USHAURI; Kabla Hujachukua Mkopo Ondokana Na Tabia Hii Kwanza.

Mpenzi msomaji wa AMKA MTANZANIA karibu kwenye kipengele hiki cha ushauri wa changamoto mbalimbali zinazotuzuia kufikia mafanikio katika jambo lolote ambalo tunafanya. Wiki hii tutajadili umuhimu wa nidhamu ya fedha kwa sababu ukosefu wa nidhamu ya fedha imekuwa kikwazo kwa wengi kuweza kufikia mafanikio makubwa.

Kabla hatujaona ni mambo gani ya kufanya ili kuwa na nidhamu ya fedha, tupate maoni kutoka kwa msomaji mwenzetu.

Habari za kazi ndugu,

Kwanza kabisa napenda kuanza kukupongeza kwa kazi kubwa na nzuri unayoifanya ya kuelelimisha jamii  juu ya kupambana ili kuweza kujikwamua katika hali ya umasikini, Mwenyezi Mungu akujalie afya nzuri, nguvu na ujasili wa kuendelea kutuelimisha jamii, pia akubariki sana katika kazi zako zote.

Mimi nikijana wa kitanzania nimekuwa nikifuatilia makala zako nyingi sana hasa za biashara na zimekuwa zikinivutia sana na kunipa hamasa ya kufanya biashara ili kuweza kuongeza kipato.

Mimi ni muajiliwa wa serikali lakini mshahara ninaoupata haukizi haja zangu ndiomaana natamani sana kufanya biashara ili kuweza kuongeza kipato, tatizo linalosababisha nisiweze kuanzisha biasha ni mtaji wa kuanzisha biashara, nimekuwa nikijaribu ku- save kiasi kidogo kutoka kwenye mshahaara lakini kulingana na matatizo yanayo pamoja na majukumu nimejikuta hata kile kiasi nacho save nakitumia.

Nilikuwa naomba ushauli kutoka kwako,  nataka kuchukua mkopo kutoka benk ili niweze kupata mtaji wa kuanzisha biashara, Je ? inafaa kukopa benk na kutumia kama mtaji katika biashara.

Asante.

Kama ambavyo tumeona kwenye maelezo ya msomaji mwenzetu hapo juu, nidhamu ya fedha ni tatizo kubwa. Mwenzetu amekuwa anajaribu kuweka akiba ili aweze kuitumia kufanya biashara ila kutokana na matatizo yanayotokea anajikuta ametumia akiba ile. Na sasa anafikiria kukopa benki ili kupata mtaji wa kuanza biashara, je haya ni maamuzi sahihi kwake?

Kabla hata hujafikiria kwenda kuomba mkopo wa benki napenda kukushauri ubadili kwanza tabia yako kuhusu fedha. Kama fedha unazoweka akiba mwenyewe unashindwa kuziheshimu na kuzitumia pale unapopata matatizo, unafikiri ni kitu gani kitakuzuia wewe kutumia fedha za mkopo wa biashara kwenye matatizo yatakayojitokeza?

SOMA; Mambo Matatu(3) Muhimu ya Kujua Kabla Hujachukua Mkopo wa Biashara.

Changamoto kubwa zinazojitokeza wkenye mikopo zinaanzia pale mkopo unapotumika kwa matumizi ambayo siyo yaliyosababisha mtu achukue mkopo. Na kama akiba ulizoweka mwenyewe unashindwa kuzilinda kwa sababu ya matatizo, hata mkopo utashindwa kuulinda na utaingia kwenye matatizo makubwa zaidi. Hii ni kwa sababu matatizo huwa hayaishi, nidhamu ya fedha pekee ndio inayoweza kukufanya uepuke kutumia fedha katika matumizi ambayo hayakupangwa.

