Kama Unataka kufanikiwa, Ni Lazima Uanze na Kitu Hiki Kwanza.

Ni mara nyingi wengi wetu umekuwa ukisikia tukijisemea sisi wenyewe ama kuwaambia jirani zetu kuwa ‘ni lazima mwaka huu nitafanya hili na lile mpaka kuhakikisha malengo yangu yanatimia’. Ni mipango ambayo huwa tunakuwa tunahamasa nayo na kutaka kuitekeleza kwa namna yoyote ile lakini ilimradi ifanikiwe.
Lakini kitu cha kushangaza hujikuta wengi wetu ile mipango mizuri ambayo huwa tumejiwekea huwa hatuitekelezi  na kujikuta siku zimekwenda na matokeo yake tunaanza kushangaa nini kilitokea. Kama unafikiri nakutania hebu jaribu kuangalia na kuchunguza mipango uliyojiwekea wakati mwaka huu unaanza, ni mingapi umeitekeleza tayari?
Kwa wengi utakuta mipango yao mingi imeishia kati na kujikuta ni watu wa kulalamika na kulaumu kila hali ambayo wanaijua wao kuwa ndiyo imewakwamisha. Matokeo yake hujikuta ni watu sasa wa kuishi kwa matarajio sana kuwa siku moja nitafanikiwa katika hili, na kusahau kujiuliza hiyo siku moja itafika lini katika maisha yao.
Kutokana na hali hiyo mabadiliko kwa watu hawa yamekuwa hayaonekani katika maisha yao, zaidi tu ya ahadi nyingi wanazojipa wao wenyewe kuwa nitafanya hiki wiki ijayo, mwezi ujao au mwaka ujao. Matokeo yake siku, wiki, miezi na hata miaka hiyo pia imekuwa ikifika lakini hakuna kilichotokea cha kuweza kubadili maisha yao.

Haya ni maisha ambayo wengi wamekuwa nayo. Unaweza ukawa wewe au jirani yako, lakini uhakika nilionao kwa sehemu maisha hayo unayajua kama siyo kwako hata kwa wengine umeyaona. Je, umeshawahi kujiuliza ni kitu gani hasa kinachopelekea hali kama hii kuweza kutokea?
Kwa vyovyote vile iwavyo mabadiliko au mafanikio yoyote unayotaka kuwa nayo yanaanza na uchaguzi. Hiki ndicho kitu usichokijua. Ni sawa unaweza ukawa umejiwekea malengo mazuri lakini kama huna uchaguzi sahihi huwezi kufikia malengo hayo. Uchaguzi ndiyo kitu pekee ambacho unaweza ukaanza nacho kama mtaji wako wa kwaza, kama kweli una nia ya kufikia mafanikio ya kweli.
Hakuna mafanikio ambayo unaweza ukayapata katika katika maisha yako bila ya kuchagua. Mimi na wewe tupo hivi kutokana na uchaguzi tulioufanya kipindi cha nyuma katika maisha yetu. Ukiamua leo kuwa unataka kufanikiwa  usibabaike sana pengine na hali mbaya ya maisha uliyonayo, anza kufanya uchaguzi sahihi wa kukufikisha kwenye maisha unayotaka.
Kumbuka kuwa ukiona leo hii upo kwenye kivuli cha mti, elewa kuna mtu ambaye aliupanda mti huo miaka mingi iliyopita. Hivyo ndivyo maisha yetu jinsi yalivyo. Tunawaona watu wamefanikiwa  ni kwa sababu walichagua hivyo kufanikiwa miaka iliyopita. Kilichowafikisha hapo si nguvu za uchawi au miujiza bali ni uchaguzi sahihi ambao walikuwa wakiufanya kila mara katika maisha yao.
Kama hupendi maisha uliyonayo sasa, hiyo isiwe shida kwako. Chagua maisha unayotaka kuwa nayo, kisha chukua hatua na kuamua kwa dhati kutoka moyoni kwako kuwa ni lazima uyafikie. Kwa kufanya hivyo hata ndoto zako ziwe kubwa vipi ni lazima utazifikia. Hii yote ni kwa sababu utakua umefanya uchaguzi sahihi wa kukupeleka kwenye mafanikio unayoyataka.
Wewe siyo jiwe ambalo haliweza kubadilika ama kutoka sehemu lilipo. Kwa namna yoyote ile unauwezo wa kubadili maisha yako utakavyo wewe. Badilika kwa kufanya uchaguzi sahihi wa maisha yako. Acha kufanya uchaguzi kimakosa au kusema ilikuwa bahati mbaya. Unachotakiwa kukumbuka kuwa kila unachokifanya unakuwa umekichagua tayari na kinamatokeo katika maisha yako yawe mazuri au mabaya lakini matokeo yapo.
Kitu muhimu na cha kukumbuka kwako kuwa, mafanikio yoyote unayoyata ni lazima yanaanza na uchaguzi unaoufanya kila siku na hakuna ubishi juu ya hilo. Kama ni hivyo, tunalazimika kufanya uchaguzi utakayoyapa maisha yetu furaha na mafanikio makubwa na sio vinginevyo. Hii ndiyo siri ya mafanikio pia unayotakiwa kuijua pia ili uweze kufanikiwa zaidi.
Tunakitakia kila la kheri katika safari yako ya mafanikio iwe ya ushindi, endelea kutembelea AMKA MTANZANIA kujifunza kila siku.
Kwa makala nyingine nzuri hakikisha unatembelea DIRA YA MAFANIKIO kujifunza na kuhamasika zaidi.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
07 13 04 80 35,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: