Swali Muhimu Kuhusu Fedha; Wazazi Wako Walikufundisha Nini Kuhusu Fedha?

Habari za leo rafiki?

Leo nina swali muhimu sana kwako kuhusu fedha. Hili ni swali ambalo limebeba msingi ambao upo hapo ulipo sasa kifedha. Swali lenyewe ni; wazazi wako walikufundisha nini kuhusu fedha? Hili ni swali muhimu kuliko maswali mengine yote unayoweza kujiuliza kuhusu fedha.

 

Iko hivi rafiki, tunapozaliwa, tunakuwa hatujui chochote kuhusiana na hii dunia. 

Tunachokuwa tunajua ni kimoja tu, kuhakikisha hatufi, yaani tunapona. Hivyo tunakuwa tunajua kunyonya ili tuweze kula na kuishi (ndiyo maana utamwona mtoto mchanga ananyonya vidole akiwa na njaa) na pia tunakuwa tunajua kujikinga na hatari (ndiyo maana mtoto akisikia sauti kali anajikunja). Mengine yote tunafundishwa hapa duniani, na wanaochukua nafasi kubwa kwenye kufundishwa huko ni wazazi au walezi wetu.

Hawa hawatufundishi tu kwa kutuambia, bali wanatufundisha kwa matendo kwa kuwa tunaona wazi kile ambacho wanafanya au hawafanyi.

Kwa kuwa fedha ni moja ya maeneo muhimu sana kwenye maisha yetu, leo hebu tafakari kwa kina kipi umejifunza kwa wazazi na walezi wako kuhusu fedha. Iwe ni namna alivyokuwa anakuambia, iwe ni namna maisha yake alikuwa anayaendesha, tafakari yapi uliyojifunza kuhusu fedha.

Watu wengi tunatokea kwenye familia ambazo hazikuwa na uwezo mkubwa kifedha. 

Wengine tunatokea kwenye familia masikini kabisa na wapo wachache wanaotokea kwenye familia zenye uwezo mkubwa kifedha. Lakini pamoja na utofauti huu wa tulipotokea, bado elimu ya fedha tuliyopata kwa wazazi na walezi wetu siyo bora. Bado tunakosa misingi muhimu ya kifedha ambayo itatuwezesha kujijengea uhuru wa kifedha na kuwa na maisha bora.

KWA WALIOTOKEA FAMILIA MASIKINI; FEDHA NI MBAYA, MATAJIRI NI WATU WABAYA.

Wale ambao wamelelewa na wazazi au walezi ambao wameishi maisha yao yote kwenye umasikini, ujumbe mkubwa wanaoondoka nao kuhusu fedha ni kwamba fedha ni mbaya na matajiri ni watu wabaya. Watu hawa kupitia wazazi wao wamejifunza kwamba umasikini wao unasababishwa na matajiri wachache, ambao wanawadhulumu haki zao. Wanaamini mtu akiwa na fedha anakuwa na roho mbaya, kwa sababu labda kuna ndugu yao amewahi kuwa na fedha na akawa hafanyi kama wanavyotaka wao.

Kwa mtazamo huu kuhusu fedha, watu waliokuzwa kwenye umasikini huishia maisha ya umasikini. Kwa sababu wanachukia fedha na utajiri, hivyo kwa kila namna watahakikisha wanapingana na utajiri. Wakipata fursa ya kutengeneza fedha ya kuweza kuwafikisha kwenye utajiri, kinatokea kitu cha kuwaondoa hapo, kwa sababu imani yao ni tofauti.

SOMA; Sheria Tatu(3) Muhimu Za Fedha Ambazo Hujawahi Kufundishwa Popote.

Umewahi kuona mtu ametoka familia masikini, labda amesoma akapata kazi, au amefanya biashara na kuanza kupata mafanikio, halafu anaharibu kila kitu, kazi anafukuzwa au biashara inakufa? Wengi husema labda wamelogwa au wana laana. Ukweli ni kwamba imani yao kuhusu fedha ambayo wamejifunza kwenye maisha yao yote ipo kazini. Na inahakikisha wanakuwa vile wanavyoamini kuhusu fedha. Watapata nafasi nzuri mno, lakini wanaishia kuziharibu na maisha yao yanakuwa magumu.

WALIOLELEWA KWENYE FAMILIA ZA UWEZO WA KAWAIDA; FEDHA NI 
NGUMU, FEDHA HAILETI FURAHA.

Wale ambao wamelelewa kwenye familia zenye uwezo wa kawaida au uwezo wa kati, nao wamekuwa na imani yao tofauti kuhusu fedha. Wazazi ambao wana uwezo wa kati kifedha, wana maisha magumu sana kifedha. Kwa sababu wanakazana kuondoka au kutokurudi kwenye umasikini, na wakati huo wanakazana kwenda maisha ya juu ya utajiri. Hivyo maisha yao yanakuwa magumu, kutokana na ukubwa wa mahitaji na ukomo wa kipato.

