Faida Kubwa Ya Kufanya Kazi Kwa Ushirikiano.

Watu wengi tumekuwa na mitazamo ambayo imekuwa haitusaidii hata chembe, kwani tumekuwa tunaamini katika kufanya kazi peke yetu pasipo kuwashirikisha wengine, lakini kufanya hivi ni sawa na kuzima moto kwa chafya, lakini ukweli ambao haufichiki ni kwamba ukitaka kwenda haraka, nenda peke yako ila ukitaka kwenda mbali nenda na wengine.
Hiyo ni falsafa nzuri sana husani katika suala zima la kuyasaka mafanikio. Pia katika suala zima la mafanikio tukumbuke ule usemi ambao husema ushirikiano ni nguvu na utengano ni dhaifu.
Ili kulielewa hili vizuri la kufanya kazi kwa shirikiano hebu angalia kisa hiki cha Yumba yumba. Tunaambiwa kwamba kupitia kisa hiki katika kisiwa fulani kulikuwako na mfalme mmoja ambaye alifahamika kwa jina la Michael.
Hata hivyo lakini watu wake walimfahamu zaidi kwa jina la Lipamila, kitu ambacho watu wengi walijifunza kutoka kwa mfalme huyo ni vile ambavyo alipenda sana kufanya kazi, hususani masuala ya kilimo, hasa katika kulima mbogamboga.

 Watu wengi sana katika kisiwa kile walifurahia sana kuwepo kwa mfalme yule mahala pale, kwani wengi wao walijifunza mambo mengi sana kutoka kwa mfalme.
Siku moja mfalme lipamila aliamua kuitisha mkutano mkubwa sana, alisisitiza kwa hali ya juu sana ya kwamba kila mtu siku ya mkutano huo,  alifanya hivo ili kuhakikisha ya kwamba kila mmoja ambaye alikuwepo katika kisiwa kile aweze kuhudhuria mkutano ule.
Hivyo taarifa zilisambaa katika kisiwa kile, ingawa kila mmoja alikuwa ana shauku ya kutaka kujua kunanini katika mkutano ule, kwani haijawahi kutokea kwa mfalme lipamila kuweza kusisitiza watu kuhudhuria mkutano ule kiasi kile.
Siku ya mkutano iliwadia na kila mmoja ambaye aliishi katika kisiwa kile alifika pasipo kukosa, ndipo mfalme akaanza kwa kusema “awali ya yote nipende kumshukuru Mungu kwa kuweza kutufikisha siku ya leo na hatimaye tumeweza kufika hapa”
Lakini jambo la pili nipende kuchukua fursa hii adhimu kwa kuwashukuru ninyi nyote kuweza kufika mahali hapa, pia nafahamu ya kwamba kila mmoja aliyo mahala hapa anawiwa kutaka kujua leo nitasema neno gani?
Lakini niwaambie ya kwamba huwezi kumuua chura kwa kumtupa ndani ya maji, maana yangu kuwaita hapa nataka nizungumze vitu ambavyo vitawasaidia katika maisha yenu ninyi nyote hivyo niwapongeze tena kwa kuweza kufika mahala hapa, 
Labda niende moja kwa moja katika lengo langu la kuwaita mahala hapa;
Jambo la kwanza ni kwamba nafahamu ya kwamba hapa tulipo kuna watu wa aina mbalimbali kutokana imani tofautitofauti na itikati za aina kadha wa kadha, lakini nataka niwaambie ya kwamba ili tuweze kufika mbali kimaendeleo na kimafanikio hatuna budi kuwa wamoja katika kufanya kazi kwa pamoja kama mchwa bila kujali tofauti zote ili tuweze kufika mbali kimafanikio, nasema hivi kwa sababu katika kisiwa hiki watu ni wamoja lakini hatuna ushirikiano katika mambo mengi sana.
Mfalme lipamila akashusha pumzi kidogo kisha akaendelea …”Tunasema ya kwamba kisiwa chetu kinaogozwa na falsafa ya “HAPA KAZI TU” lakini kila mmoja amekuwa mbinafsi katika kufanya kazi lakini niwaambie ya kwamba ili kuona falsafa hiyo ni lazima kwa mmoja wetu tuweze kupeana mbinu mbalimbali ambazo zinatufanya tuweze kupata mafanikio kutokana na kuelimisha sisi kwa sisi, ifike mahali hata kilimo ambacho tunakifanya kiwe na tija, maana tukiwa na ushirikiano tunaweza kufika mbali. 
Tutaweka utaratibu ambao tulipama kilimo ambacho ni tofauti ni tulichozea, nimeweka utaratibu ambao tutahakikisha ya kwamba tutalima kilimo cha kisasa, yaani tutalima sehemu ndogo lakini mavuno yatakuwa mengine, nmefanya pia utafiti kuhusu masoko ya kuhusu mazao ambayo tutalima kwani tutauza sana sehemu nyinginezo endapo tutashirikiana pamoja.
Jambo jingine ambalo nilitaka kulizungumza nanyi siku ya leo ni kwamba nafahamu fika ya kwamba tatizo la ajira ni kubwa sana, 
“Je unataka kujua mfalme lipamila alizungumza nini katika suala la ajira?
Usikose mwendelezo wa makala haya juma lijalo siku kama hii ya leo, upate kitu kizuri cha kujifunza.
Makala hii imeandikwa na Afisa mipango Benson Chonya.

0757909042

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: