Kanuni Ya Uhakika Itakayokusaidia Kutimiza Ndoto Zako Zote.

Ndani ya kila mwanadamu anayo mambo ambayo anataka  kuyakamilisha na kuwa nayo kwenye maisha yake. Japokuwa mambo hayo hana lakini atatamani kufanya lolote lile ili aweze kuyatimiza hivyo basi inadhihirisha kwamba kila mwanadamu ameumbiwa kutamani mafanikio kwa asili.
Hata hivyo pamoja na kutamani mafanikio hayo, wengi bado wanasumbuka jinsi ya kuweka ndoto zao na kuwa za kweli kwenye maisha yao. Kwa kawaida zipo njia nyingi ambazo mwanadamu huyu anaweza kuzitumia kufikia ndoto zake. Lakini leo katika makala haya nataka kukupa njia moja ya uhakika itakayokusaidia kutimiza ndoto zako ambayo nayo ni kuishi kwa kufanya kile unachokipenda kila siku.
Naona unashangaa! Ndiyo, hakuna uchawi wa kuweza kuzifikia ndoto zako kwa uhakika zaidi ya wewe kuishi kwa kufanya kile unachokipenda. Kama unabisha, mimi sibishi kwa kubishana na wewe ila huo ndio ukweli unaopaswa kuutambua na kuufanyia kazi karibu kila siku. Chagua kile unachokipenda, fanya kile unachokipenda siku zote utakuwa na mafanikio makubwa sana.
Nasema tena ishi kwa kufuata ndoto zako. Ni vema kwa kile unachokitamani kuwa, kwani sisi sote ni matokeo ya kile tunachokiishi na kukifikiri. Ndugu yangu, unataka kuwa mfanyabiashara ishi vivyo hivyo kama mfanya biashara, unataka kuwa kuwa daktari ishi kama daktari kwa kuhudumia wagonjwa na wenye udhaifu kuanzia sasa.

FANYA KILE UNACHOKIPENDA
Sasa utakuta wewe unataka kuwa mfanyabiashara mzuri  halafu bado unatapatapa bila mwelekeo mara leo kuajiriwa mtaani,  mara kufanya kile na hiki ambacho hata hakiendani na kile unachokitaka kwenye maisha yako. Utakuta mwisho wa siku haufanikiwi kufikia malengo yako kwa sababu hueleweki na unavutwa na kila upande matokeo yako ndoto zako zinabaki zinaelea hewani bila kufikiwa.
Jifunze sana kutembea na wale wenye nia kama yako kimaisha. Siku zote haiwezekani kumwona tembo akitembea kila siku na kundi moja na simba. Haiwezekani tena hata kidogo. Wale ni wenye nia moja na malengo ya aina moja mtasaidiana sana kushirikiana kwa kile mnachokitaka na kufika mbali kabisa.
Ishi siku zote na wale watu ambao mnataka kwenda kufanya kitu kinafanana. Kuwa  na watu hao utajifunza, mtajadili njia mtakazo tumia hadi kufikia lengo lenu kuu. Kama unataka kufanya biashara ishi na watu ambao mkikaa na kujadili muone kweli mafanikio makubwa ya kibiashara ya kikatiza kwenye vichwa vyenu bila ubishi wowote.
Kuwa na msimamo na maisha yako. Hakikisha usiweze kuyumbishwa na kitu chochote kile. Haijalishi unapitia matatizo ya aina gani. Matatizo hayo yasiwe chanzo cha wewe kukuzuia kufikia mafanikio. Kitu kikubwa amua kufanikiwa bila kuweka sababu na siku zote tambua wewe ni nani, kipi unachokitaka na kukipenda kukifanya, kisha fanya kitu hicho kila siku.
Tambua sikuzote usibadilishe badilishe ndoto zako ili kupata mafanikio ila bailisha njia zako na kufuata njia nyingine hadi kuhakikisha unafika kule unakotaka kufika kwenye maisha yako. Kwa kufanya hivyo utaweza kufikia malengo yako kwa asilimia kubwa sana na hakuna atayekuzua katika hilo.
Tunakutakia kila la kheri katika safari yako ya kufikia mafanikio makubwa na endelea kutembelea AMKA MTANZANIA kwa kujifunza kila wakati.
Kwa makala nyingine nzuri za mafanikio usikose kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kwa ajili ya kuweza kubadilisha maisha yako.
Ni wako rafiki katika kuyasaka mafanikio ya kweli,
Imani Ngwangwalu,
Simu;0713 048035,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: