Mafanikio Yako Yote Unayoyatafuta Yanaanzia Hapa.

Habari rafiki na mpenzi msomaji wa mtandao huu wa AMKA MTANZANIA. Ni siku nyingine tena ambapo tunakutana mimi na wewe kuweza kujadili namna ambavyo tunavyoweza kuboresha maisha yetu na kuwa ya mafanikio makubwa kabisa. Hili ni jukumu letu sote kuweza kuhakikisha tunayatengeneza maisha yetu na kuwa bora zaidi na ya mafanikio makubwa.
Hakuna ambaye anapenda maisha yake yakiwa hovyo ama yakiharibika huku akiyaangalia. Kila mtu kwa sehemu yake anapenda kuona mambo yake yakiwa safi, hii ndiyo furaha ambayo kila mtu anataka kuiona katika maisha yake. Kama ni hivyo ndio maana tunalazimika kujifunza kila siku ili kufanya maisha yetu kuwa bora zaidi ya jana tulivyokuwa.
Kwa moyo mkunjufu napenda kukuribisha katika makala ya leo ambapo leo tutajifunza juu ya mafanikio yako pale yanapoanzia na hatimaye kuwa makubwa. Ikumbukwe kuwa ni mara nyingi sana ambapo wengi wetu katika maisha yetu hujikuta ni watu wa kutafuta mafanikio makubwa pasipo kujua mafanikio hayo huwa yanaanzia wapi.
Wengi hujikuta ni watu wa kuumia moyo sana pale ambapo wanapoona mafanikio ya wengine ni makubwa sana. Watu hawa wanaumia kwa mambo mengi lakini mojawapo likiwani kuwa hawajui ni wapi pa kuanzia ili kufikia mafanikio hayo makubwa. Wengine kwa pupa hujikuta wakitaka kufanya mambo mengi sana ili kufanikiwa lakini wapi.
Kutokana na hilo wapo ambao hata hutamani kufanya chochote ilimradi tu afanikiwe. Hizo zote huwa ni harakati za kama vile za kutaka kulala maskini na kuamka tajiri. Lakini je, unajua ni wapi unapotakiwa kuanzia ili kuweza kujihakikishia mafanikio makubwa katika maisha yako. Hii huwa ndiyo shida ambayo wengi hawajui waanzie wapi. Na hufika mahali wengine huhisi wanahitaji muujiza katika hili.

Na kama umekuwa hujui hili au umekuwa ukitaka kutimiza malengo yako yako kwa haraka sana na kuona mafanikio makubwa katika maisha yako, ninachotaka kukukwambia malengo yako yote hayo ili uweze kuyafikia huwa hayaanzi mbali sana kama unavyofikiri. Mafanikio yako mara nyingi huwa yanaanza kwa hatua ndogo sana ambazo wakati mwingine huwa unazidharau. Hapa ndipo mafanikio yako makubwa huwa yanaanzia na siyo sehemu nyingine yoyote ile.
Hivyo, yale mabadiliko madogo ambayo huwa unayaona kama siyo mabadiliko kwako ndiyo unatakiwa kwanza kuyafanya. Kwanini? Kwa sababu hiyo ndiyo sehemu unayotakiwa kuanzia kwa ajili ya mafanikio makubwa. Kwa hiyo, ukiona unafanikiwa katika kidogo, elewa kabisa jiandae na mafanikio makubwa yanayokuja upande wako mara moja. Acha kudharau kitu, kwani upo kwenye mwelekeo sahihi wa mafanikio.
Hivi ndivyo mafanikio yako makubwa yanapoanzia kwa wewe kufanya mabadiliko kwa hatua ndogo tu. Kama imefika mahali unajiona kuwa kama huendi mbele sana jaribu kujichunguza je, kuna hatua zozote ndogo unazozipiga, kama jibu ni ndiyo basi upo kwenye njia sahihi ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa yanayokusubiri.
Kwa hiyo chochote unachokifanya hata kiwekidogo vipi kifanye kwa uaminifu na kwa ubora zaidi. Kama ni pesa unazo kidogo zitunze kwa uaminifu zaidi na usije ukazitumia hovyo. Kwani kuwa mwaminifu kwa kidogo iwe kwa jambo unalofanya ama utunzaji wa pesa kama nilivyosema hiyo ni dalili tosha kuwa hata ukiwa na kikubwa utaweza kukitendea haki vizuri na kufikia mafanikio makubwa.
Kila wakati hakikisha unakuwa mshindi katika kile kidogo unachofanya. Usikatishwe tamaa na chochote kama kweli unasonga mbele hata kwa  kidogokidogo wewe endelea kusonga mbele tu. Mafanikio yako yote makubwa yanaanzia kwa kuwa mshindi kwa mambo madogo tu. Ukiweza kufanya vizuri kwa mambo yako madogo hata makubwa utaweza. Hii ndiyo siri kubwa sana ya mafanikio unayotakiwa kuifahamu na kuifanyia kazi vizuri.
Kwa makala nyingine nzuri hakikisha unatembelea DIRA YA MAFANIKIO kujifunza zaidi.
TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YAKO YA MAFANIKIO,
IMANI NGWANGWALU,
0713 048035,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: