Habari rafiki?

Kama nilivyokueleza kwenye email iliyopita, wapo watu ambao walipenda kushiriki semina ya ELIMU YA MSINGI YA FEDHA lakini hawakupata nafasi hiyo. Lakini kadiri semina ilivyokuwa inaenda, nimeona namna ambavyo watu wengi wanakosa elimu hii ya msingi kabisa, na hilo kupelekea maisha yao kuwa magumu kuliko yanavyopaswa kuwa.Nilikuambia naandaa utaratibu maalumu wa watu kuweza kujifunza na kupata elimu hii. 

Napenda kila mtu aliye makini na maisha yake kwa upande wa fedha, apate elimu hii muhimu sana.

Hivyo nachukua nafasi hii kukujulisha kwamba mpango niliokuwa naandaa umeshakamilika na masomo yataanza siku siyo nyingi.

Nakupa taarifa hii kama ulikosa mafunzo haya na ungependa kuyapata, basi jibu email hii kwa kusema ulikosa mafunzo na unataka kuyapata. Au tuma email kwenda amakirita@gmail.com ukisema ulikosa semina ya ELIMU YA MSINGI YA FEDHA lakini sasa hivi upo tayari kuyapata. Nitakutumia maelekezo yote kamili.

Nakusihi uchukue hatua sasa, kwa sababu mpango huu utaanza mapema sana na watakaokosa sasa watakuwa wamechagua wenyewe kukosa, na siyo sababu nyingine yoyote.

Nina imani kubwa kwamba semina hii itakusaidia sana, kabla hata haijaisha, utaanza kuona maeneo ambayo unapoteza fedha zako na kuziokoa, kama ambavyo mshiriki wa semina hii alivyotushuhudia hapo chini;

Kocha Asante kwa ubatizo wa leo.

Nimeenda bank Nimepata statement kwa mwezi juni pekee nimepoteza sh 32,000
Maana mtindo wangu nikiwa na shida hata inayoweza kusubiri, navuta hela from bank to mpesa then wakala. Nina ving’amuzi viwili chumbani na sebuleni kila mwezi nalipia azam na star, muda wetu ni mdogo wa kuangalia TV hata Habari ni kwa kubahatisha. Housegirl ndio yuko nayo bize tena yuko smart ikiisha anakuhimiza kulipia. Watoto wana shinda shule khaaa!

Hapo kwenye bando ndo tuna malizia huko hela. Saa nyingine unaweka kifurushi dk hata hajapiga simu hadi ina Expire. Khaaa! Kumbe Ndio maana wengine hudhani kuna chuma ulite.

Ningepata elimu hii nikiwa na miaka 30 labda ningeshafikia au kukaribia uhuru wa kifedha. Ila Mungu bado ananipenda. Nimeandika Jamani ni hasara kubwa Napata bila kujua. Kweli tunaangamia kwa kukosa maarifa haya ila kwa ubatizo huu tumeponywa. 

Ndugu zangu leo nimejipongeza Nimeenda sokoni nikanunua Vitu ambavyo Nimeandika tu. Nikitamani kitu nikaiambia nafsi yangu Leo hiyo sio mahitaji yangu Nikitoka sokoni salama. Jaribu lingine nililoshinda ni wapo watu wanaotembelea maeneo ya kazi na bidhaa akikuhamasisha kununua na kusema hela hadi mwisho wa mwezi utanipa nikashinda sijachukua.

KOCHA HONGERA KWA KAZI KUBWA UNAYO FANYA KUTIBU AKILI ZETU. – Sara Kimweri.

Maoni ya aina hiyo yapo mengi mno, nikisema niyatume yote hatutamaliza. Ila ni maoni ya aina hiyo yamenifanya nitafakari kwa kina na kuona kama sitaitoa elimu hii kwa wengi, basi nitakuwa nawanyima kitu kizuri. Kwa sababu kama wapo watu wamenufaika nayo, ina maana wengi zaidi watanufaika.

Na hii ndiyo sababu nimeona nikupe nafasi hii ya kipekee kabisa ya kupata mafunzo haya ya semina.

Nimeandaa kundi maalumu kwa ajili ya mafunzo tu, ambapo unaweza kujiunga na kupata mafunzo haya ya semina pekee. Badala ya mpango wa awali kwamba lazima ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA, sasa hutahitaji kufanya hivyo, utajiunga na KUNDI LA SEMINA pekee.

Tuma email sasa kwenda amakirita@gmail.com kupata nafasi hii ya kushiriki mafunzo haya.

MUHIMU; Kama umeshatuma email ya kusema hujashiriki mafunzo na ungependa kushiriki, usitume tena. Fanyia kazi maelekezo uliyopewa ili uweze kushiriki semina hii.

Karibu sana rafiki yangu, sitaki ukose tena mafunzo haya.
Rafiki yako,
Kocha Makirita Amani,