwamba kesho yao huwa haifiki.

2. Kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja. Hii ni tabia nyingine ya watu wasiokuwa na mafanikio, wanataka wafanye kazi, huku wanaangalia tv, wanachat kwenye simu na kuwa kwenye mitandao ya kijamii. Akili moja huwezi kuigawa kwenye mambo yote hayo na bado ikawa na ufanisi mzuri.

SOMA; Kauli Mbili Za Kuacha Kutumia Leo, Maana Zinaashiria Kushindwa.

3. Kukubali kushindwa. Pale wanapokutana na changamoto au kikwazo wanakimbilia kusema wamejaribu ila wameshindwa.

4. Kupenda kuiga. Watu wasiokuwa na mafanikio hawana muda w akukaa na kufanya ubunifu wao wenyewe, wao hupenda kuiga kila kitu na mwishowe kujikuta kwenye wakati mgumu.

5. Hawajui njia bora za kujumuika na wengine. Watu wasiokuwa na mafanikio hawajui jinsi ya kujumuika na watu wenye mafanikio ili wajifunze mengi kutoka kwao.

6. Kufanya chochote ili waambiwe ndio. Watu wasiofanikiwa ni watu ambao wanapenda sana kuwaridhisha watu. Hujaribu kufanya chochote kile ili kuwafurahisha wengine na hivyo huishia kuwa na maisha magumu.

SOMA; Maisha Sio Rahisi Lakini Ni Mazuri Kama Hivi…

7. Kuhukumu. Watu wasiokuwa na mafanikio ni wazuri sana kuhukumu wengine. Hupend akufuatilia maisha ya wengine na kuhukumu kila jambo ambalo wanalifanya.

Epuka tabia hizi saba kama kweli unataka kufikia mafanikio kwenye maisha yako. Kama utaendelea kuzishikilia utajaribu kila mbinu lakini mafanikio hutoyaona.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: