Ijue sababu hii kubwa iliyopo nyuma ya biashara yako itakayokuwezesha kufikia mafanikio makubwa.

Kwenye biashara, kuna sababu za kufanya biashara zinazoonekana na wengi na kuna sababu ambazo hazionekani na wengi. Sababu zinazoonekana na wengi ni kile unachouza na faida unayopata. Hiki ndiyo kinawasukuma wengi kuingia kwenye biashara. Pale mtu anapoona kuna fursa ya uhitaji wa kitu fulani na katika kukitoa kitu hiko anaweza kupata faida basi anaingia kwenye biashara hiyo. Sababu hizi pia ndizo zinawasukuma wafanyabiashara wengine wengi nao waingie kwenye biashara.

Biashara ambazo zinapata wateja wengi na kukua zaidi ni zile ambazo waendeshaji wa biashara hizo wanajua sababu kubwa iliyopo nyuma ya biashara hizo. Licha ya kutoa bidhaa au huduma ambazo watu wanazihitaji na wao kuweza kupata faida, wana sababu nyingine kubwa kwenye biashara hizo ambayo inawavutia wateja wengi zaidi kuja kwenye biashara hizo.
 

KUPATA KITABU HIKI KITAKACHOKUWEZESHA KUANZ ANA KUKUZA BIASHARA YAKO UKIWA BADO UMEAJIRIWA BONYEZA MAANDISHI HAYA.


Sababu kubwa iliyopo nyuma ya biashara zinazofanikiwa na kukua siyo ile bidhaa au huduma ambayo wanatoa, bali ni ile namna wateja wanavyonufaika kupitia biashara hizo. Ni kwa namna gani maisha ya wateja yanakuwa bora sana kwa kununua bidhaa au huduma ambazo mfanyabiashara anazitoa? Hii ndiyo sababu kubwa ambayo imewezesha biashara nyingi kukua. Sababu hii inaangalia ni kipi hasa mteja anachonufaika nacho, ni kwa namna gani maisha yake yanaboreshwa kupitia biashara hiyo. Hapa unaacha kuangalia faida pekee na kuangalia maisha ya wengine kuwa bora zaidi.

Kwa mfano mfanyabiashara wa magodoro badala ya kuona anauza magodoro anaona anatoa huduma ya watu kuwa na mapumziko bora baada ya shughuli zao za kila siku. Mfanyabiashara wa chakula badala ya kuona anawauzia watu chakula, anaona anawapa watu huduma ya kuzijenga afya zao ili waweze kuwa na uwezo na nguvu za kuweka juhudi kwenye maisha yao na kupata mafanikio. Mwenye biashara ya kufanya usafi badala ya kuona anaondoa taka taka pekee, anaona anayafanya mazingira ya watu kuwa bora na hivyo kuweza kufanya kazi zao na kuishi kwenye mazingira bora kiafya. Kwenye kila biashara kuna sababu ambayo haionekani kwa haraka lakini ndiyo sababu inayomfanya mteja aamue kununua kile ambacho unakiuza.

SOMA; USHAURI; Jinsi Unavyoweza Kufanya Biashara Yenye Mafanikio Ukiwa Bado Umeajiriwa.

Ni wapi unapotumia sababu hii iliyo nyuma ya biashara yako?
Swali ambalo mfanyabiashara anaweza kuuliza ni kwa nini ahangaike kutafuta sababu iliyopo nyuma ya biashara yake? Kwa nini asiendelee kutoa kile anachotoa na kupata faida ambayo anaipata? Hapa tutaangalia sababu za kila mfanyabiashara kujua sababu kubwa iliyopo nyuma ya biashara yake na kuweza kuitumia vizuri.

1. Kutengeneza wateja wa kudumu kwenye biashara.
Lengo kuu la biashara yoyote ile ni kutengeneza wateja, halafu wateja hawa ndiyo wanaokuletea faida. Pale ambapo wateja wanajua wakija kwenye biashara yako matatizo yao yanatatuliwa, wanakuwa wateja wakudumu na waaminifu kwako na kwa biashara yako. unapoijua sababu iliyopo nyuma ya biashara yako unaona ni jinsi gani wateja wananufaika na maisha yao kuwa bora kupitia biashara unayofanya. Kwa kujua hayo unaweka mkazo zaidi kwenye kile ambacho wateja wanakipata na hivyo kuweza kuwafikia wateja wengi zaidi.

2. Kumudu ushindani wa kibiashara.
Sasa hivi kila biashara ambayo mtu anafanya, kuna watu wengine wengi ambao wanafanya biashara kama hiyo. Mteja ana uhuru mkubwa wa kuchagua ikiwa anunue kwako au akanunue kwa mtu mwingine anayefanya biashara kama unayofanya wewe. Unapoijua sababu ambayo ipo nyuma ya biashara yako unaweza kuitumia vizuri na kuhakikisha wateja wakija kwenye biashara yako wanapata huduma za tofauti kabisa ukilinganisha na anazopata kwa wafanyabiashara wengine. Kwa njia hii utaweza kumudu ushindani wa kibiashara na kuendelea kujipatia wateja wa kudumu kwenye biashara yako.

3. Kuweza kushawishi wateja wapya na kutangaza biashara yako.
Moja ya njia za kuwafikia wateja wengi na wapya wa biashara yako ni kufanya matangazo. Matangazo yapo ya aina nyingi, kuna matangazo kupitia vyombo vya habari kama redio, tv na magazeti. Pia kuna matangazo kwa njia za kawaida, kupitia mabango, vipeperushi na hata taarifa mbalimbali zinazotolewa kuhusu biashara. Kumbuka unapotoa tangazo la biashara, linamfikia mtu ambaye hakujui wewe ni nani na hana uhakika kama kweli unachosema unaweza kutoa kweli. Na pia mtu huyo anakutana na matangazo mengi ambayo yanafanana na biashara yako. unapojua sababu iliyopo nyuma ya biashara yako, na kutumia sababu hiyo kuitangaza biashara yako, utawapa watu shauku ya kutaka kufika kwenye biashara yako na kuwa sehemu ya wanaopata manufaa ya biashara yako. hapa unagusa moja kwa moja mahitaji ya msingi ya watu na kuwafanya waje kwenye biashara yako na kujionea wao wenyewe. Wanapofika na ukawapatia kile ambacho wanakihitaji, wanaendelea kuwa wateja wako.

SOMA; USHAURI; Una Mtaji Lakini Hujui Ni Biashara Gani Ufanye? Soma Hapa Kujua.

Unawezaje kujua sababu iliyopo nyuma ya biashara yako?
Hili ni zoezi muhimu ambalo kila mfanyabiashara anapaswa kulifanya kwa sababu linabadili kabisa mtazamo wake juu ya biashara anayofanya na pia kubadili mtazamo wa wateja juu ya biashara hiyo. Ili kujua sababu iliyopo nyuma ya biashara unayofanya, fuata hatua hizi;
Kwanza jua ni kitu gani hasa unachouza, iwe ni bidhaa au huduma, ijue vizuri na inafanyaje kazi.
Pili jua wateja wa bidhaa au huduma hiyo ni watu wa aina gani. Jua wana matatizo au changamoto gani ambazo bidhaa au huduma unayotoa inawawezesha kuondokana nazo. Au ni mahitaji gani wanayo ambayo bidhaa au huduma unayotoa inawawezesha kukidhi mahitaji hayo.
Tatu angalia ni namna gani maisha ya mtu yanabadilika na kuwa bora sana baada ya kutumia bidhaa au huduma unayotoa. Angalia anakuwa ametoka wapi na kufika wapi, angalia anakuwa amenufaikaje na kuridhishwaje baada ya kutumia bidhaa au huduma hiyo. Na hii ndiyo inakuwa sababu kubwa iliyopo nyuma ya biashara yako. kwa kuitumia hii unaweza kuwashawishi wengi na kutengeneza wateja wa kudumu kwenye biashara yako.
Hakikisha unaijua sababu kubwa iliyopo nyuma ya biashara yako, sababu ambayo inawafanya watu wafurahie kuendelea kufanya biashara na wewe na hii itaiwezesha biashara yako kukua zaidi. Kila la kheri.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz

MUHIMU; Kila siku naandika makala nzuri za kukuwezesha kuwa na maisha bora, ya furaha na mafanikio makubwa. makala hizi zinapatikana kwenye kipengele cha KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Kuweza kusoma makala hizi unahitaji kujiunga kwa kulipa ada ya mwaka. Kujiunga tuma ujumbe kwenye wasap kwenda namba 0717396253. karibu sana rafiki yangu.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: