USHAURI; Jinsi Unavyoweza Kuondokana Na Changamoto Za Kuendesha Biashara Na Kuweza Kufikia Mafanikio Makubwa.

KARIBU KWENYE SEMINA YA MAFANIKIO KUPITIA BIASHARA MWAKA 2015.

AMKA CONSULTANTS imekuandalia semina ya mafanikio kwenye biashara mwaka 2015. Katika semina hii utajifunz amambo yote muhimu yatakayokuwezesha kuanza, kukuza na kufikia mafanikio kwenye biashara yako. Semina itaanza tarehe 04/05/2015 na itaendeshwa kwa mwezi mzima kwa njia ya mtandao(yaani email). Mwisho wa kujiunga na semina hii ni tarehe 01/05/2015. Wahi sasa kujiunga ili upate maarifa yatakayokuwezesha kufanikiwa kwenye biashara. Kwa maelezo zaidi na jinsi ya kujiunga bonyeza maandishi haya.

Watu wengi sana hufikiri kwamba changamoto pekee wanayoipata kwenye biashara ni mtaji. Ndio maana wengi hulalamika kwamba wakipata mtaji tu basi wanaweza kufanya biashara na kufanikiwa. Wanaendelea kufikiri hivi mpaka pale wanapopata mtaji na kuingia kwenye biashara. Hapa ndipo wanapokaribishwa na changamoto nyingi zaidi na wanabaki wakishangaa. Mtu alipanga kwmaba kwa kipindi fulani atakuwa amefikia kiwango kikubwa kwenye biashara ila muda unapita na haoni mafanikio.

Wakati mwingine mtu anakuwa anafikiri akipata tu mtaji anaweza kuingia kwenye biashara yoyote, ila pale anapopata mtaji ndio anaanza kujikuta yupo njia panda. Anashindwa kujua ni biashara gani afanye, kwa sababu kwa wakati huo kila biashara inaonekana ni nzuri. Na kitu kikubwa anachofikiria wakati huo ni biashara ipi itampatia faida kubwa.

Leo katika kipengele hiki cha ushauri wa changamoto zinazotuzuia kufikia mafanikio tutaangalia mambo haya mawili;

1. Ni biashara gani ufanye pale ambapo tayari una mtaji.

2. Unawezaje kuikuza biashara yako licha ya kuwa na changamoto.

Ni biashara gani ufanye pale ambapo tayari una mtaji?

Hili ni swali linalowatatiza watu wengi sana. Mtu anaweza kuwa na wazo la biashara kabla hajapata mtaji, ila akishakuwa nao mawazo yanaanza kubadilika na kuona kuna mawazo mengine mazuri zaidi.

Kabla hatujaangalia ni biashara gani ufanye, hebu tuone maoni ya msomaji mwenzetu;

hbr bro

nimeajiriwa  na ni mwaka wa 4 ila bado hali yangu si nzuri ki maisha kabsa,mmoja ya tatizo ni mkopo nilichukua mkopo nikanunua eneo kama heka mbili na saiz lipo na mkopo nimemaliza ila sasa nataka kukopa ili nifungue biashara ya kuniweka huru kabsa,

sasa unaweza kunipa ushauri zaidi, kwan kuna rafiki yangu alinipa plan ya kufanya kilimo cha ufuta maeneo ya mbeya ila mi nipo mwanza,na pia kuna ufungaji wa kuku wa kienyeji ebu tupeane ushauri kdg kwani bado niko job na natakiwa kufungua ofisi huku naendelea na kazi mpk hapo itakapo simamama kabsa ndiyo aweza kuacha kazi n kujikita kwenye ofc yangu.

Hongera ndugu kwa kuwa na mipango mizuri ya kuanzisha biashara ambayo itakuweka uhuru ukizingatia ajira haiwezi kufanya hivyo. Ila hapa una changamoto nne kubwa.

Changamoto ya kwanza ni kutokujua biashara gani ufanye. Kufanya biashara kwa sababu kunamtu amekuambia biashara hiyo inalipa ni kitu hatari sana kufanya kwenye maisha yako. Labda kama mtu huyo ameshafanya biashara hiyo na imempa faida na anaweza kukuonesha hatua kwa hatua ni kitu gani alifanya mpaka kupata mafanikio. Nakuambia hivi kwa sababu watanzania tumekuwa washauri wazuri sana kwa mambo ambayo tumesikia tu. Mtu anasikia watu wakisema kilimo cha ufuta kinalipa sana halafu anakuja kukuhadithia na wewe. Wewe ukiingia kichwa kichwa kwenye kilimo hiko unaweza kujikuta kwneye wakati mgumu sana. Hakuna kitu ambacho hakina changamoto zake hivyo kabla hujaingia kwenye biashara yoyote hakikisha unaijua vizuri ili usije kujikuta kwenye hali ambayo hukutarajia.

Changamoto ya pili ni kutaka kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja. Kama ndio unaanza biashara, ni bora ufanye jambo moja kwa wakati. Hii itakuwezesha kupata nafasi ya kujifunza vizuri kwa kile ulichoanza kufanya, kujua changamoto zake na jinsi ya kuzitatua. Ni hatari sana pale ambapo utakuwa unafuga kuku na huku unalima ufuta, kuku wapate ugonjwa ambao unakuhitaji kuushughulikia huko ufuta nao umepata ugionjwa, au hakuna mvua na huna maji ya kumwagilia. Utakuwa unahangaika huku na huko na mwishowe utakosa yote. Fanya jambo moja, likishaonesha mafanikio na kusimama vizuri nenda kwenye jambo jingine.

Changamoto ya tatu ni kufanya biashara ukiwa mbali. Uko mwanza na unataka kulima ufuta mbeya, naweza kukushauri bora ule hiyo fedha ujue hata ulikula kuliko kuipoteza kirahisi hivyo. Kamwe usifanye biashara ya kuendesha kwenye simu, mwanza na mbeya ni mbali sana na wewe bado upo kwenye ajira. Kwa nafasi kubwa utakuwa unaendesha kilimo chako kwa njia ya simu. Utaona ni rahisi sasa hivi kwenye mipango yako, ila utakapoingia ndio utauona uhalisia wenyewe. Utapiga simu na utahakikishiwa maendeleo ni mazuri na kuambiwa utume fedha zaidi. Siku utakapofika shambani unaweza kuangua kilio, yale uliyotarajia sio ambayo utayakuta. Hakikisha biashara unayoanzisha ipo karibu na wewe na unawez akuiona mara kwa mara.

Changamoto ya nne ni kuwa kwenye ajira bado. Unapoanza biashara unahitaji muda wa kuijua biashara hiyo kw akina sana. Sasa kama ajira itakuw aimekubana sana utakosa nafasi hiyo na unaweza usiijue biashara yako vizuri. Hakikisha biashara yako inakuw akaribu sana na wewe na pia unapata muda wa kutosha wa kuifuatilia na kuisimamia. Sikiliza, hakuna mtu mwenye uchungu na fedha zako unazoweka kwenye biashara kama wewe mwenyewe, hivyo kama utashindwa kuisimamia vizuri unaruhusu watu wakurudishe nyuma.

Unawezaje kuikuza biashara yako licha ya kuwa na changamoto.

Kama tulivyojadili pale juu, unaweza kuona changamoto yako kwenye biashara ni mtaji tu na kwamba ukiupata kila kitu kitakuwa safi. Ila utakapoingia kwenye biashara ndio utaona kwmaba mtaji ulikuwa sehemu moja tu tena ndogo ya wewe kufikia mafaikio kupitia biashara. Kabla hatujaona ni jinsi gani unaweza kuepukana na changamoto, tuone maoni ya msomaji mwenzetu;

Leo nimesoma mafundisho yako mengi sana,kwa kweli nimejifunza vitu vingi.

nina swali 1. mi nimefungua darasa la computer toka mwaka jana mwezi wa 12 lkn hadi hivi sasa ninajumla ya wanafunzi 4 tu,na matarajio yangu ilikuwa ni kupata wanafunzi zaidi ya 25,je nifanyeje ili hili darasa liweze kufikia hiyo idadi ,ikiwezekana hata kuzidi hapo? nipo (W) ya Serengeti.

Kama tulivyoona kwa msomaji mwenzetu hapo juu, alishaanza biashara yake na alikuwa na mipango mizuri sana kwenye biashara hiyo. Ila ameingia kweye biashara na karibu miezi sita sasa hajafikia hata robo ya mpango wa wateja aliokuwa nao. Huenda msomaji mwenzetu alikuwa na mawazo ambayo watu wengi wamekuwa nayo kwmaba ukishakuw ana mtaji tu na ukaanza biashara basi watu lazima watakuja. Haya ni mawazo ya kizamani ambayo yamewaingiza wengi kwenye changamoto kubwa sana.

Kuna mambo mengi unatakiwa kufanya kabla hujaamua kuingia kwenye biashara biashara yoyote. Na jambo kubwa kabisa ni soko.

Je kuna soko la biashara yako, hili ni swali muhimu sana unalotakiwa kulijibu. Kama hakuna soko, usipoteze fedha na muda wako. Kama jibu ni ndio kuna soko, je soko lina ukubwa wa kutosha. Unaweza kukuta biashara unayotaka kufanya ina soko, ila ni dogo sana kiasi cha kukufanya ushindwe kufikia malengo yako. Kama jibu ni ndio soko ni kubw ana la kutosha kuna swali jingine muhimu unatakiw akujibu;

Je nawezaje kulifikia soko hilo? Hapa sasa ndio unapokuja na mpango mzuri wa kutangaza na kuvutia wateja kwneye biashara yako. Hapa unajenga wateja wanaokuamini na wanaoweza kuwaambia wengine kuhusu biashara yako. Hapa unayajua matatizo ya wateja wako na kuweza kuyatatua kwa biashara unayofanya.

Ni kazi ndefu na sio rahisi tu kama watu wengi wanavyofikiri.

Kwa changamoto zote za biashara tulizojadili leo na nyingine nyingi, unahitaji kuw ana elimu ya biashara na kuacha kufanya biashara kwa mazoea. Kufanya biashara kwa mazoea kunakufa kwa kasi kubwa sana na watu wote ambao wanaendelea kufanya hivyo wapo kwenye hatari kubwa ya kupata hasara na biashara zao kufa kabisa. Tupo kwenye ulimwengu ambao ushindani wa kibiashara ni mkubwa na kama hujajiandaa vizuri unaweza kupotezwa haraka sana.

Ili uweze kuondokana na changamoto hizi na upate maarifa ya kuzitatua, AMKA CONSULTANTS imekuandalia semina ya biashara itakayofanyika mwezi wa tano. Semina hii itafanyika kwa njia ya mtandao na masomo yatatumwa kwa email. Katika semina hii utajifunz amambo yote muhimu katika kuanza, kukuza na kufikia mafanikio makubw akwenye biashara yako. Unaweza kujiunga na semina hii popote ulipo Tanzania au hata duniani. Ili kushiriki semina hii tuma ada ya semina ambayo ni tsh elfu 30 kwenye namba 0755953887/0717396253 kisha tuma jina lako na email kw aujumbe mfupi na utaandikishwa kwenye semina hii. Semina itaanza rasmi tarehe 04/05/2015 ila mwisho wa kujiunga ni ijumaa ya wiki hii tarehe 01/05/2015. Muda wa kujiunga ukiisha utakuwa umekosa fursa hii ya kipekee ya kufanikiwa kwenye biashara. Pia nafasi za kushiriki ni chache ili kuweza kutoa darasa zuri na kujibu maswali ya washiriki wote. Wahi nafasi yako kw akufanya malipo yako leo. Karibu sana.

Nakutakia kila la kheri kwenye mafanikio ya biashara yako.

TUPO PAMOJA

Makirita Amani 

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kama una changamoto ambayo inakuzuia kufikia malengo yako unaweza kuitoa kwa kubonyeza maandishi haya na kujaza fomu. Changamoto yako inaweza kuwa moja ya makala zijazo kila siku ya jumatatu. Kama unahitaji ushauri wa haraka wasiliana na mimi kwa email makirita@kisimachamaarifa.co.tz au simu 0717396253/0755953887.

Kabla ya kutoa changamoto yako pitia changamoto ambazo tayari zimejadiliwa ili usirudie ambayo imeshajadiliwa. Bonyeza hapa kusoma changamoto zilizojadiliwa.

kitabu-kava-tangazo4322

 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s