TAARIFA MUHIMU; Samahani Rafiki, Hatuwezi Kuonana Na Njia Bora Kabisa Ya Kuwasiliana Na Mimi.

Habari za leo rafiki yangu,
Ninaamini ya kwamba unaendelea vizuri na juhudi za kuyafanya maisha yako kuwa bora zaidi. Hongera kwa hatua hizo rafiki yangu. Nikukumbushe tu ya kwamba hakuna namna unaweza kuwa na maisha bora bila ya kuweka juhudi. Juhudi ni muhimu ili kuweza kuwa na yale maisha unayoyataka.

Leo katika makala hii nataka nitoe taarifa ya upatikanaji wangu na njia bora ya kuwasiliana na mimi.

Nawapenda sana marafiki zangu wote, ambao mnachukua muda kusoma kazi zangu na kuzifanyia kazi ili maisha yenu yaweze kuwa bora zaidi. Pia nawapenda sana marafiki zangu wote ambao mnalipia huduma mbalimbali ninazotoa kama vitabu na semina mbalimbali, bila ya kusahau wale mnaolipia na kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Kadiri siku zinavyokwenda ndivyo nawafikia marafiki wengi. Na hivyo pia marafiki wengi wamekuwa wakiomba kukutana na mimi, kwa sababu mbalimbali. Wapo ambao wanataka ushauri wa moja kwa moja kutoka kwangu, wapo ambao wanataka tufahamiane zaidi na wapo wanaotaka usaidizi fulani wa moja kwa moja kutoka kwangu.

SOMA; Njia Mbili(2) Rahisi Unazoweza Kuzitumia Kutengeneza Kipato Kupitia Mtandao Wa Intaneti.

Kila siku marafiki hawa wanakuwa ni wengi, lakini changamoto kubwa ni moja, ambayo ni muda. Sina muda wa kuweza kukutana na kila mtu ambaye anataka tukutane. Nimekuwa naeleza hili lakini siyo wote wananielewa vizuri.

Kumekuwa na marafiki ambao wamekuwa wakinipa malalamiko kutokana na kushindwa kuonana. Malalamiko haya yamekuwa yananifanya nisijisikie vizuri kwa sababu napenda wewe unufaike kupitia kazi zangu. Lakini siyo kila kitu naweza kufanya kama unavyotaka, kuna mambo mengi kama ninavyoelekeza.

Kwa mfano nimekuwa napata ujumbe kama huu hapa chini;
Samahani mimi  nilipenda makala yako ila nikapata shida maelekezo yako kwa kufungua blog nikakuomba unisaidie hukuwa tayari mimi niko wilayani mpaka nilikuja Dar nikakupigia simu ili tuonane unielekeze ukasema kuonana ni vigumu mpaka jioni ukawa umenikatisha tamaa ndio maana mpaka sasa natamani ila nashindwa japo uliniuzia kitabu Ombi mimi ni mteja wako naomba unielekeze vizuri namna ya kutengeneza blog. Asanteni na kama nimetumia maneno magumu nisameheni. Amon Peter.
Jumbe za aina hii ni nyingi sana rafiki, ndiyo maana leo nimeona niseme kitu ili tuweze kuelewana vizuri.

Kwa sasa hatuwezi kuonana kabisa.
Rafiki, nasikitika kusema ya kwamba kuanzia tarehe 01/11/2016 mpaka tarehe 01/05/2017 hatutaweza kuonana kwa njia yoyote ile. Mwanzo nilikuwa nimeweka gharama za kutaka kuonana na mimi, tunapanga appoitment na tunakuwa na muda wa kuongea.
Lakini kwa miezi hii sita, sitaweza kuonana na mtu yeyote yule, hata kama anaweza kulipa gharama kiasi gani.

SOMA; Mambo 20 niliyojifunza kwenye kitabu 85 INSPIRING WAYS TO MARKET YOUR SMALL BUSINESS. (Njia 85 za kutangaza biashara yako)

Sababu kubwa ni kwamba kwa miezi hii sita nitakuwa namaliza shule yangu ya Udaktari wa binadamu, hivyo nahitaji muda mwingi kidogo wa kufanya shule na kuweza kuikamilisha. Imenichukua muda sasa, tangu mwaka 2009, na sasa ni muda wa shule hii kuisha.

Hivyo nasikitika kukujulisha rafiki yangu kwamba kama unataka sana tuonane, haitawezekana, kwa namna yoyote ile.

Ratiba yangu ni ngumu kidogo kwa siku. kila siku naamka saa kumi kamili asubuhi, naandika kwa takribani saa moja na nusu, mpaka saa kumi na moja na nusu, baada ya hapo najiandaa kuondoka nyumbani. 

Kuanzia saa 2 asubuhi mpaka saa 11 jioni ni muda wa shule, na kuanzia saa 11 jioni mpaka saa mbili usiku nakuwa na kazi nyingine za shule. Hiyo ni kila siku, juma tatu mpaka ijumaa. Siku za mwisho wa wiki nina miradi ya kampuni yetu ya KICOL ambayo nahitaji kuifuatilia kwa karibu sana. Hivyo hakuna namna yoyote tunayoweza kuonana rafiki yangu.

Njia ya uhakika ya kuwasiliana na mimi.
Marafiki zangu pia wamekuwa wakilalamika kuhusu kutokunipata kwa njia ya simu, labda simu kutokupokelewa au meseji kutokujibiwa. Ni vigumu sana kwangu kupokea kila siku na kujibu kila ujumbe wa simu. Na tena kutuma meseji inapotea haraka sana, kwa sababu meseji zinaingia nyingi.

Njia ya uhakika kabisa ya kuwasiliana na mimi ni kwa kunitumia email kwenye makirita@kisimachamaarifa.co.tz huwa nasoma na kujibu kila email ninayotumiwa. natenga muda wa kufanya hili hata kama nimebanwa kiasi gani.
Hivyo kama unahitaji kuwasiliana na mimi, niandikie email, nitakupa maelekezo mengine kwa njia ya email.
Huduma ambazo utaendelea kuzipata kila siku.

Pamoja na mimi kubanwa sana kwenye muda, kuna vitu ambavyo nitaendelea kufanya kila siku, hivi ni vitu nilivyochagua kufanya kila siku mpaka siku naondoka duniani. Kitu kikuu ni kuandika, nitaendelea kuandika kila siku, KILA SIKU. Kitu kingine ambacho lazima nifanye kila siku ni kusoma vitabu, kila siku lazima nijifunze kitu kipya, hata kama ni kwa dakika 10 pekee, kila wiki lazima nimalize kusoma angalau kitabu kimoja, na muda ukiruhusu vitabu viwili.

Huduma zifuatazo utaendelea kuzipata kila siku;
1. Makala kwenye AMKA MTANZANIA, kila siku ya wiki.

2. Makala kwenye KISIMA CHA MAARIFA, kila siku.

3. Tafakari na mafunzo kwenye KUNDI LA WASAP la KISIMA CHA MAARIFA, kila siku.

4. Utaendelea kupata vitabu mbalimbali, ukilipia unatumiwa au kuletewa ulipo. Tembelea www.mobileuniversity.ac.tz kupata taarifa za vitabu.

5. Kitabu, BIASHARA NDANI YA AJIRA ambacho kimechapihswa, utaletewa ulipo kama upo dar kwa kulipa elfu 10, kama upo mkoani utalipa elfu 15 na utasafirishiwa kwa njia ya basi. Malipo yafanyike kwa namba 0717396253 au 0755953887 kisha tuma ujumbe wa jina la kitabu na ulipo ili uweze kuletewa au kutumiwa.

Ushauri wangu kwako rafiki yangu.
Njia ya uhakika ya kuwa karibu nami kwa sasa ili tuweze kujifunza na kuwasiliana kwa urahisi ni kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. 

Kwa kujiunga utapata makala za kila siku na pia utaingia kwenye kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA ambapo utaweza kuniuliza chochote muda wowote. Kujiunga lipa ada ya mwaka tsh 50,000/= kwa namba nilizotoa hapo juu kisha nitumie ujumbe kwenye wasap namba 0717 396 253 nikupe maelekezo ya kujiunga.
Kama unahitaji tuwe na mazungumzo, ambayo ni muhimu sana, tuwasiliane kisha tutapanga muda wa kuongea kwa njia ya simu. 

Tafadhali yawe muhimu kweli, ili tuweze kutumia muda wetu vizuri.

Rafiki yangu, najitahidi kutumia muda wangu vizuri kuhakikisha naendelea kukupa maarifa na taarifa bora za kukuwezesha kufanya maamuzi bora ya maisha yako.

Karibu sana rafiki yangu tuendelee kuwa pamoja, tujifunze na kuhamasika. Karibu kwenye KISIMA CHA MAARIFA.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: