KITABU CHA APRIL; THE SEVEN HABITS OF HIGHLY EFFECTIVE PEOPLE (Tabia Saba Za Watu Wenye Ufanisi Wa Hali Ya Juu).

Habari rafiki na msomaji wa AMKA MTANZANIA?
Karibu tena kwenye utaratibu wetu huu mzuri wa kupeana kitabu cha kujisomea kwa mwezi. Tulianza utaratibu huu tangu mwaka 2013 na mpaka sasa ni vitabu vingi sana ambavyo vimeshatumwa kwa wasomaji kwa ajili ya kujisomea.
Kabla sijakushirikisha kitabu cha kujisomea kwa mwezi huu wa nne, nina habari njema sana kwa wasomaji wote wa AMKA MTANZANIA na wapenzi wa kusoma vitabu.

 
Habari njema sana.
Kwa muda mrefu wasomaji wengi wamekuwa wakishindwa kusoma vitabu ambavyo tumekuwa tunawashirikisha kila mwezi. Wasomaji hawa wamekuwa na kiu ya kusoma vitabu, ila wanakwama kutokana na changamoto ya lugha. Vitabu ambavyo tumekuwa tunawashirikisha vimeandikwa kwa lugha ya kiingereza, ambayo siyo lugha mama kwetu. Hivyo hili limekuwa changamoto kwa wengi na kuwazuia kupata maarifa.
Ni kutokana na changamoto hii nimeandaa utaratibu mpya wa kuwashirikisha vitabu vya kujisomea, ambapo sasa kila mwezi nitawashirikisha kitabu cha kujisomea cha kiswahili. Kila mwezi nitakuwa naandaa kitabu kizuri sana na chenye maarifa ya kuboresha maisha yetu na kuwashirikisha kama kitabu cha kujisomea kwa mwezi husika. Kitabu kitapatikana kwa gharama ndogo kwa wale ambao watapenda kuwepo kwenye utaratibu huu wa kupokea kitabu cha kujisomea kila mwezi.
Utaratibu huu utaanza mwezi wa tano, kwa mwezi huu wa nne tutamalizia na kitabu cha kiingereza, ila pia kuna maboresho makubwa nimeyafanya kwenye kitabu ninachokwenda kuwashirikisha mwezi huu.
Niambie unaonaje utaratibu huu mpya wa vitabu vya kujisomea kila mwezi, nijibu kwa email kwa kutuma email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz pia niambie kama utapenda kuwa kwenye kikundi cha watu ambao watapokea vitabu hivi kila mwezi.
Kitabu cha kujisomea mwezi Aprili.
Mwezi huu wa nne tunakwenda kusoma kitabu; THE SEVEN HABITS OF HIGHLY EFFECTIVE PEOPLE (Tabia Saba Za Watu Wenye Ufanisi Wa Hali Ya Juu). Hiki ni kitabu kizuri sana kuhusu kujijengea tabia muhimu za mafanikio, kuanzia na mtu mwenyewe, pia kujenga ushirikiano bora na wale wanaokuzunguka. Kitabu hiki kimeandikwa na Stephen Covey.
Hiki ni kitabu ambacho nashauri kila mtu apate muda na kukisoma, na utapata maarifa bora sana yatakayobadili maisha yako kabisa kama utayatumia.
Ili kuhakikisha unapata thamani kubwa kutoka kwenye kitabu hiki, nimekuandalia uchambuzi mzuri wa kitabu hiki kwa lugha ya kiswahili. Na leo nitakushirikisha uchambuzi huu bure kabisa ili upate nafasi ya kujifunza.
Kupata uchambuzi huu wa kitabu bonyeza maandishi haya na utapakua kijitabu kidogo nilichokuandalia chenye uchambuzi huu mzuri. Na ukishakipata kijitabu hiko na kusoma, pia washirikishe wengine kwa kuwatumia ili nao wajifunze.
Ili kupata kitabu chenyewe kwa ajili ya kukisoma kwa undani, jiunge na kundi la AMKA MTANZANIA telegram kwa kubonyeza hapa. Hakikisha una application ya telegram kwenye simu yako kisha bonyeza maandishi haya na bonyeza JOIN GROUP na utakuwa umejiunga. Ndani ya kundi hili utajifunza mengi pamoja na kupata vitabu. Kama hujui telegram ni nini, inafanana na wasap, nenda kwenye play store na tafuta telegram, chagua telegram messenger, iweke kwenye simu yako kama unavyoweka wasap, kwa kusajili namba yako. Baada ya hapo bonyeza haya maandishi na utajiunga. Kama ukishindwa save namba yangu ambayo ni 0717396253 kisha nitumie ujumbe AMKA MTANZANIA na nitakuweka kwenye kundi.
Karibu sana kwenye kundi la AMKA MTANZANIA telegram kwa ajili ya kupata vitabu na kujifunza mengine mengi zaidi.
Pata uchambuzi wa kitabu THE SEVEN HABITS OF HIGHLY EFFECTIVE PEOPLE (Tabia Saba Za Watu Wenye Ufanisi Wa Hali Ya Juu). Kwa kubonyeza haya maandishi.
Na kwa kupata kitabu chenyewe, bonyeza maandishi haya na ujiunge na AMKA MTANZANIA telegram kwa kubonyeza maandishi haya..
Pia usisahau kunishirikisha unaonaje mpango huu mpya wa kusoma kitabu cha kiswahili kila mwezi.
Nakutakia kila la kheri kwenye kusoma kitabu hiki cha mwezi wa nne.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: