Biashara Ya Uwekezaji Wa Kwenye Majengo Inavyoweza Kukutajirisha.

Na Charles Nazi.

Jee unajua kwamba ardhi ni mali? Angalia mfano huu, kuna jamaa mmoja kule maeneo ya Goba alinunua shamba kwa shilingi milioni 15 baada ya miezi 3 alipata mteja aliyekuwa analitaka kwa milioni 35 na akapata faida y ash. Milioni 20. Kwa kuona fursa hiyo ya kufanya biashara ya kununua na kuuza mashamba jamaa alizinduka na kuanza kununua na kuuza viwanja na kuweza kufanikiwa kubadilisha maisha yake. Mtindo huu kwa kitaalamu unaitwa (Flipping)

real-estate-investing

Biashara ya kununua na kuuza ardhi na majengo na upangishaji wa nyumba (Real estate)  umewatajirisha watu wengi sana duniani. Mfano mzuri wa mtu aliyefanikiwa katika biashara hii ni Donald Trump ambaye anamiliki majengo makubwa na mahoteli katika miji mikubwa ikiwemo jiji la New York. Mifumo ya biashara hii ni mingi ikiwemo ule wa kununua majengo kwa bei rahisi na kuuza kwa bei ya juu( flipping) mara nyingi mtu anayefanya biashara kwa mtindo huu huwa anatafuta dili (deals), kutoka kwa madalali wa mahakama na kununua nyumba kwa mnada kwa bei ya chini nyumba za watu walioshindwa kulipa mikopo ( foreclosure)  na baada ya muda kuzifanyia ukarabati kidogo kuziongezea thamani au kuziuza kama zilivyo.

SOMA; Hivi ndivyo unavyoweza kununua Hisa katika soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

Kwa mfano hata hapa kwetu kuna watu wanafanya biashara kwa mtindo huu. Kuna bwana mmoja alinunua nyumba kwa sh. milioni 70 baada ya miezi 2 akaiuza kwa sh. milioni 400 ambapo alipata faida y ash. Milioni 330. Hii ni biashara ya chap chap na inaweza kukutajirisha haraka.

Njia nyingine ni kujenga nyumba na kupangisha. Unaweza kujenga kwa kutumia pesa zako au kutumia mkopo kutoka benki (mortgage financing) Kama ukiomba mkopo unaweza kulipa mkopo kwa kupitia kodi ya pango kutoka kwa wapangaji au unaweza kuiuza kwa bei ya juu na kulipa mkopo wa benki na kubaki na faida kiasi. Kuna bwana mmoja kule Brazil alianza kwa kujenga nyumba yake na kuanza kuchukua mikopo ya benki ndani ya miaka 5 alikuwa anamiliki maghorofa 30 na kuwa amelipa mikopo yake.

SOMA; Huyu Ni Mjasiriamali Mwenye Hamasa Kubwa sana. Unaweza kujifunza kila kitu kutoka kwake.

Kama huna mtaji unaweza kuanza kuwa dalali (Real Estate Agent) kwa kuwakutanisha wanunuzi na wauzaji wa majengo, viwanja na mashamba kasha ukapata kamisheni. Kwa hali ya Tanzania madalali wanapata kamisheni kati ya asilimia 5% hadi 10% ya bei ya kuuzia nyumba, viwanja  na kodi ya pango ya mwezi mmoja kama kamisheni. Udalali wa viwanja majengo na mashamba unaweza kukutajirisha kwa kuwa mauzo ya majengo huwa yanatumia pesa nyingi na kamisheni inaweza kuwa kubwa. Hivyo biashara hii ukiifanya kwa ufanisi unaweza kukutajirisha.

Mwandishi wa makala hii ni Mkurugenzi wa Kampuni ya CPM Business Consultants, Mjasiriamail,Mshauri wa biashara na mtunzi wa kitabu cha mbinu za biashara , Kupata ushauri wa biashara, Ili Kupata mafunzo ya ujasiriamali bila malipo kwa email bofya hapa kujiunga;  http://tinyurl.com/mshauriwabiashara  au Piga simu namba 0784394701

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: