Ukweli Na Uongo Uliojificha Kwenye Biashara Ya Mtandao (Network Marketing)

Habari rafiki,

Kila mara nimekuwa napata ujumbe kutoka kwa marafiki zangu wakiomba ushauri kuhusiana na baadhi ya kampuni zinazofanya biashara kwa mfumo wa mtandao, yaani NETWORK MARKETING.

Kumekuwa na kampuni nyingi zinaibuka kila siku, ambazo zinajinadi kufanya biashara kwa mfumo huu, lakini nyingi zinajificha tu kwenye huu mfumo, siyo halali na ni mchezo wa upatu au kama unavyojulikana kwa kiingereza PYRAMID SCHEME.

Unaikumbuka DECI? Ilikuwa habari ya mjini na kila mtu alikimbilia kule, waelewa walionya lakini wengi hawakusikia, wakaishia kuumia. Ikaja kampuni nyingine inaitwa TELEXFREE, hii nayo iliahidi watu kutajirika bila ya kufanya chochote, kwa kuunganisha watu tu. Niliwaonya baadhi ya marafiki zangu kujiepusha nayo, wengi hawakusikia na haikuchukua muda waliumia.

Sasa naona kampuni nyingi zaidi zinakuja kwa mgongo huu wa network marketing wakati ni michezo ya upatu. Nimekuwa nawashauri marafiki wanaoniomba kuhusiana na makampuni haya. Lakini maombi yamekuwa ni mengi kila siku. Hivyo nimekaa chini na kuandika kitabu, ambacho nimeielezea biashara hii kwa kina, kuanzia misingi yake, fursa zilizopo kwenye biashara hii pamoja na misingi ya kuifanya.

Ndani ya kitabu hichi, nimeeleza kwa kina mambo kumi ya kuzingatia katika kuchagua kampuni ya kujiunga nayo kufanya biashara hii, ambayo ukiyajua hayo, hutakuja kudanganywa wala kutapeliwa kama wengi wanavyofanyiwa sasa.

Pia nimeeleza namna ya kutofautisha biashara halali ya network marketing na mchezo wa upatu yaani pyramid scheme. Kuna eneo moja kuu la kuangalia kwenye biashara na hilo pekee linatosha kukufahamisha kama ni biashara halisi au mchezo wa upatu.

Kitabu hichi kinajulikana kama IJUE BIASHARA YA MTANDAO (NETWORK MARKETING) na kitapatikana kwa mfumo wa nakala tete, yaani softcopy (pdf) na kitatumwa kwa njia ya email. Utaweza kukisomea kwenye simu yako, tablet yako au hata kompyuta yako.

Kitabu hichi kitatoka rasmi tarehe 01/06/2017, lakini nimekupa taarifa hii mapema ili uweze kupata fursa nzuri ya kukipata kitabu hichi. Kujua fursa hiyo fungua kiungo hichi; https://goo.gl/1YXp4q

Nimalize kwa kukuambia rafiki yangu, kuuelewa mfumo huu wa biashara kwa kina, kunaweza kukusaidia sana hata kwenye biashara zako za kawaida, kwa sababu uhai wa biashara yoyote ile ni mauzo, na njia ya mtandao ni moja ya njia za uhakika za kusambaza bidhaa au huduma za biashara yako. Hivyo hata kama hufanyi biashara ya mtandao, au huna mpango huo, bado unaweza kutumia maarifa haya kuboresha biashara yako.

Pata fursa hii ya kuijua biashara ya mtandao na namna ya kuitumia kwa mafanikio, fungua kiungo hichi; https://goo.gl/1YXp4q

Nikutakie wakati mwema rafiki yangu,

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: