Mafanikio ni safari na kama tunavyojua kuwa katika safari kuna changamoto nyingi, changamoto hizo zinaweza kuwa barabara mbovu, au gari kuharibika na mengine mengi yanayohusiana na changamoto za safari.
Mara nyingi dereva anapotaka kuanza safari lazima kwanza alikague gari lake na kuhakikisha kuwa amebeba baadhi ya vifaa vya akiba kama vile tairi, spana na nk. Ili viweze kumsaidia katika safari yake pindi tu gari linapopata hitilafu katika safari. Hivyo basi kutokana na akiba ya vifaa alivyowekea vitamsaidia kutatua tatizo.

 
SOMA; Hivi Ndivyo Unavyoweza Kutajirika Kwa Kuanza Na Shilingi Elfu Moja.
Kwa hiyo katika safari ya mafanikio tunapaswa tuwe spea tairi yaani katika lugha ya kawaida tuweke AKIBA. Tunapaswa kujiwekea akiba kadiri tuwezavyo jinsi unavyopata ndivyo unatakiwa kuweka akiba. Haijalishi unapata kipato kikubwa kiasi gani au kidogo kiasi gani yakupasa uweke akiba ili uweze kufika katika safari yako ya mafanikio.
Mtu ambaye anapata hela katika kipato chake na kuitumia yote bila kuweka akiba ana dalili mbaya sana ya kuangukia katika madeni pindi anapopatwa na dharura ya ghafla na huku akiwa hana hata akiba. Kwa hiyo huwezi kufikia katika utajiri au kuwa na uhuru wa kifedha kama siyo mtu wa kuweka akiba.
Uwe ni mfanyabiashara, mwajiriwa, mjasiriamali na kadhalika huna budi kuweka akiba. Toa sehemu ya kipato chako kabla ya kufanya matumizi mengine na weka akiba usifanye matumizi yote ndio uweke akiba yaani hela inayobakia weka kwanza akiba ndio uendelee na mambo mengine.
SOMA; Hakika Ukifa Masikini Umejitakia Mwenyewe.
Hakuna mtu yeyote ambaye anaweza kuendelea duniani pasipo kuweka akiba. Katika maswala ya uchumi na maendeleo kuna vitu vitatu ambavyo unapaswa kuvifahamu navyo ni;
i) Kipato
ii) Matumizi
iii) Akiba
Hivi vitu vitatu jinsi gani vinavyotumika ndivyo vitakufanya wewe ubaki na pesa uweze kufanya kitu cha nne ambacho kinaitwa KUWEKEZA. Moja ya sababu ya watu wengi kwani ni wanaingia katika madeni ni kwa sababu ya kutoweka akiba. Kutoweka akiba ni ishara ya wewe kwamba huweki mipango ya baadae yaani huna plan.
Hivyo basi, kuna faida nyingi za kuweka akiba ambazo hazihesabiki. Kama ulikuwa huweki akiba anza leo kuweka akiba. Kuna aina mbili za watu, watu ambao wanafahamu umuhimu wa akiba ambao wanajiandaa kwa ajili ya matumizi ya baadae mtu ambaye anajitambua pia kuna watu ambao hawatambui umuhimu wa akiba.
Akiba haiozi, akiba ni hazina yako, akiba ni amana yako.
Makala hii imeandikwa na Deogratius Kessy ambaye ni mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali, unaweza kuwasiliana naye kupitia namba 0717101505 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com au unaweza kutembelea tovuti yake www.actualizeyourdream.blogspot.com