Karibu Kwenye Familia Kubwa Ya Wanamafanikio Tanzania.

Habari rafiki?
Naamini unaendelea vyema na mipango yako ya maisha.
Napenda kuchukua nafasi hii kutoa taarifa muhimu kwa wanachama wa KISIMA CHA MAARIFA na wale ambao pia wangependa kuwa wanachama.
Kwanza kabisa niwapongeze wale wote ambao tumekuwa pamoja kwenye KISIMA CHA MAARIFA, kuna mengi sana ambayo mmekuwa mnaendelea kujifunza na kuyafanyia kazi.
Napenda KISIMA CHA MAARIFA iwe familia moja ya wana mafanikio wote, wale wote ambao wamejitoa kufikia mafanikio makubwa na wapo tayari kutoa mchango mkubwa kwa wale wanaowazunguka.
Na kwa kuwa safari hii sio rahisi, kuifanya peke yako ni sawa na kucheza mpira kwenye uwanja ambao ni mlima, halafu wewe unatakiwa kupanda mlima ndio ukafunge goli, wakati unayecheza naye yupo kwenye mteremko.
Hivyo kila siku nimekuwa nikifikiri njia za kukifanya KISIMA CHA MAARIFA kuwa bora zaidi, nimekuwa nikiangalia yale yaliyopo sasa na yanayoweza kufanyika kupitia KISIMA CHA MAARIFA.
Kwa njia hii nimekuwa naona njia nyingi za kuboresha na ili kuboresha mabadiliko yanahitajika. Hivyo utaona nakuja na mabadiliko mengi sana ndani ya muda mfupi, ni katika hali ya kutaka KISIMA CHA MAARIFA kiwe bora zaidi.
Na katika kuzioana njia hizi za kuboresha KISIMA CHA MAARIFA nimekuwa nakuja na mabadiliko mengi madogo na makubwa. Yale madogo unakuwa unayaona mwenyewe na yale makubwa nakuwa nakupa taarifa mapema ili uwe tayari kuyapokea.
Nafanya mabadiliko haya ili kuboresha huduma unayoipata wewe rafiki yangu, ili nione wewe ukibadilika, maisha yako yakiwa bora na ukifikia mafanikio makubwa. Kumbuka usipofanikiwa wewe mimi siwezi kufanikiwa na hivyo jukumu langu la msingi kabisa ni wewe kufanikiwa.
Katika kuhakikisha hili nimekuja na mabadiliko kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Kama utakumbuka kisima kilianza kwa udogo sana na watu wachache, baadae marafiki mkaongeza imani na kuendelea kujiunga mpaka sasa ambapo tupo zaidi ya wanachama 150 waliolipia ada na kuwa wanachama.
Na pia tulianza na uanachama wa aina moja na ada moja kwa wote, baadae tukaja uanachama wa aina tatu ili kuwawezesha wale ambao hawawezi kulipia gharama kubwa tuwe nao pamoja, baadae tukafuta uanachama wa aina moja na zikabaki aina mbili.
Mabadiliko yote haya ni katika kuangalia ni njia ipi bora ambayo watu watanufaika nayo.
Na sasa mabadiliko yanayokuja ni kuwa na uanachama wa aina moja, na wote tutabaki kuwa KISIMA CHA MAARIFA GOLD MEMBERS.
Kwa nini uanachama wa aina moja?
1. Tangu mwaka huu umeanza, wengi wanaojiunga na KISIMA CHA MAARIFA wamekuwa wakichagua uanachama huu wa juu yaani GOLD MEMBER na hii imenipa picha kwamba watu wanataka kilicho bora, hakuna anayetaka cha pili, na hivyo sisi wote ni wa kwanza.
2. Sisi ni wanamfanikio na wanamafanikio wote wanakwenda na kile kilicho bora, wanachukua namba moja na sio namba mbili.
3. Nataka kuhakikisha unajifunza na kuchukua hatua zaidi. Kwa jinsi ninavyoangalia takwimu za usomaji, na naziangalia kweli, najua nani kasoma na nani hajasoma, nani kaingia na nani hajaingia. Nimegundua ya kwamba wale ambao wapo uanachama wa chini, ukiacha gold, usomaji wao wa makala ni mdogo sana.
4. Nataka wote tuwe kwenye kundi la wasap, ambalo nitaendelea kuweka nguvu kubwa kuhakikisha kila mtu anapata thamani kubwa sana, tushirikishane wote kwa pamoja.
5. Nataka kufanya kazi na watu wachache waliojitoa kweli badala ya wengi ambao wamejitoa nusu nusu. Ni bora kwenda kwenye vita na watu watano waliojitoa kupigana kuliko kwenda na watu mia moja ambao hawajajitoa kweli. Hivyo kwa uanachama huu wa aina moja, nafasi zitakuwa chache na hivyo watazipata wale ambao kweli wamejitoa kuyafikia mafanikio.
Changamoto za uanachama huu mmoja.
Kwa kuwa kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA GOLD MEMBER pia unapata nafasi ya kuwa kwenye kundi la wasap, na kwa kuwa kundi la wasap lina uwezo w akuchukua watu 100 pekee, basi hizi ndio zitakuwa nafasi za kuwepo kwenye kisima cha maarifa.
Changamoto kubwa ni kwamba wanachama wote waliopo sasa, ambao walikuwa pia kwenye uanachama wa chini, wote wanakwenda kuwa GOLD MEMBER, hivyo kw akuwa wameshazidi 100 , hivyo nafasi zinazidi kuwa changamoto.
Hivyo kama unapenda kuwa sehemu ya familia hii ya mafanikio, basi unahitaji kuchukua hatua haraka ya kujiunga.
Malipo ya ada kwa wale ambao bado.
Wale wote ambao walijiunga na KISIMA CHA MAARIFA kabla ya mwaka 2015 unatakiwa uwe umeshalipa ada yako ili uendelee kuwepo kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Kama bado hujakamilisha malipo fanya hivyo mapema kabla ya mwezi huu kuisha.
Kujiunga na KISIMA.
Kama bado hujajiunga na KISIMA CHA MAARIFA, basi fanya hivyo mapema hii. Kuna mambo mengi mazuri unayakosa ambayo yanaendelea kwenye KISIMA CHA MAARIFA, hasa kwenye kundi la wasap.
Taratibu za kujiunga na kulipia ada.
Kwa wale ambao tayari ni wanachama na bado hawajalipia ada ya uanachama wao tafadhali fanya malipo. Tuma ada ya mwaka tsh elfu 50(50,000/=) kwenye namba 0717396253 au 0755953887 na utume ujumbe wenye email na majina uliyojiunga nayo.
Kwa wale wanaotaka kujiunga tuma ada kama ilivyoelekezwa hapo juu kisha utatumiwa taratibu nyingine.
Nakukaribisha kwenye KISIMA CHA MAARIFA, hii ni familia kubwa ya wapenda na wasaka mafanikio. Je usingependa kuwa sehemu ya familia hii? Maisha ni yako na uchaguzi ni wako. Lakini mimi kama rafiki yako nakuambia chagua kuwa sehemu ya familia ya KISIMA CHA MAARIFA, hutajutia hilo.
Nakutakia kila la kheri katika safari hii ya mafanikio uliyoishagua,
TUPO PAMOJA,
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: