Habari rafiki?
Napenda kuchukua nafasi hii kukufahamisha ya kwamba zimebaki siku mbili pekee kwako wewe kuweza kupata nafasi bora sana ya kushiriki semina ya UTOAJI WA HUDUMA BORA KWA WATEJA. Ni nafasi bora sana na ya kipekee kwa sababu semina hii ikishaanza hutapata tena nafasi ya kujiunga. Na pia tukishafanya semina hii haitarudiwa tena.
Hii ni semina muhimu sana ambayo wewe kama rafiki yangu hupaswi kuikosa. Kwa sababu ni semina ambayo itakuwezesha kujenga mahusiano bora na watu wote wanaokuzunguka. Japo jina ni HUDUMA KWA WATEJA, siyo lazima mteja awe ni yule anayenunua kitu kwako. Kwa kuwa tunaishi kwenye uchumi w akutegemeana, basi kila anayekuzunguka ni mteja wako.
Biashara za sasa zinaendeshwa kirafiki, siyo kama zamani ambapo watu walikuwa hawana namba bali kununua hata kama muuzaji hakuwa anatoa huduma bora. Sasa hivi watu wana nguvu kubwa ya kuchagua, wanaweza kuchagua kuja kwako au kuenda kwa mwingine kwa sababu biashara yoyote unayofanya, kuna wengine wengi pia wanaifanya. Sasa unaweza kuwa sumaku ambayo inawavutia wengi zaidi kuja kwako.
Na hata kwenye ajira pia, wanaohitaji nafasi za ajira ni wengi na hivyo waliopo kwenye ajira hawana tena nguvu kubwa ya kudai chochote wanachotaka. Lakini unapoongeza thamani yako na kuwa kubwa zaidi kwa kuwa na mbinu bora za mahusiano yako na wale wanaokuzunguka, unajipa nguvu kubwa ya kuweza kudai chochote unachotaka.
Hii ndiyo sababu semina hii ni muhimu sana kwako rafiki yangu, nakushauri sana usiikose, kwa sababu utakosa mengi. Na kibaya zaidi ni kwamba vitu hivi huwa havifundishwi mara kwa mara na hivyo utajikuta ukifanya kwa mazoea.
Semina hii itaendeshwa kwa njia ya mtandao, yaani kwa njia ya kutumiwa masomo kwenye email yako na pia kuwepo kwenye kundi la wasap. Hivyo unaweza kushiriki semina hii popote pale ulipo duniani, huhitaji kutoka na kwenda eneo la semina, utayapokea mafunzo hapo ulipo. Utakuwa na mambo ya kufanyia kazi na pia utapata nafasi ya kuuliza maswali na kushiriki mijadala mbalimbali itakayohusiana na mafunzo haya.
Karibu sana ushiriki semina hii. Semina itaanza tarehe 02/05/2016, lakini mwisho wa kujiunga ni tarehe 30/04/2016, hivyo zimebaki siku mbili tu. Kama kweli unataka kushiriki semina hii na bado hujajiunga basi fanya hima kwa sababu muda uliobaki  ni mchache sana. Chukua hatua sasa usije kuipoteza nafasi hii nzuri sana kwako.
Katika semina hii tutajifunza yafuatayo;
1. Kila mtu anauza, je wewe unauza nini?
2. Nani ni mteja wako?
3. Mahitaji ya msingi ya mteja wako.
4. Jinsi ya kutatua hali ya kutoelewana baina yako na mteja wako.
5. Mfanye mteja kuwa rafiki yako.
6. pokea maoni ya wateja wako.
7. Kitu kimoja unachotakiwa kuzingatia sana na kitakunufaisha wewe na mteja wako.
8. Gharama za huduma mbovu kwa wateja wako.
9. Vaa viatu vya mteja wako.
10. Matumizi ya mtandao na teknolojia katika kuboresha huduma kwa wateja.
Karibu sana ushiriki semina hii ambayo itakupa mbinu bora za kutoa huduma bora kwa wateja wako na hivyo kuendelea kufanikiwa kwenye biashara na kazi yako. Kushiriki semina hii tuma ada ya ushiriki ambayo ni tsh elfu 20 (20,000/=) kwenye namba zifuatazo; mpesa 0755 953 887, tigo pesa 0717 396 253 namba zote jina ni Amani Makirita. Baada ya kufanya malipo tuma ujumbe kwenye moja ya namba hizo au tuma ujumbe kwa wasap kwenye namba 0717396253 Ujumbe uwe na majina yako kamili na neno SEMINA YA HUDUMA KWA WATEJA. Pia bonyeza maandishi haya na jaza taarifa zako.
Ni wakati sasa wa kuongeza umakini kwenye biashara na kazi yako ili uweze kufikia mafanikio makubwa zaidi. Karibu tujifunze kwa pamoja.
TUPO PAMOJA,
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani.
makirita@kisimachamaarifa.co.tz