Hizi Ndizo Sababu Zinazopelekea Watu Kukata Tamaa Ya Maisha.

Habari mpenzi msomaji wa AMKA MTANZANIA? Natumaini unaendelea vizuri na karibu tujifunze tena. Katika makala yetu ya leo tutazungumzia kwa nini watu wanakata tamaa katika maisha na kushindwa kabisa kutimiza ndoto zao. Kukata tama ya maisha inapelekea watu hata kuona maisha hayana maana na hakuna sababu ya kuendelea kuishi na hatimaye kupelekea kujinyonga. Kukata tamaa kunaanzia katika mtazamo wa mtu ambao ni kujaza mtazamo hasi katika akili yake katika kila jambo analofanya na kujaza mambo moyoni na kusababisha mtu kuanza kudhoofika kiakili na hatimaye kimwili. 

Zifuatazo ni sababu zinazosababisha mtu kukata tamaa ya maisha na kushindwa kutimiza ndoto yake;
1. Kuishi katika hali ya mtazamo hasi;
Hakuna kitu kibaya kama kuwa na mtazamo hasi katika maisha yako. Mtazamo hasi ni sumu katika maisha yako ndio unasababisha wakati mwingine kukata tamaa. Kuna hali ya mtu kuwa na mambo mengi moyoni na kushindwa kuyatoa (introvert) inamsababishia mtu mambo mengi kumtawala katika akili na kusababisha kumchanganya kisaikolojia na hatimaye kuanza kudhoofika kiakili na hatimaye kimwili. Tuna shauriwa kutoweka mambo moyoni (extroverts) badala yake yatoe na washirikishe hata watu wengine ili wakusaidie katika tiba ya ushauri nasaha. Kuwa na mtazamo wa kuhisi kutengwa na ndugu, jamaa na marafiki nayo inachangia mtu kukata tamaa na kutotimiza ndoto ya maisha yake. Wakati jukumu la maisha yako ni wewe mwenye na hupaswi kukata tama ya maisha.
Kwa hiyo kuishi katika mtazamo hasi ni hatari , anza kuishi maisha ya mtazamo chanya wakati wote na usipendelee kukaa na mambo mengi moyoni bila ya kuyazungumza.
2. Kuishi maisha ya kuigiza;
Kuishi maisha ambayo siyo yako kwanza ni utumwa unaanza kulinganisha maisha yako na mtu mwingine, unaanza kujilinganisha na jirani yako yeye ana kitu fulani na wewe huna, unahesabu matatizo yako na kujilinganisha na mwingine mwisho unajikuta na kujiona maisha yako hayana maana na hali hii itakupelekea kukata tamaa ya maisha na kushindwa kutimiza ndoto ya maisha yako.
Kwa hiyo maisha ya kuigiza yanasababisha watu wengi kukata tamaa katika maisha yao kwa sababu ya kufanisha maisha yao na wengine. Ishi maisha yako na usijifananishe na mtu mwingine.
3. Kuzungukwa na watu hasi;
Kuzungukwa na watu wenye mtazamo hasi nayo ni changamoto inayosababisha watu wengi kukata tamaa ya maisha. Watu wenye mtazamo hasi kazi yao ni kukosoa utafikiri wako katika mashindano ya kukosoa, na katika kukosoa wanakosoa kwenye jambo zuri au baya ili afanikishe tu kukujaza fikra hasi kama alizokuwa nazo.
Ukiwa na mawazo mazuri usimshirikishe mtu wa namna hii, tafuta mtu chanya awe mshauri wako, pendelea kujifunza sana, soma vitabu, makala, hudhuria semina hakika utakua umezungukwa na watu wenye fikra chanya. Epuka kuzungukwa na watu wenye mtazamo hasi, na zungukwa na watu wenye mtazamo chanya itakuepusha na kufikiria kukata tamaa ya maisha. Haupaswi kukata tamaa kabisa kwani ni dhambi endelea kuweka juhudi na maarifa na pambana mpaka utakua mshindi.
4. Kukosa tumaini la maisha;
Hali ya mtu kukosa tumaini la maisha inamsababishia kukata tamaa kutokana na kusemwa vibaya, kukosolewa, kukosa upendo, furaha, amani. Kukosa mahitaji ya msingi katika maisha humpelekea mtu kukata tamaa, matatizo ya kiuchumi, kifamilia, kimapenzi nakadhalika husababisha mtu kukata tamaa ya maisha kutokana na kukosa matumaini katika baadhi ya mambo fulani katika maisha yake kama tulivyoona hapo juu kwa uchache kidogo.
Kila mtu ana haki ya kufurahia maisha ni kubadili tu fikra na kuanza kuishi maisha ya furaha na matumaini na wala hauhitaji mtaji katika jambo hili. Wimbi la watu mtaani waliokata tama ni kubwa sana wengine wanaamua hata kujiingiza katika ulevi, uvutaji sigara, bangi, na utumiaji madawa ya kulevya mwisho wa siku wanajikuta wameshaathirika na madawa na kuwa watuma watumwa wa madawa na nguvu kazi imepotea hatimaye kujiingiza katika wizi wa mtaani.
5. Kuomba ruhusa badala ya samahani;
Siku ukitaka kufanya jambo la mapinduzi katika maisha yako huhitaji upate ruhusa bali fanya kwanza na uje uombe samahani baadaye. Wengi wanakata tamaa katika maisha kwa sababu ya kuomba ruhusa, na siku zote kuomba ruhusa lazima utakatishiwa tamaa na watu waliokuzunguka wakiwemo wazazi, ndugu, Jamaa na marafiki.
Sasa ili usikatishwe tamaa katika maisha unatakiwa kuwa muasi wa kufanya mapinduzi chanya katika maisha yako ambayo yataacha alama duniani. Ukiendelea kusubiri upewe ruhusa utakuwa unapoteza wakati. Umri unaenda na haurudi nyuma na maisha ni muda ukishindwa kutumia vizuri unakua unapotea, kutoomba ruhusa kuna kufanya uwe mbunifu, kufanya maamuzi magumu, kuokoa kipaji chako kisife au ndoto yako isife.
Kwa hiyo, hizi ni sababu chache kati ya nyingi zinazomfanya mtu kukata tamaa ya maisha na kushindwa kutimiza ndoto yako. Mwingine anaweza kuwa na mtazamo wa kupata mafanikio ya haraka katika maisha yake na mambo yakienda ndivyo sivyo humpelekea kukata tamaa, unapaswa kujua hakuna mafanikio ya haraka na mafanikio ni mchakato na siyo rahisi unahitaji kuwa mvumilivu katika kutafuta kwenye maisha yako bila kukata tamaa na kuendelea na kuwa na mtazamo chanya wa kufanikiwa. Hivyo basi, usikate tamaa kwa wewe bado uko hai una nafasi bado ya kuboresha maisha yako na kua bora sana.
Makala hii imeandikwa na Deogratius Kessy ambaye ni mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali, unaweza kuwasiliana naye kupitia namba 0717101505 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com au unaweza kutembelea tovuti yake www.actualizeyourdream.blogspot.com

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: