Taarifa Muhimu Kwa Wasomaji Wa AMKA MTANZANIA.

Wewe ni msomaji wa AMKA MTANZANIA na ni mmoja wa watanzania wachache ambao wameamua kushika hatamu ya maisha yao na sio kukaa tu na kulalamika. Au kuwa na matumaini kwamba mambo yatakwenda vizuri. Hongera sana kwa maamuzi hayo mazuri uliyofanya kwenye maisha yako.

Nakushukuru tena kwa kuendelea kuwa msomaji wa mtandao huu ambao umejikita katika kukupatia wewe maarifa sahihi yanayokuwezesha wewe kuboresha kazi yako, baishara yako na maisha yako kwa ujumla ili uweze kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako. Mpaka sasa unajua kwmaba mafanikio makubw ani haki yako na hakuna wachache waliopewa upendeleo huo. Ila unajua unahitaji kuweka juhudi ili kuweza kufikia mafanikio hayo, nakupenda sana kw akulijua hilo.

Pia nina hakika unayafanyia kazi mambo unayojifunza kwenye  mtandao huu pamoja na mitandao mingine iliyopo chini ya AMKA CONSULTANTS, kama JIONGEZE UFAHAMU, KISIMA CHA MAARIFA, na MAKIRITA AMANI. Lengo la mitandao hii yote ni kukupa wewe maarifa ambayo yatakuwezesha kuboresha maisha yako. Ni nani asiyependa kuwa na maisha bora? Sijawahi kukutana na mtu yeyote akaniambia mimi nataka maisha yangu yawe hovyo, sitaki maisha bora, ndio maana naamini wewe msomaji unataka kuboresha maisha yako na hivyo tunakupatia maarifa ya kukuwezesha kufanya hivyo.

Kwa bahati mbaya kabisa hakuna anayeweza kukuletea maisha hayo bora, hakuna. Watu waliambiwa kwamba wataletewa maisha bora kwa kila mtanzania, wakafurahia sana, ila sasa miaka kumi imepita na wameambiwa hamkuielewa vizuri kauli ile. Wewe huhitaji kuielewa au kutokuielewa kauli, unachohitaji ni kuwa na maarifa sahihi ambayo ukiyafanyia kazi maisha yako yatakuwa bora. Na hii ndio kazi yetu kubwa.

Taarifa muhimu ninayotaka kukufikishia wewe msomaji wa AMKA MTANZANIA ni taarifa mbili muhimu sana.

Kwanza ni kuhusu semina mbalimbali ambazo tumekuwa tunazitoa kwa njia ya mtandao. Tumekuwa tukitoa muda wa kutosha wa kujiandikisha wkenye semina hizi, ila watu wengi hawafanyi hivyo, ila muda unapokwisha ndio watu hutaka kujiandikisha kwa sababu wengi wanakuw ahawajapata ujumbe wa semina. Tumekuwa tunapata wakati mgumu sana kwa sababu mipango yetu haiendi vizuri pale ambapo watu wanajiunga baadae. Lakini tumekuwa tukihakikisha watu wanapata mafunzo haya, kwa sababu lengo letu ni watu kupata maarifa, na kwa sababu tunawapenda sana basi tunalazimika kufanya kila lililopo ndani ya uwezo wetu kuhakikisha mnapata kile tunachotoa.

SOMA; Jambo Moja Muhimu La Kuzingatia Ili Uwe Tajiri.

Taarifa za semina yoyote ile inayotolewa kwa njia ya mtandao, huwa inatolewa wiki mbili kabla ya semina kuanza. Hii ina maana kwamba kwa msomaji wa kawaida wa mtandao huu atakutana na taarifa hiyo na kuiweka maanani kama kweli anataka kushiriki. Licha ya wiki mbili kabla, taarifa huendelea kutolewa karibu kila siku ili kuwakumbusha watu wanaotaka kushiriki. Kutokana na wengi kutopata taarifa kwa wakati, tumefanya uchunguzi wa kina na kuona huenda kuna matatizo mawili;

1. Watu hawasomi makala mara kwa mara kwenye mtandao huu. Kama hufanyi hivi unakosa vitu vizuri sana. Kila siku ya wiki, kunawekwa makala mpya kwenye mtandao huu, tafadhali jijengee utaratibu wakusoma blog hii kila siku na usiache hata siku moja. Maarifa yoyote ni bora kuliko kutokupata maarifa kabisa.

2. Watu hawafungui email zinazotumwa. Kwanza kama hujajiandikisha kwenye mfumo wetu wa kutumiwa email bonyeza hapa na uweke email yako. Na kama upo kwenye mfumo wetu wa email hakikisha unafungua email tunazokutumia. Hizi email tunatuma kwa mfumo ambao tunaulipia na hivyo mfumo huu huchagua watu gani wapokee email inayotumwa. Kama hujafungua email tano zilizotumwa kwako, basi hakuna email nyingine itakayokuja tena kwako. Kila wiki tunatuma email tatu, jumatatu, jumatano na ijumaa. Baadhi ya wiki tunaweza kuongeza email, ila mara nyingi ndio hivyo. Jitahidi sana katika siku hizo ambazo email zinatumwa ufungue email yako na kusoma.

Kama email yako umejiunga kwenye huduma nyingi ambazo zinakujazia email za matangazo, jiondoe kwenye huduma hizi(unsubscribe) ila zisikuzuie wewe kupata taarifa muhimu kutoka kwetu.

Kama hujafungua email nyingi kutoka kwetu, nenda kafungue email za nyuma sasa na mfumo utaona upo na kuendelea kukutumia email.

Nashukuru sana kwa ushirikiano ambao umeendelea kuonesha na tunakuahidi kuwa pamoja na wewe kwenye safari yako ya mafanikio.

SOMA; KITABU; Jinsi Ya Kufaidika Na Mabadiliko Yanayotokea Kwenye Maisha.

Taarifa ya pili ninayopenda kuchukua nafasi hii kuitoa ni kuhusu watu ambao wanapenda kuandika. Kama wewe ni msomaji wa AMKA MTANZANIA na unablog yako au unapenda kuandika, basi karibu sana. Blog yetu ya JIONGEZE UFAHAMU, inapokea makala kutoka wka watu mbalimbali. Tunaijenga blog hii iwe ni ya waandishi mbalimbali ambao wana ujumbe wanaotaka uifikie jamii. Kwa kuiandikia blog hii, utajijengea utaratibu wa kuandika na pia utapata wasomaji ambao watakuwa wanaenda na wewe na kukuamini pia. Kama una blog, utapata watembeleaji wengine kutoka kwneye blog hii. Kama ungependa kuwa mmoja wa waandishi wa blog hii, andika email kwenda amakirita@gmail.com Aina ya makala unayotakiw akuandika ni iwe ya kufundisha au kumpatia mtu maarifa na sio ya kulalamika au mambo mengine. Makala iandikwe kwa kiswahili sahihi na rahisi inayoweza kueleweka kwa kila mtu bial kujali kiwango chao cha elimu. Urefu wa makala usipungue maneno 500. Karibu sana tufanye kazi ya kutoa maarifa yatakayowawezesha wengine kuchukua hatua ya kuboresha maisha yao.

Nawatakia wasomaji wote kila la kheri katika kuboresha maisha yako.

TUPO PAMOJA.

kitabu-kava-tangazo4322

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: