Kitabu hiki kinakupatia jibu la uwekezaji. Na hapa nimekuchambulia mambo 20 muhimu kutoka kwenye kitabu hiki. Yafanyie kazi na pia kisome kitabu hiki na vingine vya uwekezaji ili uweze kufnikiwa kupitia uwekezaji.
Mambo 20 niliyojifunza kwenye kitabu INVESTMENT ANSWER…
1. Uwekezaji ni sehemu muhimu sana kwenye kipato cha kila mmoja wetu hasa kwa siku za mbeleni ambapo hutakuwa na nguvu ya kuendelea kufanya kazi. Na hata kama umeajiriwa na unategemea kupata mafao, hayatakuwezesha kuendesha maisha yako kama unavyotaka.
#BOOK_INVESTMENT_ANSWER
2. Kama ushauri wako wa uwekezaji ni vyombo vya habari basi unapotea. Maana wakati watu wanasema uwekezaji fulani unalipa basi jua umeshachelewa.
#BOOK_INVESTMENT_ANSWER
3. Wakati mzuri wa kununua hisa ni pale ambapo kila mtu anauza. Na wakati mzuri wa kuuza hisa ni pale ambapo kila mtu ananunua.
Hii ndio siri kubwa ya wawekezaji wenye mafanikio.
#BOOK_INVESTMENT_ANSWER
4. Unapoingiza hisia kwenye uwekezaji ndio wakati ambapo unasindwa kufanya maamuzi sahihi. Mara zote ongozwa na misingi na sio hisia.
Ni rahisi sana kushawishika kuuza hisa pale ambapo kuna habari nyinginza hisa kushuka thamani. Lakini kufanya hivyo ndio kupata hasara zaidi.
#BOOK_INVESTMENT_ANSWER
5. Kuna washauri wa aina mbili kwenye uwekezaji. Kuna washauri ambao ni mawakala wa hisa, hawa wanalipwa kama ukinunua hisa ambazo wao ni mawakala. Na pia kuna washauri ambao wanajitegemea, wanatoa ushauri kulingana na utaalamu wao. Na hawalipwi kutokana na wewe unavyonunua.
Mara zote chukua ushauri wa wale ambao wanajitegemea. Kwa sababu kuchukua ushauri kwa wakala, atahakikisha unanunua ili yeye alipwe.
#BOOK_INVESTMENT_ANSWER
6. Uwekezaji kwenye hisa sio kitu kigumu kama watu wengi wanavyofikiri.
Hata wewe unaweza kuwa mwekezaji kwenye hisa na ukapata mafanikio makubwa.
Unahitaji kujifunza misingi ambayo utaifuata kweny uwekezaji wako.
#BOOK_INVESTMENT_ANSWER
7. Ni muhimu sana wewe kuanza kuwekeza kwenye hisa na amana nyingine sasa kwa sababu kadiri unavyoanza mapema na kuwepo kwenye uwekezaji kwa muda mrefu, ndivyo unavyokuza uwekezaji wako na kuwa na uhakika na maisha ya baadae.
8. Usimuachie mshauri wako wa uwekezaji mamlaka ya kufanya maamuzi yoyote kwenye uwekezaji wako. Hakikisha unashiriki kikamilifu kwenye uwekezaji wako ili kujua ni jinsi gani fedha zinavyokwenda.
#BOOK_INVESTMENT_ANSWER
9. Hakuna sehemu unayohitaji kuepuka kundi kama kwenye uwekezaji.
Ni rahisi sana kufanya kile ambacho kila mtu anafanya.
Ila kwenye uwekezaji, ukiona kitu kinafanywa na wengi, kuwa makini, usiingie kichwa kichwa.
#BOOK_INVESTMENT_ANSWER
10. Watu hujiuliza ni wakati gani sahihi wa kununua hisa na wakati gani sahihi wa kuuza.
Sasa kanuni hii hapa;
Wakati sahihi wa kuuza ni pale unapokuwa na fedha. Na wakati sahihi wa kuuza hisa ni pale unapohitaji fedha.
Usiuze au kununua hisa kwa sababu kila mtu anafanya hivyo. Utakuwa unajiingiza kwenye kushindwa.
#BOOK_INVESTMENT_ANSWER
11. Hakuna kitu kinachowaumiza watu kama kuona mtu wa karibu yao anafanikiwa wakati wao bado wanakazana. Hivyo washauri na wale wanaokuzunguka wawekeze. Au zungukwa na wawekezaji wenzako ili mpeane maarifa zaidi.
#BOOK_INVESTMENT_ANSWER
12. Vigezo vya kutumia wakati unachagua mshauri wa uwekezaji.
i. Falsafa yake kwenye uwekezaji.
ii. Uhusiano mzuri na uaminifu.
iii. Utaalamu na uzoefu.
iv. Aina ya wateja alionao sasa.
Fanya kazi ya ziada ili uweze kupata mshauri mzuri wa uwekezaji.
13. Kama unataka kuwekeza kwa muda mrefu basi unaweza kuwekeza sehemu hizi mbili.
i. Wekeza kwenye hisa, hapa unanunua hisa za kampuni nanouwa sehemu ya wamiliki. Hapa utapata faida kwenye ongezeko la thamani na pia kutokana na gawio la kila mwaka.
ii. Unaweza pia kuwekeza kwenye hati fungani(bonds) ambapo hapa utakuwa unalipwa kiasi fulani kila baada ya juda fulani uliopangwa.
#BOOK_INVESTMENT_ANSWER
14. Uwekezaji wa aina yoyote ile una hatari ya kupata hasara. Lakini jinsi uwekezaji unavyokuwa wa muda mrefu ndivyo hatari ya hasara inavyokuwa ndogo.
Kama uwekezaji unaleta faida kubwa kwa muda mfupi, jua pia hatari ya kupata hasara ni kubwa.
Kuwa macho na husisha akili yako, sio hisia zako.
#BOOK_INVESTMENT_ANSWER
15. Tofauti ya uwekezaji kwenye kampuni kubwa na kampuni ndogo.
Uwekezaji kwenge kampuni ndogo au changa una faida kubwa ila pia una hatari kubwa ya kupata hasara.
Uwekezaji kwenye kampuni kubwa, zenye uzoefu una ida kidogo ila pia hatari ya kupata hasara ni ndogo.
#BOOK_INVESTMENT_ANSWER
16. Tofauti ya uwekezaji kulingana na umri.
Kama bado umri wako ni mdogo, yaani bado hujastaafu, una uwezo wa kufanya kazi na kuingiza kipato. Wekeza kwenye eneo ambalo hutatoa fedha kwa angalau miaka kumi. Hapa uwekezaji wako utakua sana.
Kama wewe umri umekwenda, yaani umestaafu au unakaribia kustaafu wekeza mahali ambapo unaweza kupata gawio la mara kwa mara litakalokuwezesha kuendelea na maisha yako.
#BOOK_INVESTMENT_ANSWER
17. Ni vyema kuwekeza kwenye makampuni tofauti na hata kwenye uwekezaji tofauti. Hii itakuwezesha kutopata hasara kubwa kwa wakati mmoja. Kama uwekezaji mmoja ukiwa na hasara mwingine utakuwa unalipa.
#BOOK_INVESTMENT_ANSWER
18. Usiwe mwekezaji wa kulivizia soko, kwa kufanya hivi utapoteza muda wako mwingi na huwezi kupata faida.
Hakuna anayeweza kuitabiri kesho kwa uhakika, hivyo usinunue hisa kwa sababu unatabiri kesho zitapanda, ila nunua kwa sababi utakaa nazo kwa muda.
#BOOK_INVESTMENT_ANSWER
19. Ushauri muhimu sana kuhusu uwekezaji ambao uondoke nao hapa leo;
1. Anza mapema, kama bado hujaanza kuwekeza anza sasa, unasubiri nini?
2. Jifunze kuhusu uwekezaji. Soma vitabu vya uwekezaji, jua mabadiliko ya uchumi na jua yale maeneo unayowekeza.
3. Usiendeshwe na tamaa. Watu wanapotaharuki na kuuza au kununua, wewe tulia na fanya uwekezaji wako kwa akili sio hisia.
#BOOK_INVESTMENT_ANSWER
20. Kila mtu anaweza kufanikiwa kupitia uwekezaji. Na dunia ya sasa kila kitu kipo wazi, ni wewe tu uchague mwenyewe kutokufanikiwa.
Wekeza wekeza wekeza, miaka kumi ijayo utajuta sana utakapokumbuka kwamba uliambiwa uwekeze leo ila ukapuuza.
#BOOK_INVESTMENT_ANSWER
Kupata kitabu hiki ili kujifunza zaidi BONYEZA MAANDISHI HAYA na kipakue.
Je ni yapi utaanza kuyafanyia kazi sasa? Tushirikishe kwenye maoni hapo chini.
CRDB ni kati ya bank zinazofanya vizuri hapa Tanzania. Vipi hisa zake, kwa nini thamani iko chini na je gawiwo linatoka mara ngapi kwa mwaka na nono kiasi gani?
Nitawapataje washauri wa kujitegemea?
LikeLike
Habari Geofrey,
Ni kweli CRDB ni benki inayofanya vizuri.
Hisa zake zipo chini kwa sasa, na hii ni kwa karibu makampuni yote. Hali ya uchumi kwa sasa nchini haiendi vizuri na hivyo soko la hisa pia limedorora.
Crdb wanatoa gawio mara mbili kwa mwaka. Kiasi cha gawio inategemea faida iliyopatikana.
Kuhusu washauri wa kujitegemea kuhusu uwekezaji kwenye hisa, ukienda kwenye kampuni za brokers wa dse, kama solomon, wanashauri kuhusu hisa zipi nzuri kununua na wanakuonesha trend.
LikeLike