Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Hii ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa kwa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ili tuweze kupata matokeo bora kabisa.

IMG_20170102_073855

Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu KUFANYA KILA SIKU….
Kama kuna kitu muhimu sana kwenye maisha yako,
Kama kuna kitu ambacho unataka kuwa bora sana,
Kama kuna kitu ambacho unataka dunia nzima ikujue kupitia kitu hicho,
Kama kipo kitu ambacho kinawaka ndani yako,
Basi unastahili kufanya kitu hiki kila siku.
Ndiyo unahitaji kufanya kila siku, ili kuwa bora zaidi na ili kufika mbali zaidi.
Usikubali siku yoyote ipite ukiwa hujafanya kitu hicho.
Siku yako itakuwa haijakamilika ikiwa hujafanya kile ambacho ni muhimu kwako.

Swali ni je, kipi muhimu kwako ambacho lazima ukifanye kila siku?
Iwe ni kwenye kazi yako, biashara yako na hata maisha kwa ujumla.
Uzuri wa kufanya kila siku ni kwamba mafanikio hayawezi kukukimbia, kwa sababu utaelewa kila eneo la kile unachofanya.
Chagua kile utakachofanya kila siku katika maisha yako.

Nakutakia siku njema sana ya leo rafiki yangu.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz