Hongera rafiki kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora kabisa.

Tutumie nafasi ya leo vizuri ili tuweze kufanya makubwa.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambao unatuwezesha kufanya nakubwa kwenye maisha yetu.
Leo tutafakari kuhusu KUISHI SASA….
Biashara yetu kubwa hapa duniani ni kuishi, yaani kuishi kwetu ndiyo msingo muhimu wa chochote tunachofanya.
Lakini kuishi kimekuwa ndiyo kipaumbele cha mwisho kwetu, hasa kuishi kwenye wakati husika.
Imekuwa ni rahisi kuishi jana kwa kuangalia yapi u eshindwa kufanya na wapi umekosea au kukosewa.
Pia ni rahisi kuishi kesho, kwa kujidanganya kwamba kesho utafanya vizuri zaidi.
Lakini kuishi sasa, kuwa pale ulipo, ndiyo mtihani mgumu kabisa.
Kuishi sasa, kwenye wakati uliopo ni kitu kinachokuhitaji wewe uweze kuyadhibiti mawazo yako.
Uweze kuacha kuhangaika na jana au kesho, na kupeleka mawazo yako yote kwenye kile unachofanya kwenye wakati husika.
Anza kuishi sasa,
Dhibiti akili yako, ili isikuhangaishe kwa jana na kesho, badala yake peleka mawazo yako yote kwenye kile unachofanya.
Na hapo utaweza kufanya kwa ubora zaidi.
Nikutakie siku njema sana ya leo.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT.