Wengi tumekuwa tukitafuta mbinu na siri za kufanikiwa maishani na kujiuliza sana maswali mengi ya nifanye nini ili niweze kufanikiwa kwenye maisha. Na kuna wakati tumekuwa tukijiuliza labda tumekosa nini, hadi tukashindwa kufanikiwa sana.
Hiyo haitoshi tumekuwa tukifiri labda hatuna kipaji cha aina fulani na tumekuwa hatujui hata vipaji tulivyonavyo ni vya aina gani. Matokeo yake tumekuwa tukihalalisha kabisa kwamba pengine tunashindwa kwa sababu hatuna kipaji.
Lakini hata hivyo, leo nataka tuambizane ukweli kwamba kipo kitu ambacho ukiwa nacho na ukakifanya utafanikiwa tu, sio lazima uwe na kipaji pekee. Hiki ni kitu ambacho hata wale unaowaona wana vipaji wanatumia sana kufanikiwa kwao.
Kitu hiki ambacho unatikiwa nacho ili uweze kufanikiwa si ingine bali ni NIDHAMU BINAFASI. Nikiwa na maana unatakiwa uwe na nidhamu binafsi kwenye kazi yako, unatakiwa uwe na nidhamu binafsi kwenye pesa na kila eneo.
Inapotokea ukaanza kukosa nidhamu katika kitu chochote kile, uwe na uhakika hapo ndipo kushindwa kwako kunanza kutokea. Mafanikio yote makubwa yanaanza kwa kujenga nidhamu binafsi na si vinginevyo.
Kama unafikiri natania kuanzia leo jiwekee nidhamu binafsi ya kufanya kazi kwa masaa mengi zaidi na enddelea na tabia hiyo kwa muda wa miaka mitano mfululizo, halafu niambie ni kitu gani ambacho kitatokea kwako, lazima utafanikiwa.
Hakuna kitakachoshindikana kwako kama unaweka juhudi lakini huku unaendeleza nidhamu binafsi. Unapokuwa na nidhamu binasfi ni kama vile umepanda gari la kukupeleka kwenye mafanikio yako.
Hiyo ikiwa na maana kwamba, ukiona huna nidhamu kwenye ,maisha yako, basi elewa kabisa utakuwa ni sawa na yule mtu aliyeanza kushuka kwenye chombo cha kumpeleka kweye mafanikio yake na kuamua kutembea kwa miguu, mtu huyo atafika kweli?
Kufikia mafanikio itakuwa kazi kubwa sana kwako na itakuwa kazi ambayo nikwambie tu hutaweza kuifanikisha kama tu, utaendeleza mchezo wa kuishi maisha yakutokuwa na nidhamu binafsi.
Nidhamu binafsi ni silaha tosha ya mafanikio yako, nidhamu binafsi ni chombo tosha cha kukupeleka kwenye mafanikio. Chohote ukifanyacho chagau kukifanya kwa nidhamu ya hali ya juu, tena na kwa nidhamu endelevu kitu hicho kitafanikiwa.
Uelewe kukosa nidhamu ni sawa na mtu ambaye amechagua kwenda safari ya umbali mrefu sana kwa miguu. Hata wewe kama umechagua maisha ya mafanikio lakini huna nidhamu binafsi, ni ngumu sana kufanikiwa.
Ni wakati wako wa kukaa chini na kujikagua na kuangalia ni maeneo yapi ambayo huna nidhamu binafsi. Je, huna ndhamu binafsi katika eneo la pesa au huna nidhamu katika matumizi yako ya muda?
Fanya ufanyanyacho, lakini tambua nidhamu ni msingi mkubwa wa mafanikio yako leo na hata kesho.
Nikutakie kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa na endele kutembelea www.amkamtanzania.com kujifunza kila siku.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,