Vichocheo Saba Vinavyowasha Moto Wa Mafanikio Kwenye Jambo Lolote Lile.

Habari Mpendwa Rafiki na Msomaji wa Amka Mtanzania? Ni matumaini yangu uko salama rafiki na unaendelea na shughuli zako za kila siku. Napenda kukualika katika makala yetu ya leo nakusihi ungana nami mwazo hadi tamati ya makala hii.

Katika makala yetu ya leo tutajifunza vichocheo saba vinavyowasha moto wa mafanikio kwenye jambo lolote lile. Katika kufanya kazi mbalimbali watu hufanya kazi kulingana na hamasa wanayopata kwenye maisha yao. Kuna aina mbili za hamasa yaani hamasa ya ndani (intrinsic motivation) na hamasa ya nje (extrinsic motivation). Kama unataka kufanikiwa na kupata hamasa ya kudumu kwenye jambo lolote lile tumia hamasa ya ndani lakini ukitegemea hamasa za nje huwa hazidumu sana utafanya leo kesho hamasa imetoweka. Licha ya kuwa na hamasa zote mbili lakini mtu ambaye anapenda kazi huwa ni mtu ambaye ana hamasa ya ndani atafanya bila kujali kitu chochote kile. Mpenzi msomaji, karibu sasa tujifunze vichocheo vinavyowasha moto wa mafanikio kwenye jambo lolote lile katika maisha yako.

 

1. Juhudi ; siku zote ukiwa unajituma na kufanya kazi kwa juhudi hakika utafika mbali. Juhudi ni moja ya kichocheo kinachowasha moto wa mafanikio kwenye jambo lolote lile. Kama huna juhudi au bidii ni sawa na kuchora sifuri kwenye maji rafiki yangu kwani juhudi ni kama lifti inayokuvusha kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine. Kama unataka ushindi tumia kichocheo cha juhudi na utafanikiwa kwenye jambo lolote lile.

2. Maarifa; silaha ya kuchochea mafanikio ni maarifa. Huwezi kufanya mambo kienyeji na ukategemea kufanikiwa. Dunia imebadilika na mabadiliko yanaendelea kutokea kila siku kwenye maisha yetu. Hata ufanye kazi kwa kujituma namna gani lakini kama huna maarifa sahihi kwenye akili yako ni kazi bure. Lazima ujifunze kulingana na hitaji la soko linavyokwenda sasa na fanya mambo kulingana na mabadiliko yanayotokea kwa jamii na dunia nzima.

SOMA; Mambo Kumi(10) Muhimu Usiyojua Kuhusu Mafanikio, Na Jinsi Yanavyokurudisha Nyuma.

3. Nidhamu; nidhamu ni daraja la mafanikio mpendwa rafiki yangu. Nidhamu siyo jambo la mchezo rafiki yangu unajisimamia mwenyewe bila shuruti na mtu yeyote. Kwa mfano, unajiwekea nidhamu ya kuamka saa kumi au kumi na moja kila siku alfajiri bila sababu au unajiwekea nidhamu ya kuandika makala kila siku katika maisha yako. Kuna mambo mengi ambayo ukiwa unafanya kama huna nidhamu lazima ushindwe. Nidhamu ni utii na kuheshimu kile unachokifanya bila shuruti ya kusukumwa na mtu. Kuna watu wengine wameshazoea kufanya kazi kwa kusimamiwa na mtu ndio afanye kitu Fulani.

4. Kujitoa kwa moyo. Kujitoa kwa moyo ni kufanya kazi unayoipenda kwa moyo. Na mtu yoyote anayejitoa bila kujibakiza kwenye jambo lolote lile huwa anafanikiwa kwenye maisha yake. Jinsi unavyojitoa kwa moyo ndio kinakuwa kichocheo cha kuwasha moto wa mafanikio. Anza kuwasha moto wa huu wa kuchochea kile unachofanya kwenye maisha yako. Kama unafanya kazi kwa shingo upande ni ngumu kupata mafanikio kwenye kile unachofanya yaani unafanya tu ili mradi umalize au ili mradi liende.

SOMA; UCHAMBUZI WA KITABU; PROSPERITY ON PURPOSE (Mwongozo wa kuishi maisha ya mafanikio makubwa).

5. Kutoahirisha mambo. Kama unavyojua watu wengi wanakumbana na changamoto ya kuahirisha mambo katika maisha yao. Kuahirisha mambo ni mwizi wa muda wa watu wengi ni wangapi kila siku wanapanga kufanya jambo Fulani lakini wanaishia njiani kwa kuahirisha. Kutoahirisha mambo ni kichocheo cha kuwasha moto wa mafanikio kwenye jambo lolote lile katika maisha yako. Ukipanga kitu Fulani hakikisha unakifanya kwa moyo na wakati bila kuweka sababu yoyote ile.

SOMA; Kama Unafikiri Mafanikio Yako Hivi Tu, Tayari Umeshapotea.

6. Kutosikiliza wengine wanasema nini. Ukianza kusikiliza wengine wanasema nini utashangaa unazima kichocheo cha kuwasha moto wa mafanikio kwenye maisha yako. Unatakiwa kuwa kiziwi kabisa kutowasikiliza watu kwa sababu wataanza kukukatisha tamaa kama ukiwapa nafasi ya kuwasiliza ndio mwanzo wa kukatishwa tamaa. Wewe sikiliza sauti yako ya ndani kwani ndio inaona kule unakotaka kwenda na siyo mtu mwingine. Hakuna mtu anayekujua wewe zaidi ya wewe mwenyewe. Jisikilize uendelee kuchochea moto wa mafanikio mpaka unafika pale unapotaka kufika.

7. Kutokuwa mtu wa sababu. Kuna watu kazi yao ni kulalamika na kutafuta sababu kila siku ya maisha yao. Akitaka afanye kitu Fulani lazima aanze kutanguliza sababu kwanza. Ukiwa ni mtu wa sababu rafiki sahau kuhusu mafanikio kwenye maisha yako kwani sababu ndio zinazaa vitu kama uvivu, wivu, majungu, umbea, kulaumu na kulalamika. Hivyo acha kuwa mtu wa sababu na washa moto wa mafanikio.

Kwa kuhitimisha, dunia imejaa kelele nyingi sana hivyo ni vema kuangalia kile kitu unachopenda wewe kufanya na siyo kusikiliza watu. Hakuna kichocheo chochote kinachoweza kutokea kwenye maisha yako kama vile radi au ajali lazima uamue kuwa navyo. Habari njema ni kwamba uamuzi ni bure wala huhitaji uwe na mtaji ndio uanze.
Makala hii imeandikwa na Deogratius Kessy ambaye ni mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali, unaweza kuwasiliana naye kupitia namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com, kessydeo@mtaalamu.net au unaweza kutembelea tovuti yake, www.mtaalamu.net/kessydeo ,www.actualizeyourdream.blogspot.com

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s