Ijue Siri Ya Mafanikio Ya Kiuchumi

Na Charles Nazi.

Watu wengi huwa wananiuliza nini siri ya mafanikio ya kiuchumi/utajiri? Jee ni vigumu kuwa tajiri au ni rahisi? Jee kuna njia ya mkato? Katika makala hii nitatoa majibu.

Siri ya mafanikio ya kiuchumi au Utajiri ni kuwa na ndoto za kufanikiwa (kuwa tajiri) Ninapenda kila mtu awe na ndoto hii kwani inawezekana. Kisha aweke malengo yaani ni kiasi gani cha utajiri anachokitaka na kwa muda gani. Malengo yanatakiwa yawe makubwa mfano kuwa milionea (kumiliki mali zenye thamani ya bilioni 1.7 ambayo ni sawa na dola milioni 1.) Muda ambao unapaswa kujiwekea ni kuanzia miaka 5 hadi 10. Tafuta fursa ya biashara au mradi wa kufanya kufikia malengo yako. Fursa ya biashara ni kuwa na bidhaa au huduma inayotakiwa na watu wengi. Kwa kuangalia historia ya matajiri wengi wamefanikiwa kwa kujishughulisha na fursa zifuatazo;

  1. Kumiliki biashara zinazotokana na jambo wanalolipenda (hobi)
  2. Kuwekeza kwenye majengo( Real estate)
  3. Kuwekeza kwenye kununua hisa
  4. Biashara ya madini (Dhahabu)
  5. Biashara ya mafuta (Petroli)
  6. Biashara ya kampuni ya simu
  7. Biashara ya mabenki
  8. Ushauri wa biashara
  9. Biashara ya magazeti
  10. Kufanya Biashara kupitia mtandao wa internet

Fursa zote nilizozitaja hapo juu nitazizungumzia kwa kirefu kwenye makala zangu zinazofuata.

SOMA; Unapokuwa Tayari Kuingia Kwenye Ujasiriamali Fanya Vitu Hivi Vitano.

Hakuna njia ya mkato kwa mtu anayetaka kupata mafanikio. Malengo yako yanatakiwa yachukue muda wa miaka 5 hadi 10. Uwe na mtizamo wa muda mrefu. Mawazo ya kupata utajiri wa haraka haraka kwa njia za Freemason, ushirikina kutumia viungo vya Albino, kuuza madawa ya kulevya ni makosa ya jinai ambayo yanaweza kukusababishia matatizo ya kufungwa jela. Kitu kingine Unachotakiwa kukifanya ni kutafuta mwalimu, mtu aliyefanikiwa na mwenye upendo wa kuwafundisha watu. Mfano mwandishi wa makala hii huwa anatoa huduma hii. Tuonane wiki ijayo.

Mwandishi wa makala hii ni Mkurugenzi wa Kampuni ya CPM Business Consultants, Mjasiriamail,Mshauri wa biashara na mtunzi wa kitabu cha mbinu za biashara , Kupata ushauri wa biashara, Ili Kupata mafunzo ya ujasiriamali bila malipo kwa email bofya hapa kujiunga;http://tinyurl.com/mshauriwabiashara au Piga simu namba 0784394701

 

SOMA; Maswali Matatu Muhimu Ya Kujiuliza Kwenye Wazo Lako La Biashara.

 

kitabu-kava-tangazo432

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: