Kama Unaishi Sana Kwa Kufikiri Hivi…Huna Mafanikio.

Acha kufikiri kwa kudhani kwamba ni kazi rahisi kutekeleza jukumu fulani eti kwa sababu umemuona rafiki yako kalifanikisha jambo hilo kwa urahisi. Inaweza ikawa ni ngumu sana kuliko unavyowaza, kwa sababu hujui changamoto alizozipitia.
Acha kufikiri kwamba eti kuuliza jambo fulani ambalo hulijui, linaweza likakupotezea uaminifu wako kwa watu. Kama hizo ndizo fikra zako basi zitakuwa zinakuangusha.  Kama kuna kitu hukijua uliza na itakusaidia sana kufanikiwa.
Acha kufikiri eti kwa sababu umeshindwa kwa jambo unalolifanya basi eti maisha yako ndio hayawezekani tena kuwa ya mafanikio. Unaweza kufanikiwa kwa kuanza tena upya hata kama imetokea umeshindwa mara mia moja.
Acha kuchukulia kwa kudhani kwamba kwa sababu unaona mambo ni magumu, mipango haiendi na ndoto zako uniona kama hazitimii, ukaona maisha ndio basi hayawezekani. Maisha yako yanaweza kubadilika tena na kuwa bora zaidi ya hapo ulipo.

Acha kufikiri kwamba utakataliwa kwenye jambo ambalo hata bado hujaomba. Kama kuna kazi unaitaka peleka barua, acha kudhani kwamba hutapata hata kabla hujaomba.  Acha kufikiri hivyo mara moja. Fikra hizo ni sumu kubwa sana ya mafanikio yako.
Acha kufikiri mawazo yako ni lazima yatakuwa hayana thamani hata kabla hujayaotoa. Kama una mawazo ya kutoa sehemu yatoe mawazo hayo bila kujishauri. Badili kampuni yako kwa kutoa wazo lako na wala usilifiche. Nani kakwambia kwamba wazo lako halina thamani?
Acha kudhani kila mtu ana hamasa kubwa ya kufanikiwa kama uliyonayo wewe. Ikiwa utajiaminisha hivyo basi utakuwa unajidanganya. Wengine ni wasindikizaji tu wala hata hawana mpango wa kufanikiwa sana kama ulivyo wewe.
Acha kudhani kwamba utatatua changamoto kubwa kwenye maisha yako kwa kuweka juhudi kidogo na za kawaida. Huwezi kutataua changamoto hizo kwa ‘staili’ hiyo. Inatakiwa kuweka juhudi nyingi na tena kwa nguvu nyingi ili kushinda changamoto za kimaisha.
Acha kufikiri maisha uliyonayo leo au kile kinachofanya vizuri leo kinaweza kufanya vizuri hivyo hata kesho ikiwa hutachukua hatua za kukiboresha. Ikiwa utakuwa unafikiri hivyo, andika maumivu, ni lazima utashindwa sana mpaka utashangaa.
Acha kufikiri kwa kudhani kwamba ipo njia ambayo unaweza kuitumia kukimbia changamoto zako mwenyewe. Hakuna njia ambayo unaweza kuitumia kukimbia changamoto zako. Kama unafikiri ipo, unajidanganya na jiandae kushindwa.
Acha kujifikiria huwezi kufanikisha mambo makubwa eti kwa sababu kila mtu ukimuangalia hakuna aliyefanikiwa kwa sehemu kubwa. Uwezo huo wa kufanikiwa kwa kiasi kikubwa unao tena sana hata kama wengine hawajafanikiwa kwa kiwango hicho.
Acha kufikiria kwamba changamoto uliyonayo ni kubwa sana na huiwezi. Kama unajifikiria hivyo basi ni wazi huwezi kufanikisha jambo lolote. Kila changamotio unayoiona mbele yako, una uwezo wa kukabiliana nayo na kuishinda.
Kumbuka, kuna wakati tunashindwa sana katika maisha kwa sababu ya kuishi kwa kufikiri au kudhani. Ili ufanikiwe unatakiwa uishi kwa uhalisia na sio kuishi kwa kufikiri iko hivi kumbe uhalisia uko vile.
Wengi wamekua wakikwama kwa sababu ya kudhani. Je, jiulize ni mara ngapi umekuwa ukichukulia na kuamini kwamba jambo linatakiwa hivi, kumbe badala yake linakuwa vile.
Kuanzia sasa acha kuishi kwa kudhani tena…kama utaendelea kushi kwa kufikiri…kama utaendelea kuishi kwa kudhani…basi hakuna mafanikio makubwa utayoweza kuyaambulia.
Endelea kujifunza kupitia www.amkamtanzania.com kila siku.
TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,

One thought on “Kama Unaishi Sana Kwa Kufikiri Hivi…Huna Mafanikio.

Add yours

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: