USHAURI; Changamoto Ya Wategemezi Wengi Na Changamoto Ya Kipato Kuwa Sawa Na Matumizi.

Habari za leo mpenzi msomaji wa AMKA MTANZANIA karibu tena kwneye kipengele hiki cha ushauri wa changamoto mbalimbali zinazotuzuia kufikia mafanikio makubwa.

Changamoto ni sehemu ya maisha na maisha yoyote ambayo hayana changamoto ni maisha ambayo hayakui, yaani yamebaki pale pale. Huwezi kufikia mafanikio maka hukutani na changamoto. Unapojaribu kufanya mambo mapya ili ufikie mafanikio makubwa kuliko uliyonayo sasa ni lazima utakutana na hali ambazo hukuzitegemea.

Leo katika kipengele hiki cha changamoto za mafanikio, tutaangalia changamoto ambazo yumewahi kuzipatia ufumbuzi hapa kwenye kipengele hiki ila bado wasomaji wanaendelea kuuliza. Kwa kuwa lengo letu ni kutoa maarifa kwa wasomaji wote, basi tunahakikisha kila ambaye anahitaji kupata maarifa sisi hatuwi kikwazo kwake.

Leo tutaangalia changamoto mbili; changamoto ya kwanz ani kuw ana wategemezi wengi na changamoto ya pili ni kipato kuwa sawa na matumizi.

Tuanze na changamoto ya kwanza na haya hapa ndio tumepokea kutoka kw amsomaji mwenzetu;

Habari kaka, hongera kwa kazi nzuri unayofanya. Samahani kama utakuwa ukijibu swali hili kwa mara ya pili kwani nimejaribu kuangalia katika makala zilizopita na sikuona swali kama hili.
Changamoto yangu ni moja, je ni namna gani nitaweza kuondokana na watu tegemezi (dependants, ambao si wanangu au wale ambao katika hali ya kawaida wangekuwa ni jukumu langu)?
Mimi ni muajiriwa, lakini pia nina biashara zangu ambazo zinaniingizia kipato cha ziada.Ukweli ni kwamba kwa vipato vyote hivi ninavyopata, kama ingekuwa ni mimi na familia yangu tu, basi ningekuwa naishi comfortably na pengine hata kutoingia katika madeni mengine yasiyo ya lazima.Changamoto yangu kubwa ni kubwa nina watu(ndugu wa karibu ambao kwa kiasi kikubwa sana wananitegemea kifedha). Kutokana na ukaribu nilio nao kwao na kutokana na matatizo ambayo huwa wananiambia, huwa najikuta tu nalazimika kuwasaidia. Hii imekuwa ikichangia kwa kiasi kikubwa kurudisha nyuma malengo yangu ya kibiashara kwani huwa inanilazimu kutumia savings zangu kwa kuwasaidia wao. Je nitawezaje kuondokana na changamoto hii? Je inawezekana kweli kuondokana na changamoto hii pasipo kutoharibu mahusiano yangu na wao?

Habari Ndugu, pole kwa changamoto hii kubwa ambayo unaipitia. Ndio tulishajadili changamoto hii na tuliona njia ambazo mtu aliyepo kwneye changamoto hii anaweza kuzitumia na akapunguza au kumaliza kabisa changamoto hiyo. Na ndio njia hizo hazitoharibu mahusiano yako na watu hao ambao ni wa karibu sana kwako.

Kuzijua njia hizo fungua makala hii; Ushauri; Ni Jinsi Gani Unaweza Kufikia Malengo Yako Kama Una Idadi Kubwa Ya Wategemezi?

 

Changamoto ya pili ni kuhusu mapato kuwa sawa na matumizi, na haya hapa ndio maoni ya msomaji mwenzetu;

Nafanya kazi ila mshahara wangu kinachoingia ndo kinachotoka. Yaani MAPATO=MATUMIZI Na natamani kufanya biashara ila sina hela.

Ili kuweza kupiga hatua kwenye maisha, ni muhimu sana mapato yawe zaidi ya matumizi. Kile ambacho kinazidi kwenye mapato yako ukiondoa matumizi ndio unachoweza kufanyia shughuli mbalimbali za kimaendeleo. Lakini watu wengi wamekuwa na matumizi makubwa sana ambayo yamelingana na mapato au wakati mwingine kuzidi mapato na hivyo mtu kuingia kwneye madeni.

Kuna vitu vingi vinavyosababisha hali hii, ikiwepo kipato kidogo, matumizi makubwa, kukosa nidhamu ya fedha, kushindwa kujilipa wewe kwanza na mengine mengi. Kuondokana na changamoto hii ambayo ni kikwazo kufikia mafanikio makubwa, unahitaji kufanya mambo matatu makubwa.

Kwanza ni kuongeza kipato chako, unaweza kufanya hivi kwa kuongeza thamani kwenye kazi unayofanya sasa na hivyo kuongezewa mashahara au kutafuta kitu cha ziada cha kufanya ili kutengeneza kipato cha ziada. Kitu cha ziada kinaweza kuwa biashara au uwekezaji.

Pili ni kudhibiti matumizi yako, katika wakati wowote ule, kuna matumizi unayofanya ambayo sio ya msingi. Ondokana na matumizi haya ili uweze kuokoa fedha yako unayoendelea kupoteza.

Tatu ni kujijengea tabia ya kuweka akiba kabla hata hujafanya matumizi yoyote. Yaani unapopata kipato chako, weka kwanza pembeni kile ambacho unaweka akiba, unaweza kuanz ana asilimia 10 ya kipato chako halafu ndio ufanye matumizi. Ukianza na matumizi kabla ya kuweka akiba, itakuwa vigumu sana kwako kuweka akiba, maana matumizi huwa hayana mwisho.

Hapa nimeeleza kwa kifupi ila haya yote tumeshayajadili kwenye makala nitakazoweka link hapa, fungua na usome, utapata mwanga sana kwenye changamoto hii;

1. USHAURI; Hivi Ndivyo Unavyopoteza Fedha Bila Ya Wewe Mwenyewe Kujua.

2. USHAURI; Mambo Ya Kufanya Pale Matumizi Yanapokuwa Makubwa Kuliko Mapato.

3. Unawalipa watu wote kasoro huyu mmoja wa muhimu.

Nawatakia wote kila la kheri katika kutatua changamoto zinazowazuia kufikia mafanikio makubwa. Hakuna kinachoshindikana kama mtafanyia kazi yale ambayo mnajifunza.

TUPO PAMOJA

Makirita Amani 

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kama una changamoto ambayo inakuzuia kufikia malengo yako unaweza kuitoa kwa kubonyeza maandishi haya na kujaza fomu. Changamoto yako inaweza kuwa moja ya makala zijazo kila siku ya jumatatu. Kama unahitaji ushauri wa haraka wasiliana na mimi kwa email makirita@kisimachamaarifa.co.tz au simu 0717396253/0755953887.

Kabla ya kutoa changamoto yako pitia changamoto ambazo tayari zimejadiliwa ili usirudie ambayo imeshajadiliwa. Bonyeza hapa kusoma changamoto zilizojadiliwa.

kitabu-kava-tangazo4322

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s