Wazazi hawa hujikuta wanafanya kazi kupitiliza lakini bado fedha hazitoshi. Wanakuwa na mikopo mingi na vipato vyao vimekuwa havikutani. Watoto wanaolelewa kwenye familia hizi huondoka na imani hii kuhusu fedha, kwamba fedha ni ngumu sana, ndiyo maana wazazi wao wanateseka, na fedha haileti furaha, kwa sababu hawajawahi kuwaona wazazi wao wakiwa na furaha ya muda mrefu. Watoto hawa pia wanakua na dhana kwamba kama fedha haitoshi matumizi, basi wewe kopa, usihangaike kujisumbua, kopa na ukipata fedha utalipa. 

Hapo ndipo unapotengenezwa utumwa mkubwa kwenye maisha yao.

Watoto wanaotokea familia hizi wamekuwa wanakwenda na wakati mgumu kifedha. Mara nyingi wanakuwa wameaminishwa kuajiriwa ndiyo njia pekee ya kufanikiwa kwenye maisha, kwa sababu mara nyingi wazazi wao wanakuwa waajiriwa. Hukazaniwa kusoma sana na kupata kazi, na hata kama kazi isipokuwa nzuri kwao, hawawezi kuiacha, maana wazazi wanaweza hata kuwaachia laana. Kazi ni kitu wanakiamini sana, na hata kama hailipi, wanaamini kuwa na kazi ni usalama. Hili ni kundi limezalisha watu wengi ambao wamekubali utumwa kwa hiari yao wenyewe. Na kwa zama hizi ambapo ajira ni ngumu, kundi hili lina wakati mgumu sana.

WALIOKULIA FAMILIA ZA KITAJIRI; HUNA HAJA YA KUHANGAIKA, MIMI MZAZI WAKO NITAKUHAKIKISHIA KILA KITU.

Kundi la tatu ni la wale ambao wamekulia familia za kitajiri hasa. Zile familia ambazo fedha siyo tatizo, mtoto hajawahi kuomba chochote akakosa. Mtoto anapewa kila anachotaka, maisha ya wazazi yanaonekana kuwa mazuri kabisa.

Tatizo kubwa kwenye familia hizi huwa ni wazazi kutaka kuwahakikishia watoto wao uhuru wa kifedha. Hivyo wazazi hukazana kuwapa watoto kila kitu. Mtoto anaanza maisha tayari ana nyumba, magari, ana fedha za kutosha benki na miradi inayozalisha.

SOMA; Hizi Ni Sababu Kwa Nini Baadhi Ya Watu Wanaopata Fedha Nyingi Huishia Kufa Masikini, Na Hatua Za Wewe Kuchukua.

RMambo huwa mazuri sana wakati wote ambapo mzazi yupo na hivyo kusimamia mambo vizuri. Changamoto huibuka pale mzazi anapofariki, hapa sasa mtoto anaachwa na mali nyingi ambazo hajui msingi wake hasa ni nini. Kinachotokea ni mali zote kumfuata aliyezitafuta, yaani kila kitu kinakufa. Utashangaa watoto wanauza kila kitu, wengine mpaka nyumba wanazokaa. Unaweza kushangaa wana matatizo gani, lakini ukweli ni kwamba mtazamo wao kuhusu fedha ni kuzipata na kuzitumia, na hawana msingi wa kuzitafuta na kuzizalisha zaidi.

Katika makundi yote hayo matatu, ambapo kila mmoja wetu anaangukia kwenye kundi moja wapo, watu hawana elimu ya msingi kabisa ya fedha, na hilo ndiyo limekuwa tatizo kwenye maisha ya wengi.

KARIBU UJIFUNZE ELIMU YA MSINGI YA FEDHA MWEZI WA SABA.

Mwezi wa saba mwaka 2017, nimeandaa semina ya ELIMU YA MSINGI YA FEDHA (BASIC FINANCIAL EDUCATION). Hii ni semina ambayo nitaiendesha kwa njia ya mtandao, kupitia kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA. Unaweza kushiriki semina hii popote pale ulipo Tanzania na hata duniani. Huhitaji kusafiri au kuacha kazi zako, unachohitaji ni kutenga muda wako mfupi kila siku wa kufuatilia semina hii.

Ili kuweza kushiriki semina hii, unapaswa kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA. Kwa kuwa mwanachama unaweza kusoma makala nyingi kwenye blog ya KISIMA CHA MAARIFA, ambayo ni ya wanachama tu, pia unakuwa kwenye kundi la wasap ambapo kila siku unapata tafakari na kila jumapili tunakuwa na madarasa ambapo tunajifunza mambo muhimu kuhusu mafanikio.

Kuwa mwanachama unapaswa kulipa ada ya mwaka ambayo ni tsh 50,000/= ambapo ada hii inakwenda kwa mwaka mmoja tangu siku unayolipa. Ada inalipwa kwa namba 0755 953 887 au 0717 396 253 majina Amani Makirita. Ukishalipa ada tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba 0717396253 na nitakuweka kwenye kundi.

Semina hii ya ELIMU YA MSINGI YA FEDHA, siyo semina ya kukosa kwa mtu yeyote yule ambaye yupo makini na maisha yake. Fanya malipo leo ili uweze kujihakikishia nafasi ya kushiriki semina hii ya kipekee sana kwako.

Karibu sana tujenge msingi imara wa kifedha kwetu na kwa vizazi vyetu. Chukua hatua kwa kufanya malipo leo ili kuweza kushiriki semina hii nzuri.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu, unayoweza kuitumia kutengeneza kipato, BONYEZA maandishi haya.

Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: