Habari mpenzi msomaji wa AMKA MTANZANIA? Karibu katika makala yetu ya leo tuweze kujifunza tena mambo ambayo yanabadilisha maisha yetu kiujumla.
‘’Mimi ni mwamini mkubwa kwamba kama ukitafuta furaha,mafanikio yatafuata’’ maneno haya nimenukuu kutoka kwa bilionea Richard Branson ambaye niliyasoma katika moja ya makala zake kupitia tovuti yake ‘’ I’m a big believer that if you find happiness, then success will follow’’ ni kweli kabisa furaha huwa ina leta mafanikio katika maisha yako.
Furaha hufungua milango ya fursa kubwa, ukiwa na furaha maisha yako yatakuwa mazuri kila siku. Furaha hujenga uhusiano mzuri. Ni vema kuwa na furaha na maamuzi ya kuwa na furaha yako mikononi mwako acha maisha ya kuwa na kisirani, tabasamu, cheka nakadhalika.

 
Furaha ya kweli katika maisha itakupa hamasa kubwa ya kufanya kazi ili kufikia katika mafanikio makubwa. Makirita Amani aliandika hivi katika falsafa mpya ya maisha ‘’kila mmoja wetu anafanya anachofanya kutafuta furaha kwenye maisha. Juhudi zote tunazofanya kwenye maisha ni kwa ajili ya kupata furaha’’ kwa hiyo kila mtu anapigania kuwa na mafanikio ili kutafuta furaha ya kudumu na siyo furaha ya muda mfupi.
Chagua kuishi maisha ya falsafa yako ambayo yatakupa furaha ya kudumu katika maisha yako na ukiendelea kuishi maisha ambayo si yako, maisha ya kushindana basi ni dhahiri kabisa utakuwa unaikimbiza furaha. Njia nzuri ya kupata furaha kwanza kuwa na shukrani kwa kile ambacho unacho sasa na kwa kile ambacho unakipata hii itakusaidia kukupa hamasa ya maisha, itakuletea furaha na itakuongezea juhudi na maarifa ya kutafuta zaidi na utaziona fursa lakini kama hutoshukuru kwanza kwa kile ambacho unacho ni ngumu kupata furaha ya kudumu.
SOMA; Kama Unafikiri Vitu Hivi Ndivyo Vitakupa Furaha Ya Kweli Katika Maisha Yako, Unajidanganya Mwenyewe.
Dale Carnegie katika kitabu chake cha How to stop worrying and start living aliandika hivi ‘’ Think and Thank’’ yaani fikiri na na shukuru. Fikiri vyote ambavyo tunapaswa kutoa shukrani na mshukuru Mungu.
Zifuatazo ni kauli kumi zinazohusiana na furaha kutoka kwa watu mbalimbali;
10. ‘’Happines is not something ready made.it comes from your own actions’’ – Dalai Lama
Furaha siyo kitu ambacho tayari kimetengenezwa. huwa inakuja kutoka katika matendo yako mwenyewe’’
9.’’ Happiness is like a kiss. You must share it to enjoy it’’– Bernard Meltezer
Furaha ni kama busu. Lazima mgawane ili mfurahie
8. The greater part of our misery or unhappiness is determined not by our circumstance but by our disposition’’– Martha Washington
Sehemu kubwa ya kutokuwa na furaha kwetu inatambulika siyo kwa mazingira yetu bali kwa ubora halisi wa tabia ya mtu.
7. ‘’ Remember that the happiest people are not those getting more, but those giving more’’-H.Jackson Brown,jr
Kumbuka kwamba watu wenyewe furaha sana siyo wanaopata zaidi, bali wale wanaotoa zaidi.
6. ‘’Action may not always bring happiness; but there is no happiness without action’’ -Benjamini Disraeli
Matendo mara nyingi siyo lazima yalete furaha, lakini hakuna furaha bila matendo.
SOMA; Starehe za Muda Mfupi Zinakukosesha Furaha ya Muda Mrefu.
5. ‘’Happiness is not the absence of problems,it’s the ability to deal with them– Steve Maraboli
Furaha siyo hali ya kutokuwepo na matatizo, bali ni uwezo wa kukabiliana nayo
4. If you want happiness for an hour take a nap.
If you want happiness for a day –go fishing
If you want happiness for a year – inherit a fortune.
If you want happiness for a lifetime-help someone else
-chinese proverbs
Kama unahitaji furaha kwa saa moja pata usingizi wa muda mfupi.
Kama unataka furaha kwa siku moja, nenda kavue samaki.
Kama unataka furaha kwa mwaka mmoja, rithi mali.
Kama unahitaji furaha kwa maisha saidia watu wengine.
Hizi ni nukuu kutoka katika methali za kichina
3. Happy people are beautiful. They become like a mirror and they reflect that happiness’’- Drew Barrymore
Watu wenye furaha ni wazuri. wako kama kioo na wana akisi furaha hiyo.
2. ‘’everyone wants to live on top of the mountain, but all the happiness and growth occurs while you’re climbing it-Andy Rooney
Kila mmoja huwa anapenda kuishi juu ya kilele cha mlima, lakini furaha yote na kukua huwa inaonekana wakati ukipanda mlima.
SOMA; Mambo Sita(6) Muhimu Ya Kuzingatia Ili Kuwa Na Maisha Yenye Furaha Na Mafanikio Makubwa.
1. Happiness is not a goal…it’s by –product of a life well lived’’ – Eleanor Roosevelt
Furaha siyo malengo bali ni zao la kuishi maisha mazuri
Kwa hiyo mpenzi msomaji mpaka hapo umepata kujifunza umuhimu wa wewe kuwa na furaha hivyo basi chukua hatua leo furaha iwe sehemu ya maisha yako siku zote.
Makala hii imeandikwa na Deogratius Kessy ambaye ni mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali, unaweza kuwasiliana naye kupitia namba 0717101505 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com au unaweza kutembelea tovuti yake www.actualizeyourdream.blogspot.com