Kuchukua mkopo kwa ajili ya kwenda kuanza biashara ni jambo ambalo siwezi kukushauri. Ni hatari sana kwa sababu kama hujawahi kufanya biashara kuna changamoto nyingi sana utakazokutana nazo kwa kipindi cha mwanzo. Changamoto hizi ni bora ukakabiliana nazo ukiwa umeanza kidogo kwa fedha zako. Baada ya kujua ni kitu gani kinawezekana ndio unaweza kuchukua mkopo ili kuimarisha biashara yako zaidi.

SOMA; USHAURI; Tatizo La Kuanza Biashara Na Mtaji Wa Kukopa.

Hivyo nakushauri ubadili tabia yako kuhusu fedha, anza kuweka akiba na safari hii kuwa na nidhamu kubwa sana na tumia akiba hiyo kuanza biashara. Ukishakuwa mzoefu kwenye biashara na ukajua ni kipi kinakuletea faida, ndio wakati ambao unaweza kuchukua mkopo na mambo yako yakaenda vizuri.

Tumeshajadili sana kuhusu tabia za fedha kwenye makala mbalimbali zilizopita. Ila kwa ufupi unaweza kufanya mambo yafuatayo ili kujiimarisha katika eneo la kuweka akiba.

1. Weka akiba yako sehemu ambayo sio rahisi kuitoa.

Kwa kuwa tayari wewe nidhamu yako ya fedha ni ndogo, usiweke fedha kwenye eneo ambalo ni rahisi kuzitoa. Weka akiba yako kwenye eneo ambalo sio rahisi kuzitoa kama ilivyo benki. Baadhi ya njia unazoweza kutumia ni kuwekeza kwenye hisa au vipande.

2. Weka akiba mbili tofauti.

Ukiwa na akiba moja, basi tatizo lolote litakalotokea utapeleka macho yako kwenye akiba yako. Badala yake kuwa na akiba mbili tofauti. Akiba ya kwanza ni fedha za dharura na hii ndio utakayoitumia pale matatizo mbalimbali yanapojitokeza. Na akiba ya pili ni fedha za kuwekeza ambapo hii ukishaweka fedha unasahau kama ni za kwako. Yaani ukishaweka fedha kwenye akiba hii unafikiria ni kama ulishazitumia kununua vitu na hivyo huwezi kuzipata tena.

SOMA; Ukweli Kuhusu Kutengeneza Fedha Kwa Njia Ya Intanet Na Jinsi Ya Kuepuka Kutapeliwa.

3. Fanya lengo lako likusukume.

Kama lengo lako la kuingia kwenye biashara ni kubwa sana na linakupa shauku kubwa, utajikuta unafanya kila juhudi ili kuweza kulifikia. Kaa chini na uweke lengo lako vizuri ili liwe hamasa kubwa kwako kuchukua hatua, na utajikuta unafanya mambo makubwa sana ambayo hukuwahi kufikiri ungeweza kufanya.

Kabla hujafikiria kukopa fedha angalia wkanza tabia zako za fedha zipoje. Hii itakusaidia usije kuingia kwenye matatizo makubwa zaidi kifedha. Jijengee nidhamu ya fedha na hii itakuwezesha kufikia mafanikio makubwa. Pia usikope fedha kwa ajili ya kwend akuanza biashara, unajiweka kwenye hatari isiyo ya msingi.

Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya mafanikio.

TUPO PAMOJA

Makirita Amani 

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kama una changamoto ambayo inakuzuia kufikia malengo yako unaweza kuitoa kwa kubonyeza maandishi haya na kujaza fomu. Changamoto yako inaweza kuwa moja ya makala zijazo kila siku ya jumatatu. Kama unahitaji ushauri wa haraka wasiliana na mimi kwa email makirita@kisimachamaarifa.co.tz au simu 0717396253/0755953887.

Kabla ya kutoa changamoto yako pitia changamoto ambazo tayari zimejadiliwa ili usirudie ambayo imeshajadiliwa. Bonyeza hapa kusoma changamoto zilizojadiliwa.

kitabu-kava-tangazo4322

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: