Itambue Na Kuitoa Thamani Kubwa Iliyopo Ndani Yako.

Habari mpenzi msomaji wa AMKA MTANZANIA? Karibu katika makala yetu ya leo tuweze kujifunza. Leo tutazungumzia kutoa hazina, thamani au kutoa /kuonyesha kile ambacho unacho au unajua katika dunia ya leo.
Kila binadamu ana kitu cha kipekee kuliko binadamu mwingine wowote hapa duniani. Kila binadamu ana nguvu kubwa ndani yake za kufanya kitu chochote ambacho anakipenda. Kila mtu anatakiwa kutoa kile alichonacho ili kuleta maendeleo chanya katika dunia ya leo. Ni watu wangapi wana vitu vizuri hawataki kuvitoa na kujaribu mwisho wa siku wanakufa navyo, kabla hujafa fanya kitu cha kuacha kumbukumbu au alama yako hapa duniani ambayo dunia itakukumbuka kwa yale mazuri uliofanya hapa duniani.

 
Kila mtu ana kitu cha kipekee ambacho akikitoa duniani itafaidia siyo tu dunia kufaidika bali pia yeye mwenyewe atalipwa kulingana na hiyo hazina ambacho anayo. Kama una hazina yoyote unayo tafadhali itoe usiendelee kukaa nayo siyo vizuri unajidhulumu mwenyewe na dunia pia.
SOMA; Kama Hutengenezi Hiki Mahali Ulipo Hustahili Kulipwa Chochote.
Kama una kipaji cha kuimba, kuchora, kucheza mpira, kuandika nk. Kitoe na kifanyie kazi kwa juhudi na maarifa acha kuongea tu una kipaji Fulani halafu bado unaendelea kukikalia kipaji chako badala ya kutoa hazina ambayo unayo ili ikusaidie katika maisha yako. Nina mfano mmoja wa rafiki yangu ambaye ni mshonaji nguo ana uwezo wa kushona nguo kila mtindo wa jinsia zote mbili yaani mwanamke na mwanaume lakini hatoi hazina yake ambayo anayo bali anakazana kutafuta kazi wakati ana kitu ambacho kinaweza kubadili maisha na kujiajiri kabisa. Ana shona sampuli za nguo nzuri lakini anaziacha chumbani( nyumbani) hataki kuonyesha dunia anafanya nini kama una kitu unafanya waonyeshe watu unafanya lakini siyo kukaa nacho chumbani, hii ni sawa na kukimbia mbio mwenyewe halafu unajihesabia mshindi.
Hakuna mtu mwingine anayeua hazina ambayo unayo zaidi ya wewe, amini katika kile unachoweza halafu kipende kifanyie kazi utapata matokeo mazuri sana. Usiogope kufeli/ kushindwa ndio kujifunza wala usiangalie kelele za dunia zikakukatisha tamaa wewe angalia unachofanya na ishi maisha yako.
SOMA; Una Nini Cha Tofauti Mpaka Watu Wakufuate Na Kukusikiliza? Jua Hapa.
Usikubali kufa na hazina ndani yako. Kwanini usikubali kufa na hazina ndani yako? Hii ni kwa sababu, WEWE ni Zawadi kwako mwenyewe na ni zawadi kwa dunia. Kama watu wengine wangekufa na hazina zao leo dunia ingekua wapi? Mimi naamini kila mtu akitoa kile ambacho anacho tutafika mbali.
Bado watu wengi hawaamini katika kile wanachoweza tafadhali ndugu thubutu kujiamini na onyesha kile unachoweza dunia itakupa nafasi. Una kila kitu cha wewe kuweza kufanikiwa kuna baadhi ya watu wanasema hawana elimu hivyo hawawezi kufanikiwa. Nani kasema huna elimu? Mungu amempa kila mtu kipaji, amempa kitu muhimu ambacho ni hazina kubwa kwake na kwa dunia.
Amini unaweza katika yeye akutiaye nguvu kuwa imara, kuwa na uwezo wa kukabiliana na magumu ( be strong and be courageous). Kuwa na imani chanya juu ya wewe, usijifananishe na mtu mwingine jiamini una kitu cha kipekee kuliko mtu mwingine.
Ukipata fursa ya kuishi hapa duniani basi usife na kipaji chako, usiogope kujaribu changamoto ni kitu ambacho kitakufanya wewe uwe imara, na hakuna maisha bila changamoto.
SOMA; Kama Unavipa Thamini Sana Vitu Hivi,… Lazima Maisha Yako Yawe Magumu.
Mwisho, Maisha ni muda na wakati ambao ni muhimu sana kwako ni sasa na siku ambayo ni muhimu sana kwako ni leo. ‘’Kuna wakati wa Mungu ( Kairos) uko juu ya wakati wa wanadamu (Chronos). Wakati wa Mungu unapotimia au kuwadia mwanadamu hawezi kutenda lolote katika wakati wake (Chronos)’’ (Mch. Mkilindi 2014). Hivyo basi usipotumia vema wakati ukiendelea kusubiri wakati mwingine ndio ufanye utakua unajidanganya.
Makala hii imeandikwa na Deogratius Kessy ambaye ni mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali, unaweza kuwasiliana naye kupitia namba 0717101505 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com au unaweza kutembelea tovuti yake www.actualizeyourdream.blogspot.com

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: