Habari rafiki?
Nina imani mpaka sasa unajua ya kwamba mwezi wa tano tutakuwa na semina yetu ya pili kwa mwaka huu ambayo itaendeshwa kwa njia ya mtandao. Na pia nina imani unajua imebaki siku moja tu ya kuweza kujiunga na semina hii nzuri sana kwa kukuongezea maarifa ya kuboresha mahusiano yako na wale ambao wanakuzunguka kwenye kile unachofanya.
Kama mpaka sasa bado hujachukua hatua ya kujiunga na semina hii kwa sababu upo njia panda iwapo ushiriki au la, basi napenda nichukue nafasi hii kukupa ufafanuzi zaidi, kwa yale mambo ambayo unaweza kuwa una wasiwasi nayo.
1. Kuhusu utapeli.
Kama unafikiri semina hii kwa njia ya mtandao ni utapeli, ya kwamba ukituma fedha yako basi unaibiwa, usishiriki semina hii. Nakubaliana kabisa na wewe ya kwamba kwenye mtandao kuna utapeli mwingi. Lakini mimi natoa semina hizi kwa marafiki zangu, watu ambao tupo pamoja kwa muda mrefu, ambao wameshanunua vitu vingine kwangu kwa njia hii ya mtandao na wakavipata bila ya tatizo. Nimekuwa naendesha semina hizi kwa miaka mitatu sasa, na nategemea kuziendesha kwa miaka mingi ijayo, hivyo kama una wasiwasi nakushauri usome makala nyingi zaidi kwenye AMKA MTANZANIA na KISIMA CHA MAARIFA utapata thamani kubwa na kisha wakati mwingine utaona kama ni salama kwako kushiriki au la.
2. Kuhusu thamani.
Huenda upo njia panda kama kweli utapata thamani inayoendana na ada unayolipia kwenye semina hii. Huenda una wasi wasi kwamba hutapata thamani kubwa inayoendana na ada unayolipa, elfu 20 ni kubwa sana, unaweza kufanya nayo vitu vingi vya msingi zaidi.
Napenda nikuambie kwamba thamani ndiyo kitu pekee ninachopigania mimi, napenda kutimiza kile ambacho ninaahidi. Na kama ikitokea umeshiriki semina lakini hukupata thamani uliyotegemea, huna cha kupoteza, wewe niandikie tu ya kwamba SIKUPATA THAMANI KWENYE SEMINA HII, ukiwa umeambatanisha namba yako ya simu na nitakurudishia fedha uliyolipa, bila ya kukuuliza swali lolote lile.
Hivyo unaweza kushiriki semina hii bure kabisa, unalipa ada, unapokea mafunzo na mwisho unasema hujapata thamani, na ninakurudishia ada uliyolipa.
NIDHAMU, UADILIFU na KUJITUMA ndiyo vitu ambavyo navisimamia kwenye jambo lolote ninalochagua kufanya, na kama umekuwa rafiki yangu mpaka sasa utakuwa unalijua hilo. Hivyo ondoa wasi wasi wowote iwapo utapata thamani au la.
Nakuahidi kitu kimoja, UTAPATA THAMANI YA FEDHA ULIYOLIPA, AU UTARUDISHIWA FEDHA YAKO. Hakuna mjadala mwingine.
3. Muda bado upo.
Huenda kitu kingine ambacho kinakuweka njia panda mpaka sasa hujafanya maamuzi ya kujiunga na semina hii ni kuona muda bado upo. Naomba nikukumbushe ya kwamba imebaki siku moja tu, na hivyo kama kweli unataka kushiriki semina hii, jiunge leo kwa kulipa ada na kutuma taarifa zako. Ikishafika mwisho hutapata tena nafasi hii.
Mara zote ambazo nimekuwa naendesha semina, kuna watu wamekuwa wakitaka kuingia kwenye semina baada ya muda kupita na mafunzo yameanza. Mara zote huwa nawauliza kwa nini wamechelewa na sababu huwa kwamba walisahau, au hawakusoma email na mengine kama hayo. Pamoja na sababu hizi bado wamekuwa wanaikosa nafasi. Naomba nikujulishe mapema rafiki yangu, kama unataka kuipata nafasi hii wakati bora kwako ni leo hii, sasa hivi unaposoma hapo, jiunge kwanza ndiyo uendelee kusoma.
4. Semina inafanyikaje kwa njia ya mtandao, nimezoea kuhudhuria.
Ni kweli tumezoea semina za kuhudhuria, lakini hiyo siyo njia pekee ya kupata mafunzo ya semina. Na ukizingatia ulimwengu wa sasa ambao kila mtu muda ni tatizo kwake, kupata siku moja nzima au mbili kukaa kwenye semina siyo rahisi. Na kingine muhimu ni kwamba kuna watu wengi wapo mikoani mbalimbali, wengine vijijini kabisa, kusema wahudhurie semina inabidi wapange safari ambayo itawachukua muda mrefu. Lakini pale wanapoweza kupata mafunzo ya semina wakiwa walipo, inakuwa ni nafasi bora zaidi kwao.
Karibu sana, utapata mafunzo bora na ili mafunzo hayo yakunufaishe, kutakuwa na mambo ambayo utahitaji kuyafanyia kazi kwenye kila somo. Utajifunza mengi sana, nakuahidi hilo.
Karibu sana kwenye semina hii, na kama una swali au wasiwasi wowote ambao sijaujibu hapo juu unaweza kuniuliza kwa simu 0717396253, fanya mapema kabla muda haujaisha.
Karibu sana rafiki yangu tujifunze kwa pamoja.
Semina hii itaendeshwa kwa njia ya mtandao, yaani kwa njia ya kutumiwa masomo kwenye email yako na pia kuwepo kwenye kundi la wasap. Hivyo unaweza kushiriki semina hii popote pale ulipo duniani, huhitaji kutoka na kwenda eneo la semina, utayapokea mafunzo hapo ulipo. Utakuwa na mambo ya kufanyia kazi na pia utapata nafasi ya kuuliza maswali na kushiriki mijadala mbalimbali itakayohusiana na mafunzo haya.
Karibu sana ushiriki semina hii. Semina itaanza tarehe 02/05/2016, lakini mwisho wa kujiunga ni tarehe 30/04/2016, hivyo imebaki siku moja tu. Kama kweli unataka kushiriki semina hii na bado hujajiunga basi fanya hima kwa sababu muda uliobaki  ni mchache sana. Chukua hatua sasa usije kuipoteza nafasi hii nzuri sana kwako.
Katika semina hii tutajifunza yafuatayo;
1. Kila mtu anauza, je wewe unauza nini?
2. Nani ni mteja wako?
3. Mahitaji ya msingi ya mteja wako.
4. Jinsi ya kutatua hali ya kutoelewana baina yako na mteja wako.
5. Mfanye mteja kuwa rafiki yako.
6. pokea maoni ya wateja wako.
7. Kitu kimoja unachotakiwa kuzingatia sana na kitakunufaisha wewe na mteja wako.
8. Gharama za huduma mbovu kwa wateja wako.
9. Vaa viatu vya mteja wako.
10. Matumizi ya mtandao na teknolojia katika kuboresha huduma kwa wateja.
Karibu sana ushiriki semina hii ambayo itakupa mbinu bora za kutoa huduma bora kwa wateja wako na hivyo kuendelea kufanikiwa kwenye biashara na kazi yako. Kushiriki semina hii tuma ada ya ushiriki ambayo ni tsh elfu 20 (20,000/=) kwenye namba zifuatazo; mpesa 0755 953 887, tigo pesa 0717 396 253 namba zote jina ni Amani Makirita. Baada ya kufanya malipo tuma ujumbe kwenye moja ya namba hizo au tuma ujumbe kwa wasap kwenye namba 0717396253 Ujumbe uwe na majina yako kamili na neno SEMINA YA HUDUMA KWA WATEJA. Pia bonyeza maandishi haya na jaza taarifa zako.
Ni wakati sasa wa kuongeza umakini kwenye biashara na kazi yako ili uweze kufikia mafanikio makubwa zaidi. Karibu tujifunze kwa pamoja.
TUPO PAMOJA,
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani.
makirita@kisimachamaarifa.co.tz