Hii Hapa Ni Njia Bora Ya Wewe Kuweza Kufikia Malengo Na Mipango Yako Mikubwa Kwenye Maisha Yako.

Habari za wakati huu mpenzi msomaji wa AMKA MTANZANIA? Tuna imani kwamba uko vyema na unaendelea vizuri kuweka ubora kwenye kila unachofanya maishani mwako. Hili ni jambo muhimu sana kwani ndio litafanya maisha yako yawe bora na wewe uweze kuyafurahia.
Katika maisha yetu, kuweka malengo na mipango ni hatua moja muhimu sana ya wewe kuanza safari ya kuboresha maisha yako. lakini kuweka tu malengo na mipango sio jawabu la maisha bora kwako. Ingekuwa hivi kila mtu unayekutana naye angekuwa na maisha bora sana. Hii ni kwa sababu kila mtu ana mipango mizuri sana na maisha yake.
Eneo muhimu sana litakalobadili maisha yako ni kuweza kufanyia kazi malengo na mipango yako. kuweza kukomaa nayo hata pale unapokutana na changamoto, na kwa hakika ni lazima utakutana na changamoto.

 
Wengi hawafiki mbali.
Kwa mfano tuanze na mwanzo wowote wa mwaka. Watu wengi hufurahia mwaka mpya, huweka malengo ya mwaka huo na kuwa na mategemeo makubwa sana. Lakini kadiri siku zinavyokwenda ile hamasa inaanza kupungua na baada ya muda wengi wanakuwa wameachana kabisa na yale malengo na mipango yao. Inapofika tena mwisho wa mwaka na mwanzo wa mwaka unaofuatia zoezi hili linaanza tena.
Watu wengi wamekuwa wakirudia hivi miaka nenda miaka rudi, je na wewe ni mmoja wao? Je leo ukipata njia ya uhakika ya kukuwezesha wewe kufanyia kazi malengo na mipango yako utaifanyia kazi? Kama ndiyo basi endelea kusoma.
Kushindwa ni kukubwa kuliko kushinda.
Watu wengi hivi kuishia njiani licha ya kujiwekea malengo na mipango mizuri haitokei tu kwa sababu imetokea, kuna sababu kubwa sana ambazo zipo nyuma ya hili. Sitaki kukukatisha tamaa lakini ninachoweza kukuambia ni kwamba kwa jambo lolote unalofanya au unalotaka kufanya, uwezekano wa kushindwa au kukata tamaa ni mkubwa kuliko ule wa kushinda.
Kushindwa ni kukubwa kwa sababu kila jambo kubwa ambalo unakwenda kufanya linakuwa na changamoto zake ambazo hujawahi kuzijua hapo kabla. Na hivyo unapokutana nazo ni rahisi sana kuamua kuacha kuendelea.
Sababu nyingine inayopelekea kushindwa iwe rahisi ni wale wanaokuzunguka, unaweza kukazana na kuzivuka changamoto, ila sasa ukakutana na nguvu ya kupinga kutoka kwa wale watu ambao wanakuzunguka. Watu ambao ni wa karibu kwako na wanakujua vizuri. Watu hawa wanakuletea habari za kukukatisha tamaa kwamba utashindwa, au huwezi au unachofanya hakitafanikiwa. Na wakati mwingine watakuletea mpaka na mifano ya watu ambao walijaribu kama wewe na wakashindwa.
Kwa vikwazo hivi ni rahisi sana kuamua kuachana na kile ulichopanga na kuamua kurudia maisha yako ya kawaida.
Kuna mtu anaweza kukusaidia kuvuka vikwazo hivyo.
Kama huwa unafuatilia mchezo wowote, hasa mpira wa miguu utagundua kwa mfano, Ronaldo au Messi ni wachezaji wenye uwezo mkubwa sana. Lakini wachezaji hawa hawajiendei tu wenyewe jinsi wanavyotaka, japo wanaweza kujiwekea mipango yao wao wenyewe. Bali wachezaji hawa bora sana wana makocha wao ambao wanawasimamia vyema kwenye malengo na mipango yao ya kutaka kuwa wachezaji bora zaidi.
Mchezo wowote kuna mtu ambaye ni kocha, mtu huyu anakuwa na jukumu la kuifundisha na kuiongoza timu ili iweze kufanya vizuri na kufikia malengo ambayo kila mmoja amejiwekea.
Kocha hataingia uwanjani kucheza, lakini kocha anazijua mbinu bora sana ambazo kama wachezaji wake watazitumia basi wataweza kushinda mashindani wanayoshiriki. Kocha anao uwezo wa kuona changamoto na suluhisho la changamoto hizo zaidi ya mchezaji ambaye yuko uwanjani anacheza.
Timu zote ambazo zimefanya vizuri, wachezaji wote ambao wamefanya vizuri ni kwa sababu wamekuwa na makocha wazuri.
Unahitaji kuwa na kocha.
Kwa hapa kwetu Tanzania, dhana kwamba mtu binafsi unaweza kuwa na kocha wa kukuongoza katika malengo na mipango yako ni kitu kigeni. Watu wengi wamezoea kocha ni kwenye mambo ya michezo tu. Lakini ukweli ni kwamba unahitaji kocha hata kama haupo kwenye michezo. Kwenye maisha yako, kwenye kazi zako au biashara zako, unahitaji kocha ambaye atakuongoza na kuweza kuzivuka changamoto ambazo zinaweza kuwa hatari kwako.
Kuwa na kocha kuna umuhimu mkubwa sana kwako;
Kocha anakusaidia wewe kuvuka changamoto ambazo huwezi peke yako. kwa mfano unapokuwa kwenye matatizo, ni vigumu sana wewe mwenyewe kupata suluhisho bora kwa sababu unakuwa umelichukulia tatizo lile moyoni, yaani unakuwa umelibeba kihisia. Lakini kocha wako hana hisia zozote juu ya tatizo lile, hivyo inakuwa rahisi kwake kuona njia ya wewe kutatua tatizo hilo. Na fikiri kama huwa unafuatilia michezo utakubaliana na mimi kwamba ukiwa nje unaweza kuona makosa mengi sana ambayo wachezaji waliopo uwanjani wanayafanya. Na unasema kama angefanya hivi mambo yangebadilika, sasa kocha wako anakuwa anakuona wewe kwa jicho hilo.
Kocha atakufanya uendelee na malengo na mipango yako hata pale mambo yanapokuwa magumu. Haijalishi unafanya nini, kuna wakati mambo yatakuwa magumu. Licha ya kuwa na malengo na mipango mizuri, kuna mahali ambapo utakwama. Sasa ikiwa malengo na mipango hii umejiwekea wewe mwenyewe ni rahisi kuachana nayo na kwenda kwenye jambo jingine, lakini kama kuna kocha ambaye anakufuatilia hatakuruhusu uache kirahisi hivyo na hata wewe mwenyewe utajisikia vibaya kuacha kitu ambacho uliahidi kukifanyia kazi mpaka kifike mwisho. Kocha ni muhimu sana kwenye jambo lolote unalofanya kwenye maisha yako.
Kocha atakupa mbinu bora kabisa za wewe kufikia malengo na mipango yako na pia atakupa hamasa kubwa ya wewe kuendelea kuweka juhudi. Pia atakupa moyo pale ambapo maneno ya wengine yanaanza kuwa kikwazo kwako na kukufanya ufikirie kukata tamaa. Kwa kuwa na kocha ambaye anaelewa vizuri kile unachofanya, unakuwa kwenye nafasi kubwa sana ya kuweza kufikia kile unachotaka.
Je upo tayari kuwa na kocha?
Jibu ni NDIO au HAPANA.
Kama jibu ni hapana kila la kheri katika kuendelea kujaribu na kuacha. Maisha ni yako na maamuzi ni yako.
Kama jibu ni ndio karibu sana. Kwanza hongera kwa kuwa makini na maisha yako na kuamua kuchukua hatua.
Pili karibu sana mimi niwe kocha wako na nakukaribisha kwenye programu mpya ua ukocha.
Kwa kawaida gharama za mimi kuwa kocha wako moja kwa moja huwa zipo juu kidogo, na hili limekuwa linawazuia wengi kupata huduma hii nzuri sana kwao.
Kwa sasa kuna PROGRAMU MPYA YA UKOCHA ambapo nitafanya kazi na watu wachache ambao kweli wamejitoa kwa kile wanachotaka kufanya na watakuwa tayari kufanyia kazi malengo na mipango yao bila kuishia njiani. Pia watu hao ni lazima wawe tayari kufundishika na kufanyia kazi yale ambayo wanashauriwa.
Kutokana na ufinyu wa muda, nitaweza kufanya kazi na watu wachache tu kwenye programu hii.
Katika programu hii tutakuwa tunakutana au kuwasiliana angalau mara mbili kila mwezi kujua unaendeleaje, changamoto unazokutana nazo ni zipi na jinsi gani ya kuzifanyia kazi. Gharama za programu hii ni ndogo sana na kama kweli umejitoa kupata kile unachotaka basi hazitakushinda.
JINSI YA KUINGIA KWENYE PROGRAM HII;
Andika email yenye maelezo yako, ni kitu gani unafanya au unataka kufanya ambacho unahitaji mwongozo wa kocha. Andika changamoto ambazo unakutana nazo au zinazokuzuia.
Pia weka mawasiliano yako ya simu na eneo ulilopo na pia andika utapendelea kukutana au mawasiliano ya simu.
Email hiyo itume kwenda kwenye email amakirita@gmail.com
Baada ya kutuma email hii, kama maelezo yako yatakuwa mazuri na kama nafasi bado zipo basi tutawasiliana kwa maelekezo mengine zaidi. Jukumu lako kwa sasa ni kutoa maelezo mazuri yatakayompa mtu mwanga wa kujua unachotaka ni nini na kufanya hivyo haraka kabla nafasi hizi chache hazijaisha. Utaratibu unaotumika ni wa kwanza kuja ndio wa kwanza kupewa.
Karibu sana tufanye kazi pamoja, kwa pamoja tunaweza kuvuka changamoto nyingi zaidi ya ukiwa peke yako.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
AMKA CONSULTANTS.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: