Una Uwezo Mkubwa Sana Ndani Yako, Usikubali Kurudishwa Nyuma Na Watu Hawa.

Habari za jumapili mpenzi msomaji wa Amka Mtanzania. Ni matumaini yangu kuwa wote mnaendelea vyema katika utekelezaji wa majukumu yetu ya kila siku. Ninamshukuru Mungu kwa ajili ya nafasi hii tena aliyotupatia ili kuzidi kukumbushana mambo mbalimbali.

 
Ndugu yangu leo naomba kusema na mtu yule ambaye amekuwa akifanya kazi kwa bidii sana lakini imekuwa kinyume kwamba hakuna mtu anayeona kile anafanya au amekuwa akitafsiriwa vibaya na wale waliompa majukumu hayo. Inawezekana kabisa kuwa hakuna anayekuelewa unapong’ang’ana kufanya kazi yako hiyo, lakini wewe pekee ndiye unajua kwa nini upo hapo, kwa nini unafanya hicho unafanya, ni wewe peke yako unajua kule unaelekea , pengine ni hiyo biashara yako au hiyo shughuli yako nyingine uliyoianzisha hakuna mtu anayekuelewa kabisa, hata wale uliofikiri kwamba ni wa karibu sana na wewe, ulifikiri wanakuelewa na kuelewa kile unafanya lakini imekuwa kinyume sasa kwamba kwa kuwa wanakufahamu vyema basi wanakazana kujipambanua na kukuonyesha ni namna gani utashindwa katika hilo.
SOMA; TOFAUTI YAKO WEWE NA MBUZI NI HII HAPA
Watu wengi wameshindwa kuishi ndoto zao au kutimiza malengo yao kwa kuwa tu kuna watu wanawapinga, kwakuwa tu walipoanza kuchukua hatua walisikia sauti nyingi za watu wanaowaambia kuwa hawawezi, watashindwa, watapata hasara na mengineyo mengi. Ndugu yangu kama umekuwa ukifuatilia mfululizo wa makala hizi basi naamini yapo mengi ambayo utakuwa umejifunza na hata namna ya kukabiliana na changamoto kama hizi, kwa yule ambaye ndio anasoma mahala hapa leo, naomba nimwambie kuwa wewe ndiwe mwenye uamuzi wa kuamua ufike kule unaenda au la, wewe ndio unao uamuzi wa kuamua kusikiliza kelele za kila mbwa anayebweka, ndugu katika safari ya maisha haya, pale unapojaribu kufanya kile umeumbwa uje ufanye uwe na uhakika kuwa ni wengi watakupinga tena unaofikiri watakuunga mkono, lakini ndugu yangu kupingwa na hao haimaanishi kwamba hauwezi, hao hawana hatima ya maisha yako, wanachoona au kusema wao juu yako siyo NDIYO maishani mwako, wasikilize ndiyo lakini ikiwa unajielewa wewe ni nani , kwa nini ulizaliwa basi naamini itakuwa rahisi kwako kupuuzia zile kelele zinazotaka kukuchelewesha kuelekea kule unaenda, kwa kuwa utatambua kuwa una uwezo mkubwa sana ndani mwako na ni kwa huo unapata ujasiri wa kuweza kufanya mambo makubwa sana maishani ambayo pengine hakuna mtu mwingine anaamini kuwa unaweza kuyafanya kwa ufanisi.
Ni kweli kwamba yawezekana umejaribu na kushindwa mara kadhaa au hata kwenye familia yako hakuna ambaye amewahi kufanya jambo hilo akafanikiwa, hivyo jamii inatumia hiyo kama sababu ya kukuonyesha kuwa huwezi fikia pale unatamani kufika, ndugu yangu huenda ni kweli wasemayo lakini kujaribu kwako na kushindwa hakukuachi bila shule, yapo mengi unajifunza hata katika kushindwa hivyo ukirudia kufanya kitu kile kile lazima utakitenda kwa ufanisi zaidi maana unaelewa kwa nini ulianguka mwanzoni. Kutokuwa na mtu aliyefanikiwa katika jambo hilo unafanya kwenye familia yako siyo maana kwamba wewe hauwezi au hakuna mwingine kwenye familia anaweza fanya jambo hilo vyema , Mungu ametuumba kila mtu kwa tofauti na kwa kusudi maalumu, unajuaje kwamba pengine ulizaliwa ili kuja tu kufuta hiyo rekodi mbaya kwenye familia yenu kuwa labda hakuna ambaye amewahi kusoma mpaka akafikia kidato cha nne.
SOMA; Kuwa Dereva wa Maisha Yako
Inuka ndugu, fanya kile unajua ndicho unatakiwa ufanye duniani hapa, usimuogope yeyote maana mwenye kutoa ujuzi , maarifa na kila jema ni Mungu pekee. Upo kwa ajili ya kuvunja rekodi, kufanya vile kila mtu anajua hauwezi, wewe si wa kawaida ndugu usitende kikawaida, usijifananishe na wengine, wewe ni wewe hakuna aliye kama wewe. Usiache kufanya kazi kwa bidii kwa kuwa hakuna anayekukubali, kumbuka unapofanya kazi kwa bidii na ikafanikiwa unajisikia vizuri wewe mwenyewe pia, hivyo usitegemee msukumo wa nje chanya ili uweze endelea kufanya kazi zako kwa bidii, hata ukipingwa ili mradi unajua kile unafanya, ng’ang’ana ndugu watakuelewa tu wakati wao wa kuelewa ukifika.
Makala imeandikwa na Beatrice Mwaijengo
+255755350772

One thought on “Una Uwezo Mkubwa Sana Ndani Yako, Usikubali Kurudishwa Nyuma Na Watu Hawa.

Add yours

  1. Kaka jaribu kutumia Kiswahili sanifu. Kumbuka makala zako zinasomwa na watu wa Elimu tofauti hivyo zingatia matumizi sahihi Kiswahili. Mfano:”Usikatishwe tamaa na watu” halafu wewe ukasema “Usijekatishwa tamaa na watu” Asante.

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: