Hongera rafiki yangu kwa nafasi hii nzuri sana ya leo.
Na siku nyingine nzuri ambapo tumepata nafasi ya kipekee ya kwenda kuweka juhudi zaidi kwenye kile tulichochagua kufanya. Tutumie nafasi hii ya leo vizuri rafiki.

img_20161112_091656

Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu SELFISHNESS yaani UBINAFSI.
Ili tuweze kuendelea, na ili tuweze kuwasaidia wengine, tunahitaji kiwango fulani cha ubinafsi, kila mmoja wetu.
Ndiyo, tunahitaji ubinafsi ya kufanyia kazi yale muhimu kwenye maisha yetu ili tuweze kuendelea kufanya makubwa kwa wengine pia.
Bila ya ubinafsi, tutashindwa kutoa mchango bora kwa wengine.

Kwa mfano huwezi kuwasaidia wengine kama afya yako ni mbovu na unaumwa.
Huwezi kumsaidia masikini kama na wewe ni masikini.
Unahitaji kufanyia kazi afya yako kila siku ili uweze kuwa na afya imara na kuweza kuendelea kufanya yake muhimu.
Unahitaji kuweka juhudi kubwa ili kuwa sawa kifedha ndiyo uweze kuwa wa msaada kwa wengine.

Katika kujitoa kwako kuwasaidia wengine usisahau kufanya yale muhimu kwako, yatakayopelekea kuendelea kuwa na afya bora na uhuru wa kifedha pia.
Hakuna ushujaa kwenye kuharibu afya yako kwa kisingizio ulikuwa bize kuwasaidia wengine. Au kuwa masikini kwa sababu ulikuwa bize kuwasaidia masikini.
Weka kipaumbele kwako pia, ukishakuwa sawa, utaweza kuwasaidia wengine nao kuwa sawa.

Nakutakia siku njema sana.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
http://www.makirita.info