Mafanikio Na Utajiri Unaotafuta, Yanategemea Sana Kitu Hiki.

Habari mpenzi msomaji wa AMKA MTANZANIA. Ni matarajio yetu ya kwamba umeianza siku hii ya leo vizuri na upo hapa tayari kwa ajili ya kujifunza mambo muhimu ya kuweza kubadilisha maisha yako na kuwa mtu wa tofauti.
Leo hii katika makala yetu ningependa nianze kutoa ushauri hasa kwa wale wanaolalamika sana kila siku na kila wakati kwamba maisha ni magumu. Najua watu hawa unawajua vizuri na wamekuwa ni watu wa kulalalamika sana karibu kila siku.
Kama na wewe ni mmoja wa watu hawa ningependa kukwambia ili utoke hapo unatakiwa kufanya jambo moja tu, ambalo ni  kufanya kazi kwa bidii zote kana kwamba hutakufa. Fanya kazi na weka juhudi zako zote hapo. Kwa kufanya hivi itakuwa kwako njia bora kabisa ya kukufanikisha.
Kama unatembeza bidhaa zako, usijihurumie mwenyewe, pita kila mahali, nenda kila ofisi uwezavyo kuingia, fanya kama kichaa asivyojihurumia. Usinielewe vibaya. Wakati unafanya yote hayo kumbuka kutunza afya yako pia. Hiyo kwani ndiyo itakayokusaidia kuyafikia mafanikio yako.
WEKA JUHUDI, PESA UTAZIPATA TU.
Ninachotaka kusema hapa ni kwamba fanya kazi kwa juhudi zote. Acha kutafuta visingio vitakavyokuletea uvivu. Jitume huku ukijua kabisa kwamba kazi ndio mkombozi wa maisha yako yote. Bila kufanya hivyo huna maisha ya kusonga mbele.
Haijalishi una malengo mazuri kiasi gani, haijalishi wewe ni mbunifu kiasi gani, haijalishi wewe una vipawa kiasi gani lakini kama tu haujitumi na unategemea muujiza wa kufanikiwa hilo halitaweza kutokea kamwe kwenye maisha yako hata siku moja.
Kanuni hii ni muhimu sana kuitambua. Hakuna ambaye ameifanyia kazi kiukamilifu ikamuangusha. Kwa wote wenye bidii ukiongeza na ubunifu mafanikio makubwa huwa yapo upande wao. Kwa anayetumia kanuni hii, hakuna mashaka ya kutajirika. Hakuna mashaka ya kuwa maskini tena.
Waangalie wale watu wote walioweka bidii na juhudi katika mambo yao nyakati zote nini kiliwatokea? Bila shaka ni mafanikio makubwa. Huo ndio ukweli ambao hauwezi kupingwa. Unaweza ukaangalia historia au vitabu vya kuhamasisha vyote vimeongelea jambo hilohilo.
Hivyo, utaona wale wote wenye bidii huwa ni watu wasiochoka , wasiotulia, wala kuwa na utulivu mkubwa nafsini mwao mpaka wamepata kile walichokuwa wakikihitaji katika maisha yao. Kitu gani kinakuwa kimewasaidia ni bidii yao.
Ili na wewe uweze kufanikiwa kwa kila jambo, hii ni kanuni mojawapo bora ya mafanikio ambayo hutakiwi kuitupa nyakati zote. Hakikisha huridhiki wala hutulii mpaka ufanikiwe unalolitafuta. Fanya kana kwamba ni nafasi pekee ya kulifanya hilo unalolifanya na haitatokea tena.
Natamani uwe na kiu kubwa sana ya mafanikio ii ikusaidie kuwa na bidii ya ajabu sana katika utendaji wako. Ukishaweka ubunifu katika unalolitenda, weka bidii zote mpaka uone limefanikiwa na hakika litafanikiwa hakuna wa kuweza kulizuia hilo.
Hivi ndivyo kanuni hii inavyofanya kazi na ni kama vile injini ya kanuni zingine. Bila kanuni hii zingine zote zaweza kushindwa. Unaweza ukawa una kipaji, mbunifu na una malengo mazuri, yote haya yanaweza kuwa bure usipoweka juhudi. Kumbuka, mafanikio yako na utajiri wako unategemea sana bidii yako katika utendaji wako.
Ansante kwa kutembelea mtandao huu wa AMKA MTANZANIA kila wakati. Endelea kuwaalika wengine wajifunze kupitia makala tunazozitoa hapa.
Kwa makala nyingine za maisha na mafanikio usikose kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kwa kujifunza zaidi.

Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu;0713 048035,
  

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: