Hizi Ndizo Nguvu Ulizonazo Ndani Mwako, Zenye Uwezo Mkubwa Wa Kukupa Utajiri.

Katika maisha yetu kwa kawaida kuna ukweli huu, ambao mara nyingi sio rahisi sana kujulikana, kwamba kuna nguvu zilizo ndani yetu binadamu na zile zilizo nje yetu. Kwa bahati mbaya nguvu tunazozijua au pengine kuziamini ni zile zilizo nje yetu. Nguvu hizi ni zile ambazo tunaziona moja kwa moja na tunaweza kuthibitisha moja kwa moja juu ya ufanyaji kazi wake.

Tukizungumzia umeme na jinsi unavyofanya kazi, tukizungumzia mawimbi ya sauti na namna vinavyoweza kufanya kazi, tukizungumzia athari za mwezi, jua na sayari kwa binadamu, hewa, radi au matetemeko na mfumuko wa volcano, inaeleweka na kukubalika kirahisi kabisa.

Lakini unapomwambia mtu kwamba, binadamu ana nguvu nyingi ndani mwake za kumwezesha kufikia mafanikio makubwa sana na kufanya mambo ambayo hayatarajiwi kwa mazoea kufanywa naye, anaweza asikubali kirahisi. Ukweli ni kwamba, ndani mwetu kuna nguvu nyingi  sana ambazo zinapofanya kazi wakati mwingine hata sisi wenyewe bila kujua, sisi wenyewe hushangazwa nazo na pengine kuogopa.


Hebu fikiria juu ya watu ambao wanaweza kukueleza kuhusu maisha yako wakati hujawahi kukutana nao hata mara moja na hawakufahamu kabisa! Likikutokea jambo kama hili unaweza kubisha kwamba, watu hawa wanatumia mbinu za kumchunguza mtu kwa siri au utawaona wana umungu fulani ndani yao ambao unafanya kazi na kuwezesha wao kujua mambo yako.
Kama tunakubali au hatukubali, ni kwamba binadamu ana nguvu za ziada ndani mwake ambapo anapoweza kuzitumia zinaweza kumsadia sana. Hata hivyo, nguvu hizi ni kubwa kwa baadhi ya watu na ni za wastani kwa baadhi na ndogo kwa wengine. Lakini kila mmoja anazo na kwa wakati mmoja au mwingine au kwa njia moja au nyingine huweza kumsaidia kila mmoja.

Nguvu hizi kuna wakati huweza kujitokeza kidogo na kutoweka siyo kwa sababu wengi tunaojua kwamba zipo, hivyo hakuna anayezipalilia  ili ziweze kustawi na kutumiwa kikamilifu. Kila miongoni mwetu ameshawahi kutokewa na nguvu hizi, zaidi ya mara moja maishani mwake na anaweza kuthibitisha hili kama nikisema namna mtu anavyoweza kuzigundua.


Inawezekana kuwa vigumu kwetu kukumbuka kwamba tulishatokewa nazo kwa sababu hatukujua kwamba tulishatokewa nazo, kwa sababu hatukujua kwamba ndizo zenyewe au kwa sababu hatukujali, tuliona ni kitu cha kawaida au nasibu tu ya mambo.

Kwa kuthibitisha hili hebu jiulize hivi, umeshawahi kutaka kumpigia mtu simu lakini wakati uatafuta jina lake ili umpigie ghafla unashangaa yeye ndiye unayekupigia?

Je, hujawahi kuhisi kwamba kutatokea jambo fulani baya kwako kama msiba, wakati hakuna mgonjwa au taarifa ya matatizo, na kweli jambo hilo likatokea? Kwa upande wako hii huwa unaichukulia vipi?

Je, hujawahi kuhisi unavutwa na hamu ya kufanya jambo na ukaanza kulifanya na baadae unakuja kugundua kuwa, hilo jambo umelifanya mahali pake na wakati wake kabisa? Unafikiri hali hii huwa inatokana na kitu gani?

Je, hujawahi kuhisi kwamba unajua kinachoenda kwenye hisia za mtu, hata kama nje au usoni haonyeshi  hivyo na ukaja kujua kwamba ulichokuwa unafikiria ni kweli kabisa? Kwako jambo hili linaashiria kitu gani?

Je, hujawahi kuwaona watu ambao kila wakati wako sahihi, yaani wanachosema au kuamua ndicho hicho, wakati siyo kwamba wana ufahamu mkubwa kuliko wengine au wanajituma sana kuliko wengine? Unadhani huu uwezo unatoka wapi?


Kuna ishara nyingi ambazo huwa zinatutokea na kutuonyesha kwamba,tuna nguvu za ziada ndani mwetu, ambapo, zinapotusaidia, kwa sababu hatujui lolote kuzihusu, huwa tunaita bahati. Lakini kiukweli kama hujui, hizi ndizi nguvu za ziada ulizonazo zenye uwezo mkubwa wa kukupa mafanikio yoyote unayotaka katika maisha yako na kukufanya kuwa tajiri.
Kwa kujua hilo kuwa unazo nguvu hizo ambazo wengi hata hawazitambui, kuanzia sasa acha kutilia mashaka uwezo ulionao. Anza kujiwekea malengo na mikakati ya kufikia ndoto zako bila woga tena, kwani utakuwa unajua sasa kumbe mafanikio ni matokeo ya nguvu tunazitumia ndani mwetu kila siku na siyo suala la bahati kama wengi wanavyoikiri.

Unaweza ukawa pengine unajiuliza, ni ushahidi gani tunaouweza kuupata kuhusiana na kuwepo kweli kwa nguvu hizi? Ushahidi ni mwingi sana, kwetu wenyewe, kwa ndugu zetu, jamaa na jirani. Kama siyo sisi, watu hao wanaotuhusu au kutuzunguka wanaweza kuwa wameshawahi kutusimulia kuhusu kutokewa nazo.

Ukweli ni kwamba kuna nguvu nyingi sana ndani mwetu na nguvu hizi zote kama tutaweza kuzitumia vizuri zitakuwa chazo cha kutuletea mafanikio makubwa sana katika maisha yetu. Kitu cha msingi tambua kuwa zipo na kaa katika mkabala wa kufikiri chanya ili uweze kuzitumia kwa manufaa na kukupa mafanikio makubwa katika maisha yako.

Kwa makala nyingine nzuri hakikisha unatembelea DIRA YA MAFANIKIO kujifunza zaidi.

TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YAKO YA MAFANIKIO.

IMANI NGWANGWALU,
0713 048035,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: