FEDHA: Hiki Ndicho Kitu Kinachokuzuia Wewe Kuufikia Uhuru Wa Kifedha.

Kila mtu kwa sehemu yake huwa ana nia ya kubadilisha maisha yake na pengine kuwa huru kabisa kifedha. Nia hii huwa ndiyo inayowaongoza wengi kufanya kila kinachowezekana ili angalau kuweza kuongeza kipato ambacho kitaweza kusaidia kubadilisha maisha. Kutokana na juhudi hizi, wapo ambao huamua kubadilisha kazi, kuongeza juhudi zaidi katika kile wakifanyacho, kujiwekea akiba ya kutosha na hata kuwekeza zaidi ili mradi tu kipato kiongezeke na hatimaye kuufikia uhuru wa kifedha wanaouhitaji.
 

Pamoja na juhudi hizi, hata zile za kuweza kubadilisha kazi hii na kazi ile ili kuweza kupata kazi inayolipa zaidi ambayo itatusaidia kutufikisha kwenye uhuru wa kifedha tunaouhitaji, lakini kitu cha kushangaza huwa hatupati matokeo mazuri au kuona mabadiliko makubwa kama ambavyo huwa tunatarajia iwe kwetu. Hiki ni kitu ambacho huwa kinawashangaza wengi na kushindwa kuelewa ni kitu gani kinachofanya iwe hivyo? Wengi hapa huishia kusema hawana ‘nyota’ ama ‘bahati’ ya pesa.
Hali hii pengine umeshawahi kukutokea ama umeshuhudia katika maisha ya wengine wakiishi kwa mfumo huo pasipo kuona kitu ama mabadiliko yoyote endelevu ya maana yanayotokea katika kuufikia uhuru wa kifedha. Wengi wanapokutana na hali hii hapa ndipo huanza kumtafuta ‘mchawi’ na kuweka visingizio na sababu za kila aina za kujaribu kutuonyesha kuwa kwanini wanashindwa kufikia hasa yale malengo ya kifedha ambayo wamekuwa wamepanga wayaone katika maisha yao.
Kwa vyovyote vile utakavyofikiria unaweza  ukasingizia au ukaja na sababu nyingi kama vile Aaaah wao wamejaliwa na  nyinginezo nyingi ambazo utakuwa unajitetea kwazo, lakini ukweli ni kwamba kipo kitu kimoja ambacho huwa kinasababisha ama kukufanya ushindwe wewe kufikia uhuru wa kifedha. Kitu hiki si kingine bali ni mawazo uliyonayo. Kwa sababu zote unazozitoa hizo ni sababu za nje tu, lakini mawazo yako ndiyo yanayokufanya uishi kama ulivyo hapo ulipo.
 
Unaweza ukaanza kuuliza Imani ni kwa vipi hapo mbona kama sielewi elewi sielewi sikiliza, mawazo yako yamekufikisha hapo ulipo kutokana na wewe unavyoamini juu ya mafanikio hasa yale ya pesa. Kama unaamini unaouwezo wa kupata pesa kisha ukachukua hatua kwa vitendo sio ukabakia unawaza tu uwe na uhakika utafanikiwa katika hilo. Kabla hujaanza kulaumu juu ya hali uliyonayo kwanza anza kujikagua katika mfumo mzima wa mawazo ulionao na kisha  jiulize mwenyewe, je unawaza sawasawa na mkabala wa kile unachikitaka? 
Watu wengi wenye mafanikio makubwa na kuweza kufikia uhuru wa kifedha huwa ni wa watu wa mitizamo chanya juu ya pesa na mafanikio kwa ujumla. Huwa wanaamini wanaouwezo katika kupata pesa na utajiri na ndicho hutokea. Huwa sio waotaji wa ndoto au kuwa na matumaini ambayo hayafikiki.
Haijalishi upo katika hali gani, lakini kitu kimoja pekee ambacho unatakiwa ujue ni kuwa unaouwezo wa kubadili hali uliyonayo na kufikia uhuru wa kifedha unaoutaka. Utaufikia uhuru huo endapo tu wewe utaamua kwanza kuwa na mtazamo chanya juu pesa. Hiki ndicho kitu pekee unachotakiwa  kufanya sasa ili kubadili matokeo na kuweza kuufikia uhuru wa kifedha vinginevyo utafanya kazi sana, lakini utakuwa huyaoni hasa yale matunda unayategemea.
Kwa kuthibitisha hili, angalia maisha ya watu wote wenye mafanikio makubwa duniani ukianza na Bill Gates, Warren Buffet, Donald Trump, Larry Ellison na wengineo wengi wote hawa maisha yao kwa ujumla yametawaliwa na mitazamo chanya na kuamini mafanikio kwao yanawezekana na ni kitu cha lazima sio hiari. Ukiwa na mtazamo wa kuamini kuwa kufanikiwa kwako ni lazima na hakuna uhiari wowote kwa hilo  ni lazima ufanikiwe.
Unaanza ukaanza leo kubadili mfumo wa kuamini kwako ili ukuletee mafanikio unayotaka. Jaribu kukaa chini na kuchunguza kwa kina imani ulizonazo juu ya pesa ni zipi ambazo zinakurudisha nyuma? Unaweza ukawa umebeba mtazamo kuwa watu wote wenye mafanikio kipesa ni wabaya, mitazamo kama hii itakusumbua sana na itakuwa ngumu kwako kuweza kusonga mbele.
Kitu ambacho unatakiwa kukifanya ni kufutilia mbali mitazamo hasi uliyonayo juu ya pesa na kubeba mitazamo chanya ambayo itakusaidia kukufikisha kwenye uhuru halisi wa kipesa unaoutaka uwe katika maisha yako. Ila utabadilisha mitazamo hii tu ikiwa utakuwa una nidhamu binafsi na pia kujisomea sana vitu chanya ambavyo vitaweza kubadili maisha yako kwa sehemu kubwa na kuwa na fikra mpya.
Siku zote acha kukaa na kuanza kulaumu watu juu ya maisha yako uliyonayo. Kumbuka unalojukumu la kubadili maisha yako wewe mwenyewe na sio mtu mwingine. Yapo mambo mengi yanayoweza yakawa yanakuzuia kuufikia uhuru wa kifedha unaoutaka, lakini liliokubwa ni mawazo yako mwenyewe, ndiyo yanayokufanya ushindwe kufikia ndoto na malengo yako. Kuwa makini na mawazo yako, chukua hatua sahihi, utafanikiwa na kuufikia uhuru wa kifedha unaoutaka.
Kwa makala nyingine nzuri hakikisha unatembelea DIRA YA MAFANIKIO kwa maarifa na elimu bora itakayoboresha maisha yako.
Ansante kwa kutembelea mtandao huu wa AMKA MTANZANIA, endelea kuwashirikisha wengine kujifunza mambo mazuri yanayoendelea hapa.
TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YAKO YA MAFANIKIO.
IMANI NGWANGWALU,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: