Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kupata matokeo bora kabisa.

img-20161217-wa0002
Ni wajibu wetu kuitumia vizuri siku ya leo ili kuweza kufanikisha kile tunachotaka.
Ni kwa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tutaweza kufanya makubwa sana leo na kila siku.

Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu SLIGHT EDGE….
Kinachowatofautisha wale wanaofanikiwa sana na wanaoshindwa siyo kitu kikubwa, bali tofauti ndogo sana.
Kwa mfano ukichukulia mashindano ya mbio, mshindi wa kwanza na wa pili wanaweza kutofautiana kwa sekunde 10 au hata dakika moja, lakini mshindi wa kwanza anapata zawadi zaidi hata ya mara mbili ya anayopata mshindi wa pili.
Tofauti ya watu hawa wawili ni kitu kidogo sana, yaani kuna ncha ndogo sana kati ya anayeshinda na anayeshindwa.

Tuchukue mfano mwingine,
Mtu mmoja akiwa anajiwekea pembeni shilingi elfu moja kila siku, wakati mwingine hafanyi hivyo, baada ya miaka michache, labda 5 au 10, aliyekuwa anajiwekea eldi moja atakuwa mbali mno ukilinganisha na ambaye alikuwa haweki chochote.

Hivyo basi rafiki, huhitaji kuwa tofauti kabisa na wengine ili kufanikiwa, bali unahitaji kujitofautisha kidogo sana, halafu kuendeleza tofauti hiyo kila siku, kila siku.
Ni ncha ndogo sana inayowatofautisha washindi na wengine, itumie vizuri ncha hiyo.

Chagua vitu ambavyo utakuwa unafanya kila siku kwenye kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla. Vinaweza visiwe na tofauti kubwa sasa, ila kadiri unavyofanya vinajenga tofauti.
Kila mtu anahitaji SLIGHT EDGE yake ili kuweza kufanya makubwa na kufanikiwa.

Nakutakia siku njema sana ya leo.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT.