Anayetakiwa Kutafutwa Sana Kila Kona Kwa Dunia Ya Sasa Ni Nidhamu.

Habari za leo ndugu msomaji wa makala hii, ni matumaini yangu unaendelea kupambana kwa hali yeyote ile, ili kufikia kiwango kile unachokihitaji kufika katika maisha yako, haijalishi unakutana na vikwazo vya aina gani kwa kuwa umeamua hilo halitaweza kukukwamisha wewe usifike pale unapopataka kufika.
Pamoja na juhudi zote hizo, upo uwezekano mkubwa kuna eneo/sehemu unakosea ndio maana huoni matokeo mazuri ya kukufikisha pale unapotaka, kama ni biashara huoni wateja wakiongezeka zaidi unaona wale waliokuja leo hawaji/hawarudi tena vivyohivyo siku zinavyozidi kwenda mbele unapokea wageni kwenye kile unachokitoa lakini hawarudi mara ya pili au tatu baada ya kuwahudumia.

JE UPO TAYARI KUFANYA KILE AMBACHO NI SAHIHI HATA KAMA UNAUMIA?

 
Pengine upo kazini kwa miaka mingi sasa, unafanya kazi kwa bidii na maarifa yote, umejitahidi kujiongezea zile sifa zinazohitajika wewe kuwa nazo ili upande daraja lakini hayo yote hayajakupa matokeo mazuri, wenzako wanakuja leo unashangaa mwaka unaofuata amepandishwa daraja zaidi yako wewe mpaka wakati mwingine wanakuongoza hadi wewe. Umefika sehemu umeanza kujiona labda kuna mkono wa mtu, wengine wameanza kukuambia una laana kwenye ukoo wenu ndio maana husogei daraja, na wewe ukianza kuangalia historia ya familia yenu unaona ni kweli hakuna aliyewahi kuwa hata balozi wa nyumba kumi.
SOMA; Sababu Tatu(3) Zinazokuzui Kufanikiwa Kwenye Kazi Unayofanya.
Umefanya kazi miaka mingi sana ukiwa umeajiriwa na ile miaka 30 uliyokuwa unaiona ni mingi sana ya kustaafu zaidi uliona unao muda mwingi wa kutosha kufanya vitu, leo miaka kumi/ishirini imekatika majukumu ya familia yanakuandama, kama umeolewa/kuoa familia yenu inawatazama ninyi, watoto wako shule wanahitaji ada, mavazi pia, hujaja kwa wazazi wenu nako wanawatazama ninyi. Ukiangalia hayo yote unaona/unajiona huna kitu kabisa, ‘salary’ imechafuka kwa mikopo ya bank/taasisi za watu binafsi… umebaki na faraja kuwa kuna kiinua mgongo kipo kitakusaidia kumaliza ule ujenzi uliouanza miaka mitano iliyopita, umebaki kuwaza nikistaafu nitaanzisha biashara fulani, ama ukistaafu unawaza kuwa mheshimiwa kwa tiketi ya chama fulani ambacho utagombea ikiwa lengo lako kubwa ni kuendelea kupata pesa.
Unaweza kuona ni kiasi gani wale walioajiriwa kwa muda mrefu serikalini/makampuni/taasisi mpaka kufika umri wa uzee wao, kama hawakujitengeneza/kujipanga vizuri katika maisha yao ya baadaye kwenye eneo la uchumi wengi wao hupoteza maisha(uhai) kwa miaka michache sana baada ya kustaafu, wengine hata hiyo miaka mitatu hawamalizi baada ya kuacha kupokea mshahara, wengine hupoteza maisha baada tu ya kuambiwa mwezi fulani mwaka huu unastaafu kazi.
Unaweza usinielewe sana haya yote ninayosema hapa ila unaweza kuona ni presha tu za uzee zinawafanya wale uliowakuta kazini wakiwa wamebakisha miaka michache sana kustaafu, siku ikifika ya kuondoka kazini hali yake inakuwa mbaya zaidi na zaidi kadri siku zinavyozidi kwenda mbele.
SOMA; Sheria 6 Za Mafanikio Na Jinsi Zinavyoweza Kukuongoza Kufikia Mafanikio Makubwa.

Nataka kukuambia nini sasa kuhusu NIDHAMU baada ya utangulizi wa maneno mengi hapo juu?
Kila mtu anatamani kufikia/kuwa na maisha fulani mazuri sana ambayo anafikiri akiwa nayo maisha yake yatakuwa vizuri sana, hiyo mimi sikukatalii japo ninaweza kukuambia furaha hailetwi tu na mali nyingi bali tu mali ni sehemu ya kukusaidia kupata mahitaji yako muhimu ya huu mwili.
Kilichowakwamisha wengi kwenye maeneo yao ya biashara ni kukosa nidhamu, nidhamu imewafanya wengi kuhudumia wateja jinsi wanavyojisikia wao, nidhamu imewafanya wengi kushindwa kukua kibiashara maana ndani mwao hakuna kitu nidhamu.
Wafanyakazi wengi ni wafanyaji kazi kwa bidii ila kitu nidhamu haimo ndani mwao mpaka wengine imewapelekea kufukuzwa kazi wakiwaacha wale walionekana uwezo wao sio mkubwa sana katika utendaji kazi ila wana nidhamu ya hali ya juu ya kutaka kujifunza zaidi ili wawe bora.

Kukosa Nidhamu imewafanya wengi washindwe kujiwekea Akiba na kutumia kile wanachokipata pasipo uangalifu, wengi wameishia kununua nguo, wengi wameishia kula vyakula vya anasa(chipsi kuku), wengine kuweka heshima kwa kutoa ofa za vinywaji/vyakula pindi tu anapopokea mshahara wake, wengine hawataki kuonekana wapo nyuma akiona mwenzake amenunua gari na yeye anataka anunue, ukimuuliza hiyo pesa ya kununua gari la kutembelea kuna sehemu umezalisha au umekopa na hiyo pesa ya kuweka mafuta utaipata wapi majibu yote ni ndani ya mshahara, huko ni kukosa nidhamu ya kujiendesha.
Kwanini nidhamu? nidhamu inakufanya umhudumie vizuri kila mteja bila kujali uwezo wake kipesa, nidhamu inakufanya usile vyakula visivyo na faida kwako zaidi vina madhara kwako japo vinaonekana ni vitamu na vinapendwa na wengi, nidhamu itakufanya umheshimu mkubwa kwa mdogo, nidhamu itakufanya ujifunze kwa kila mtu, nidhamu itakufanya kuwa msikivu pale inapotokea mtu kutaka kukuelimisha/kukushauri kuhusu jambo fulani la kuokoa biashara/kazi yako.
SOMA; Tafakari Kuhusu Viungo Hivi Vitano (5) ili Uweze Kupata Wateja wa Bidhaa na Huduma zako Kila Siku.
Nidhamu yako itakufanya kuishi popote pale na watu vizuri, itakufanya usiwe na tamaa za kimwili, itakufanya kuwajali wengine, itakufanya kuhudumia vizuri, itakufanya upendwe zaidi na wale watakaobahatika kupewa huduma na wewe katika eneo lako la kazi/biashara, itakufanya kulea familia yako vizuri pasipo kutumia nguvu nyingi.
Utafanya nini sasa kuondokana na hili tatizo? Hujachelewa, wakati ni sasa endelea kutembelea mtandao huu wa AMKA MTANZANIA, utajifunza mambo mengi sana mapya ya kukusaidia zaidi na zaidi, kama utaona unahitaji msaada wa karibu sana wasiliana na ndugu Amani Makirita kwa namba
0717396253, ama na mwandishi wa makala hii; samsonaron0@gmail.com
Makala hii imeandikwa na Samson Ernest ambapo anapatikana facebook kwa jina hilohilo, pia waweza LIKE page yake ya Mtazamo Wa Maisha, pia waweza wasiliana naye kwa njia ya kupiga simu ama kutuma sms kwa njia ya kawaida/whatsApp 0759808081.
Asante sana, karibu.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: