Okoa Muda Huu Muhimu Ambao Unaupoteza Kila Siku Na Kukuchelewesha Kufikia Mafanikio.

Kuna muda mwingi sana ambao unaupoteza kila siku na kwa kufanya hivyo unajichelewesha kufikia mafanikio.

Kumbuka muda una thamani kubwa kuliko fedha kwa sababu muda ukishapotea haurudi tena, ila ukipoteza fedha leo kesho unaweza kupata nyingine.

SOMA; UKURASA WA 09; MUDA–Kitu Chenye Thamani Kubwa Ila Kisichothaminika Na Wengi.

Muda huo unaopoteza ni ule unaotumia kusema mabaya ya wengine, au kuonesha mapungufu ya wengine.

Ni kweli kwamba wengine wanaweza kuwa wana mapungufu makubwa, wanaweza kuwa wanakosea sana ila wewe kutumia muda wako kuyasemea hayo hakutakusaidia kwa vyovyote kufikia mafanikio unayotarajia.

Kwa mfano wewe ni mfanya biashara na unatumia muda wako mwingi kusema jinsi gani wafanyabiashara wengine wanakosea, au wanamadhaifu. Kwa kufanya hivi hauna tofauti na wao. Ni heri kutumia muda wako mwingi kuimarisha biashara yako.

SOMA; Sheria NANE Za Kufanikiwa Kwenye Biashara Kutoka Kwa Warren Buffett.

Inawezekana wewe ni mchungaji ambae una kanisa, ila unatumia muda wako mwingi kusema jinsi gani wachungaji wengine wana mapungufu au wana mabaya. Ni vyema ukatumia muda huo vizuri kuwaonesha watu ni kipi sahihi kinachotakiwa kufanywa.

Inawezekana wewe ni mwanasiasa na unatumia muda mwingi kuonesha madhaifu ya chama kingine au mgombea mwingine. Hii haitakusaidia kushinda uchaguzi, ni vyema kutumia muda wako mwingi kuwaeleza watu utawafanyia nini na watakuona upo makini.

Sisemi tusikemee mabaya, ila hii isiwe agenda yetu kuu, labda kama ndio agenda yako na kama ndivyo hujui unachokifanya au itakuwa vigumu kifikia mafanikio.

Kumbuka kitu chochote ambacho hakipo kwenye malengo na mipango yako ni kelele kwako. Achana nacho mara moja na wekeza nguvu zako kwenye kukuza kile unachofanya.

SOMA; USHAURI ADIMU; Unapokutana Na Tatizo Jiulize Jambo Hili Moja La Msingi.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: