Mambo Matatu Yakuzingatia Katika Dakika Tano Za Kwanza, Kwenye Usaili.

Habari rafiki wa AMKA MTANZANIA, naamini umzima wa afya na unaendelea vyema na majukumu yako ya kuboresha maisha yako kama ilivyo kawaida. Kwa upande wangu niko vizuri, kwa furaha moyoni nakukaribisha tena kwenye siku nyingine bora kabisa kwa ajili ya kujifunza na kuboresha maisha yetu.
Leo katika makala yetu, tutaangalia mambo matatu yakuzingatia katika dakika tano zako za kwanza kwenye usaili.  Ikumbukwe kuwa wengi wetu  mara tunapomaliza masomo, jukumu la kwanza huwa ni kutafuta kazi. Kazi hizo mara nyingi upatikanaji wake hupatikana kupitia usaili. Sasa je, kama ni hivyo ni mambo gani unatakiwa uzingatie ili kufanikiwa kwenye usaili?
Yafutayo Ni Mambo Matatu Yakuzingatia Katika Dakika Tano Za Kwanza, Kwenye Usaili.
1. Mwonekano wako.
Ni lazima uwe na mwonekano mzuri ambao hautaleta maswali mengi kwa wale wanaokufanyia usaili. Jitahidi ukavaa nguo za heshima ambazo zitakuonyesha wewe ni nani. Acha kuvaa mavazi ya hovyo, ambayo yatakukosesha heshima na pengine hata kukukosesha kazi yenyewe unayoitafuta.
Mavazi unayovaa yana nguvu kubwa ya kukutambulisha wewe ni nani. Ikiwa mavazi yako ni ya kiustaarabu basi ni wazi utaonekana ni mstaarabu hivyo hivyo. Usije ukafanya kosa la kuvaa mavazi yaliyobana hasa kwa wanawake au mlegezo kwa wanaume hii, itakuwa ni kujivunjia heshima na itakuwa raisi kwako kupoteza hiyo kazi.
LAZIMA UJIAMINI KWANZA ILI KUJIHAKIKISHIA KAZI HIYO.
2. Kujiamini kwako.
Hakuna bosi au kampuni ambayo inategemea kumwajiri mtu ambaye hajiamini. Katika dakika tano zako za kwanza kwenye chumba cha usaili, unatakiwa kuzitumia vizuri kwa kujiamini kwa asilimia zote. Kwa jinsi utakavyokuwa unajiamini, ndivyo utavyozidi kumpa imani bosi wako mpya kuwa unajua mambo.
Lakini inapokuwa kinyume chake, yaani unaposhindwa kujiamini wewe mwenyewe inakuwa ni ngumu kuweza kufanikiwa kwenye usaili hata pia kwenye kwa jambo lolote lile. Kwa msingi huo hata unapokuwa kwenye chumba cha usaili usitishwe na kitu chochote kama uzuri wa ofisi au idadi ya watu waliokuzunguka, lililo kubwa kwako ni kujiamini ili uwe mshindi.
3. Taarifa zako.
Mwonekano wako unaweza ukawa mzuri, na hata kujiamini kwako kunaweza kukawa kwa hali ya juu lakini kama taarifa zako nyingi haziko sahihi, itakuwa sio rahisi kwako kuweza kufanikiwa kwenye usaili huo. Ukweli ni muhimu sana katika usaili wako. Kama ikatokea hujui jambo ni vyema ukaweka wazi kuliko ukadanganya halafu baadae ikaja kujulikana, utakuwa kwenye wakati mgumu. 
Kwa kuuzingatia mambo hayo matatu mwonekano, kujiamini na taarifa sahihi yatakusaidia sana kukuweka katika wakati mzuri wa kupata kazi unayoitafuta.
Tunakutakia kila la kheri katika maisha miasha yako, endelea kutembelea AMKA MTANZANIA na DIRA YA MAFANIKIO kwa kujifunza lakini zaidi jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kuboresha maisha yako.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Simu; 0713 048 035,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: