Haya Ndiyo Mambo Yanakukwamisha Na Kukufanya Ushindwe Kufikia Malengo Yako Uliyojiwekea.

Mara nyingi unashindwa kufikia malengo yako makubwa uliyojiwekea siyo kwa sababu huna mipango na malengo mazuri uliyojiwekea ila ni kwa sababu ya mambo madogo madogo ambayo  huwa unayafanya kimakosa na yanayokupelekea wewe ushindwe kufikia malengo yako uliyojiwekea kwa urahisi.
 

Kwa kufanya makosa haya mara kwa mara bila kujua wengi hujikuta wakishindwa kufanikisha na kutimiza ndoto zao walizojiwekea. Ni muhimu sasa kwako kuweza kutambua kuwa yapo mambo ambayo yanakukwamisha na kukufanya ushindwe kutimiza ndoto zako. Je unajua hayo ni mambo gani?  
Haya Ndiyo MamboYanakukwamisha Na Kukufanya Ushindwe Kufikia Malengo Uliyojiwekea.
1. Haufanyi mabadiliko katika maisha yako.
Ikiwa unataka kuboresha maisha yako na kutoka hapo ulipo kwa sasa ni muhimu kwako  kufanya mabadiliko ya lazima katika yale mambo unayoyafanya. Kama utaendelea kufanya mambo yako kwa namna ulivyokuwa ukiyafanya hutabadilisha chochote zaidi ya kupata matokeo yaleyale kama uliyonayo sasa. 
Mara nyingi kitu kitu kikubwa kinachotofautisha kati ya watu waliofanikiwa na ambao hawajafanikiwa ni namna jinsi wanavyotenda mambo yao. Watu wenye mafanikio huwa ni watu wa kufanya mabadiliko mapema katika mambo yao kama njia walizotumia awali hazifanyi kazi vizuri. Kama unataka kubadili maisha yako kabisa, fanya mabadiliko kwa kile unachofanya utafanikiwa.

2. Unasubiri sana muda sahihi.
Kati ya kitu kinachokukwamisha na kukurudisha nyuma sana katika maisha yako ni kuendelea kusubiri sana muda mwafaka wa kuleta mabadiliko katika maisha yako. Kama utaendelea kusubiri muda sahihi na mwafaka ndio uendelee kufanya mambo yako, nakupa uhakika huo muda kwako hautafika na ukiendekeza hali hiyo hutaweza kutoka kwenye umaskini.
Kitu unachotakiwa kuelewa kuwa unao muda mchache sana hapa duniani. Hauna haja ya kusubiri kesho au kesho kutwa ndio uanze kutekeleza ndoto zako. Anza kutekeleza ndoto zako hata kama ni kwa kidogokidogo, lakini ilimradi ufanye kitu kitakachokusogeza kwenye malengo yako. Kuendelea kusubiri kesho utakuwa umechelewa na hutofanikiwa kamwe.
3. Hujajiwekea mipango endelevu ya kutimiza ndoto zako.
Ni muhimu sana kujiwekea mipango endelevu na malengo kwa kile unachotaka kwenda kukitimiza hatua kwa hatua. Ni lazima uweze kujua leo, kesho utafanya nini kidogo ambacho kitakupeleka karibu kufikia ndoto zako hata kama ni kwa mwendo mdogo mithili ya kinyonga. Kama hujajiwekea mipango endelevu huwezi kufika mbali.
Watu wengi wenye mafanikio makubwa huwa wana mipango endelevu kwenye ndoto zao. Huwa ni watu ambao wana mpangilio mzima wa kuweza kujua nini kitafanyika kesho ama kesho kutwa cha kusaidia kutimiza malengo muhimu. Kama utakuwa unaishi kwa kuwa na mipango endelevu, tambua utaweza kufikia malengo yako uliyojiwekea.
4. Hauchukui jukumu la kujitoa mhanga.
Kila kitu unachokifanya katika maisha yako ni lazima ujifunze kujitoa mhanga ili kuweza kufikia ndoto zako. Hakuna utakachoweza kukifanikisha kwa kufanya mambo kwa urahisi. Maamuzi na hatua unazochukua kila siku ni lazima ziwe za maamuzi magumu yatakayolenga kufanikisha kile unachokihitaji katika maisha yako.
Hakikisha kwa kila unachokifanya kifanye kwa ukamilifu kwa kujitoa mhanga mpaka ufanikiwe. Acha kuogopa kitu jitoe kwa nguvu zote utafanikiwa na kufika mbali katika maisha yake. Watu wengi waliofanikiwa nakufikia viwango vya juu vya mafanikio ni watu wa kujitoa mhanga siku zote na wewe unaweza kufanya hivyo na kufanikisha malengo yako.
5. Unashikiria mambo mengi ambayo hayana msaada kwako.
Kuna wakati umejikuta ukiwa unashindwa kutimiza ndoto zako kutokana na kushikilia mambo mengi kichwani ambayo hayana msaada kwako. Hebu jaribu kufikiri, ni mara ngapi umekuwa ukiamini na kujiambia kuwa huwezi k kufanikiwa kwa sababu ya hii na hii. Yote hayo ni moja ya mambo ambayo umekuwa ukiyashikiria na hayana msaada kwako. 
Kama unataka kuona mipango na malengo yako yakifanikiwa, jifunze kutokushikiria vitu ambavyo huviwezi. Acha kuamini kuhusu maneno ya watu ambayo wanaweza kukuambia wewe kwa namna moja au nyingine kuwa eti huwezi kufanikiwa kwa sababu wanazojua wao. Jiamini kuwa unaweza na kisha songa mbele.
6. Unataka kufanya mambo yako kwa ukamilifu sana.
Hiki pia ni moja ya kitu kinachokufanya ushindwe kufikia malengo yako muhimu uliyojiwekea. Kikubwa kinachokukuta hapa unataka sana kuona mambo yako ukiyafanya ukiwa umekamilika kwa asilimia zote na kitu ambacho hakiwezekani kwako.
Kama unataka kufanikiwa na kutimiza ndoto zako, acha kujiandaa sana kwa kufanya maandalizi ambayo hayaishi. Anza kuishi kwa kufuata ndoto zako kila siku, utafanikiwa. Ukisubiri sana mpaka kila kitu kikamilike kwako utajikuta hutaweza kufanya kitu zaidi ya kukwama.
Hayo ndiyo mambo ambayo kwa sehemu kubwa yanakukwamisha na kukuzuia usiweze kufikia mipango na malengo yako makubwa uliyojiwekea. Kwa kujua hilo ni muhimu kuweza kuyaepuka na kuchukua hatua sahihi zitakazoweza kukufikisha kwenye maisha unayotaka.
Kwa makala nyingine nzuri hakikisha unatembelea DIRA YA MAFANIKIO kwa elimu na maarifa bora yatakayoboresha maisha yako.
TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YAKO YA MAFANIKIO.
IMANI NGWANGWALU,
0713 048035,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: