Hii Ndiyo Mifereji Nane (08) Ya Kipato Ambayo Kila Mtu Anayetaka Utajiri Anapaswa Kuwa Nayo.Habari za leo rafiki?

Naamini unaendelea vizuri na unaweka juhudi kubwa kuhakikisha kwamba maisha yako yanakuwa bora zaidi. Kama ambavyo nimekuwa nakusisitiza kila mara, kama maisha yako ni nyumba inayoungua, basi jua wewe pekee ndiye wa kuizima nyumba hiyo, hakuna msaada wowote unaokuja kwako kukusaidia kuzima nyumba hiyo. Hivyo maisha yako ni jukumu lako, kama kuna kitu chochote unachotaka au hutaki kwenye maisha yako, basi ni wewe mwenyewe wa kubadili kitu hicho.
Rafiki, mwanzoni mwa wiki hii nilitoa vitabu vitano bure kabisa vya Raisi mteule wa marekani na bilionea Donald Trump. Ni vitabu vizuri ambavyo vinatufundisha mengi kwenye safari yetu ya mafanikio. Je ulipata vitabu vile? Kama hukuvipata basi bonyeza maandishi haya na ufuate utaratibu.
Kwenye makala ya leo nataka nikurudishe darasani kidogo, na darasa nitakalokurudisha leo ni darasa la jiografia. Usiogope rafiki, siyo darasa kubwa, na sitakupa mtihani, nataka nikuoneshe tu jinsi asili inavyofanya kazi.
Ichukulie bahari, au maziwa makubwa, hivi ni vyombo vikubwa ambavyo vinaweka maji, si ndiyo? Je umewahi kuona bahari inakauka? Je umewahi kuona ziwa kubwa linakauka maji yake? Kwa hakika jibu ni hapana. Kwa nini maji hayo hayakauki ili hali kuna jua kali ambalo linayafanya yapungue kwa njia ya mvuke?
Jibu ni kwamba, bahari na maziwa makubwa, yanaendelea kupata maji kutoka kwenye vyanzo mbalimbali. Maji yaliyopo kwenye bahari yanapopata jua, yanageuka kuwa mvuke, hivyo yanapungua kidogo, lakini mvuke huu unaenda kutengeneza mawingu, mawingu yanaleta mvua, mvua zinakusanya maji kwenye vijito, vijito vinakuwa mito na mito inarudisha maji kwenye maziwa au bahari. Nimekuacha mahali? Rudia tena taratibu utaelewa.
Sasa hali hii ndiyo inayopaswa kutokea kwenye maisha yetu, hasa kwenye upande wa kipato. Kila mtu anapenda kuwa na utajiri, na kama hupendi kutumia neno utajiri, basi unapenda kuwa na uhuru wa kifedha, uweze kutimiza mahitaji yako yote kwa maisha yako yote.
Licha ya wengi kupenda utajiri, ni wachache sana ambao wanaijua kweli misingi ya utajiri na kuweza kuifanyia kazi. Wengi hawaijui misingi na hivyo kuivunja, kitu ambacho kinawazuia kupata utajiri wanaoutaka.
Msingi mmoja wa utajiri ni kuwa na vyanzo vingi vya kipato. Kwa lugha nyingine ni kuwa a mifereji mingi ya kipato. Kama tulivyoona kwenye mfano wa bahari na maziwa hapo juu, havikauki kwa sababu kuna vyanzo vingi vya maji vinavyoelekea kwenye bahari au maziwa makubwa.
Hivyo pia ndivyo inavyopaswa kuwa, kama unataka kipato chako kisikauke, basi lazima uwe na mifereji mingi ambayo inakuingizia kipato. Lazima uwe na vyanzo vingi ambavyo vinakuletea kipato, na hapa ndipo unapoweza kutengeneza uhuru wako wa kifedha.
Hatari ya kuwa na mfereji mmoja wa kipato ni kwamba inapotokea changamoto, basi inakuathiri moja kwa moja. Wote tunajua kila tunachofanya kwenye maisha yetu kina changamoto, iwe umeajiriwa, umejiajiri au unafanya biashara. Zipo changamoto kila siku ambazo zinakuwa tofauti na mipango yako. Changamoto inapotokea kwenye kile chanzo chako pekee cha kipato, inakuathiri kwa kiasi kikubwa sana, bila ya kujali una kipato kikubwa kiasi gani.
Kwa mfano, kama wewe ni daktari wa upasuaji, ambaye unalipwa labda milioni moja kwa kila upasuaji, na kila siku unafanya upasuaji mmoja una kipato kikubwa, si ndiyo? Lakini kama hiki ndiyo kipato pekee unachotegemea, una hatari kubwa sana. Kama itatokea ukaumwa na ukawa huwezi kufanya upasuaji, kipato chako kimekauka. Kama itatokea umepata ajali na ukakatwa mkono huwezi tena kufanya upasuaji, tayari kipato chako kimeathirika na huwezi tena kuendelea na maisha yako ya kawaida.
Hata kama wewe ni fundi ambaye unafanya kazi zako vizuri sana na unalipwa kiasi kikubwa, bado wewe ni masikini kama kipato chako pekee ni kupitia ufundi wako. Kama utakosa kazi, kipato chako kimekauka.
Hali ni hatari zaidi pale inapotokea kwamba umeajiriwa na chanzo chako pekee cha kipato ni mshahara. Inapotokea kazi imekwisha, unajikuta kwenye wakati mgumu sana kwa upande wa kipato.
Hata kama unafanya biashara, na unayo biashara moja pekee, kuna changamoto zinazoweza kutokea na zikaathiri biashara yako kwa kiasi kikubwa na hivyo kupelekea kipato chako kupungua.
Suluhisho la changamoto hii ya kipato.
Kwa kuwa hatuwezi kuzuia changamoto zote zinazoweza kutokea kwenye maisha yetu, tunahitaji kuwa na njia bora ya kuhakikisha kipato chetu kinaendelea kuwa kikubwa hata kama kuna changamoto tunazopitia.
Na njia pekee ya kufanya hivi ni kuwa na njia tofauti za kuingiza kipato. Tunahitaji kuwa na mifereji mingi ya kipato ili tunapopata tatizo kwenye mfereji mmoja, basi mifereji mingine iendelee kutuletea kipato. Huu ndiyo uhuru wa kifedha kwenye maisha yetu.
Je unahitaji mifereji mingapi ya kipato ili kuwa tajiri?
Unahitaji angalau mifereji saba ya kipato ili uweze kufikia utajiri, ili uwe na uhuru wa kifedha. Ipo mifereji nane ambayo kila mtu anaweza kuitumia kutengeneza kipato kwenye maisha yake. Wewe unahitaji angalau mifereji saba kati ya mifereji hiyo nane.
Je unawezaje kujitengenezea mifereji hiyo nane ya kipato?
Kwenye kitabu changu kipya, BIASHARA NDANI YA AJIRA, nimeeleza kwa kina kuhusu mifereji hii nane ya kujitengenezea kipato. 
Nimeeleza kwa mifano namna unavyoweza kuanza kujitengenezea mifereji hii ya kipato. Pia nimeeleza mifereji minne unayoweza kuanza nayo leo, ndiyo yaani LEO HII unaweza kuwa na mifereji minne ya kukuingizia kipato, kwa kuanzia hapo hapo ulipo, bila hata ya kufanya mabadiliko makubwa kwenye maisha yako.
Sitaweza kuielezea mifereji yote nane kwenye makala hii, hivyo nitakusihi sana wewe rafiki yangu upate kitabu hichi cha BIAHSARA NDANI YA AJIRA, ni kitabu kizuri sana kwa kila mtu anayetaka kuanzisha biashara na kupata uhuru wa kifedha. Iwe umeajiriwa, umejiajiri, unafanya biashara au huna kazi kabisa, soma kitabu hiki na utapata mawazo mazuri ya jinsi ya kuongeza kipato chako.
Jinsi ya kupata kitabu cha biashara ndani ya ajira.
Kitabu hiki kinapatikana kwa bei ya tsh 10,000/=
Kama upo dar piga simu namba 0654426721 na utaletewa kitabu ulipo na kukilipia ukishakipokea.
Kama upo mkoani, unahitaji kulipia kitabu na nauli ya kukisafirisha kwa basi au kwa njia ya posta. Hivyo utalipa fedha tsh 15,000/= (elfu 10 ya kitabu na elfu 5 ya nauli) kupitia namba 0717 396 253 au 0755 953 887 kisha tuma majina yako, namba ya simu, mkoa ulipo na gari ambayo ungependa tutumie kukusafirishia kitabu, kisha tutakusafirishia.
Pia tuna baadhi ya mawakala kwenye maeneo yafuatayo; Njombe 0769761297, Songea 0782744713, Zanzibar 0714312924, Mbeya 0759051543, Mtwara 0784503076, Mwanza 0719756365. Kama upo mkoa mwingine ambao haujatajwa hapo piga simu 0654426721.
Pata kitabu chako leo cha BIASHARA NDANI YA AJIRA ili uweze kujitengenezea mifereji nane ya kipato.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: